Chadema yawezekana tulibebwa na udhaifu wa makamba na tambwe hizza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yawezekana tulibebwa na udhaifu wa makamba na tambwe hizza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkono, Dec 4, 2011.

 1. M

  Mkono JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tangu uchaguzi mkuu umalizike mwishoni mwa mwaka jana nimekuwa sielewi vizuri movement za chama changu kuanzia tulivyoyapokea matokeo ya urais na kilichofuatia,kuna hili la umeya wa Arusha nafikiri hata hii hatua tuliyofikia ni jitihada binafsi za mh LEMA hasa tukikumbuka kuna kipindi zilishatoka habari za muafaka kabla Mh Lema hajapinga vikali,na sasa kuna hili la mswaada wa katiba mpya hatua ya kwanza tuliiweza ila hapa mwishoni tumecheka japo wengi hatupendi kukiri hivyo kama ilivyo ngumu kwa CCM kukiri kuwa chama chao kipo hatarini kupoteza utawala.Ni kwa nini tumefika hapa ?
  1.CHADEMA tumekuwa tukisubiria makosa ya CCM kuongeza mtaji wa wanachama bila kuwa njia mbadala ,na hili linajidhihilisha baada ya akili za mizaa toka kwa Yusuph Makamba kukaa pembeni hata kama MUKAMA sio mzuri sana ila anamzidi HUYO msambaa hali ni hiyo hiyo kwa NAPE na TABWE HIZA japo madhala ya NAPE kwa chama yanaweza kuwa makubwa sana siku za usoni
  2.Kuna tetesi kuwa mikakati mingi ya Chadema ilitengenezwa pale chuo kikuu UDSM hivyo pengine kuondoka kwa PROF BAREGU kunaweza kuwa ndo athari ya tunachojiuliza.
  3.Mgomo baridi ndani ya viongozi wa juu wa chama hili linaweza kutokana na kutoridhika kwa baadhi mgawanyo wa mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi hiki rejea yule mama wa KIGOMA aliyehamia NCCR muda mfupi baada ya kupatikana wabunge wa viti maalum
  4.Usalama wa taifa umeamua kutimiza wajibu wake kwa kuwaondoa watu walio kuwa wanasaidia upinzani huku wakiwa ndani ya system ;huyu namtolea mfano tu sina hakika kama aliwahi kuusadia upinzani ila watu wanamna yake ''TIDO MHANDO''
  5.Mwisho japo siyo mwisho kabisa ni M/kiti MH MBOWE tangu awe mbunge amejitahidi sana kujionyesha eti yeye ni mtu mstarabu sana hadi kufikia kujionyesha kama anatafuta sifa kutoka upande wa pili yaani CCM matoleo yake maamzi yote ya chama yanalenga kutoichukiza CCM na SERIKALI yake nafikiri alipaswa kuishi kama alivyo na si kuiga.
   
 2. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wewe si Mwana Chadema,umetumwa kupandikiza huo UPUUZI ili uwa aminishe watu UJINGA huo.Kwenda zako huko!
   
 3. M

  Mkono JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mwanachama ni nani ?
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Tapeli mkubwa wewe!
   
 5. M

  Mkono JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ukituliza akili utaelewa nachomanisha
   
 6. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Kawambie waliokutuma kuwa Hatudanganyiki kilahisi hivyo. Hoja hizi ni mfilisi.
   
 7. M

  Mkono JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ukituliza akili utagundua nachomanisha
   
 8. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  hoja hazina mshiko, umbea umbea tu.
   
 9. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #9
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Katika uchambuzi wako kuna sehemu nyingi umeingia chaka.

  1.0 Tido Mhando hakuwa anapendelea upinzani bali alikuwa anatekela weledi. CCM haioendi weledi badala yake imeendekeza mbeleko katika tasnia hiyo!!!!!
  2.0 Kuhusu Mbowe, Prof. Baregu hayo ni majungu ya wazi. Naona himjui kamanda Mbowe wewe. Nakujuza katika watu ambao siyo wanafiki katika CDM na wanaogopwa sana na serikali na CCM kwa ujumla wake ni Mbowe, Lissu na Slaa. Zitto haaminiki sana.
  3.0 Kuhusu CDM kubebwa na akina Makamba ni uongo wa mchana. CCM inajutia kuwachagua watu ambao wamekuwa mzigo kwa chama badala ya kukisaidia!! Mkama hana mvuto wala ushawishi katika chama, ni muongo na pale alisema habari ya makomandoo. Makamba asingeweza kusema upuuzi kama ule.
  Nape wala siitaji maelezo.

  Nimalizie kwa kusema wewe si mwanaCDM bali chui katika kondoo.
   
 10. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  nimetuliza akili nimegundua kuwa hamaanishi alichoandika.

  Wewe umegundua nini?
   
 11. T

  Topical JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  wala hamjui watu wasiotisha eti mbowe..

  kalagabao...aisee serikali haina tabu na mshirika huyo..ana matundu mengi sana ya kumbinya..

  Lakini huo ndio uzuri wa chadema fans..hawajui candidate mzuri..faida kwa ccm..
   
 12. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Shukuruni mna dola tu ambayo bado haijaiamini CDM, system ipo tayari CCM itawale wakati inajua mapungufu yake kiutendaji na kuua nguvu ya umma.

  Lakini hilo halina mashaka kabisa, ngoja nishikustue kumbe Mbowe ni kitisho kwa serikali yako maana hamchelewi kum Mwakyembe nyie.
  Nafuta kauli yangu Mbowe ni mtori sana anafanana na Shibuda kabisa. Nakuongozea Mbowe ni mnafiki sana, mwizi, bepari na mnyonyaji.
  Sawa Topical?
   
 13. M

  Mkono JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  rudia vizuri pale kwenye mf. Tido usiwahi kujibu tuuu!
   
 14. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #14
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hebu elewa Mkono, ni Tido Mhando hakufukuzwa pale TBC1 kwa kuoendelea upinzani bali Tido alikuwa ni mtu anayetekeleza weledi (profesional), serikali haipendi hilo na ndiyo maana walimuundia zengwe gavana wa banki kuu Rashid ili wafanye ufisadi.
  Hiyo ndiyo CCM bana.
   
 15. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #15
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ni mwenye Kadi ya uanachama na kulipia ada ya uanachama kila kipindi,mwenye mapenzi ya dhati kwa chama + nchi,asiye na majungu na umbeya kwa chama kama WEWE.
   
 16. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #16
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  linajidhihilisha = linajidhihirisha
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  analysis nzuri,kwa kweli kuna haja ya kubadilika.
   
 18. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #18
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Agreeed! 100% FACTS!

  William.

   
 19. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #19
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Uchambuzi wako una utata mwingi, kwa mfano unahusisha mafanikio ya cdm na usalama wa taifa. Kwa yeyeyote mwenye akili na uelewa wa siasa za tanzania ni dhahiri kuwa usala umekuwa nguzo dhahiri kwa ccm na serikali yake (kuhakikisha haking'oki madarakani)

  Pia umezungumzia Mbowe kubadilika na kuwa mstaarabu asiyetaka kugombana au kulumbana na ccm, hiyo si kweli katika kipindi chote cha uongozi wake katika cdm hakuwahi kupata misukosuko kama kipindi hiki (2010/2011) sasa huo ustaarabu unao uzungumzia sijui ni upi ndugu yangu.

  Mbowe na viongozi wengi wa cdm wamekuwa na kesi nyingi za kubambikizwa kwakuwa tu wamezidisha kasi ya mapambano sasa wewe hilo hulioni ila unacho kiona ni kuporomoka kwa cdm kama si kudumaa. Kwa taarifa yako tathmini za kisiasa zinaonyesha hali sasa ni mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa 2009/2010, kama kutafanyika uchaguzi leo kwenye baadhi ya mikoa ambayo cdm haiukuwa na nguvu ccm inahatari ya kushindwa na mafano dhahiri ni Igunga.. 2010 cdm haikuwa na hata kura moja ya ubunge (haikusimamisha mgombea) lakini juzi hapa pamoja na uchakachuaji na serikali yote kuhamia huko na kuisaidia ccm bado cdm kiliibuka na 46%. Huko ni kukua ambako wewe kwa upofu ulio nao hutaki kuona.

  Hakika chama hiki kinakua na kinaelekea kushika hatamu za nchi hii miaka michache ijayo, ila sikatai kuna mageuzi ya kiufundi yanapaswa kufanywa ili kuhitimisha safari ya kuikomboa nchi yetu.
   
 20. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #20
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  lol, kuna nyingine umeacha. Mizaa = mizaha...
   
Loading...