CHADEMA yawaumiza vichwa CCM Mpanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yawaumiza vichwa CCM Mpanda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Nov 19, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  CHADEMA yawaumiza vichwa CCM Mpanda

  Viongozi wa jumuiya tatu za CCM wilayani Mpanda, mkoani Katavi wamezuiliwa kufika kwenye ofisi za chama hicho kwa ajili ya usalama wao, kwa kile kinachodaiwa kukisaliti chama kufuatia kushindwa kulirejesha Jimbo la Mpanda Mjini ambalo limenyakuliwa tena na Chadema.

  Kwa mujibu wa Katibu wa CCM wa Wilaya ya Mpanda, Jacob Nkomola, amewataja viongozi hao kuwa ni Katibu wa UVCCM, Peter Tungulu, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Theodora Kisesa, na Mwenyekiti wa UWT, Rose Mayaya.

  Hatua hiyo inafuatia viongozi hao kutuhumiwa na kundi la wafuasi wa chama hicho (CCM) na kufika hatua ya kufunga ofisi za jumuiya hizo kwa kuweka makufuli milangoni na kuzilinda huku wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mawe.

  Hali hiyo ilitokea mwanzoni mwa wiki hii baada ya chama hicho kushindwa kulirejesha jimbo la Mpanda Mjini mikononi mwao na kuendelea kushikiliwa na Chadema kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita………………..

  …………Habari zaidi katika T. Daima Uk. 5.


  My take:

  Penye red: Mimi nahoji kuhusu huo unaoitwa 'usaliti.' Mimi naona hiki si kingine bali ni kuanza kuporomoka kwa CCM kila mahali -- na sasa wanajifanya kuita usaliti n.k. Hivi majuzi vigogo fulani ktk CCM akiwemo Jaji Warioba walisema kuporomoka kwa kura za CCM katika uchaguzi wa mwaka huu kunatokana na makundi yaliyojitokeza baada ya kura za maoni za uteuzi.

  Mimi naona hiyo ni namna moja ya' kiheshima' ya kusema chama kinaporomoka vibaya kutokana na sera zake zilizo mbovu -- hususan kuendeleza na kukumbatia mafisadi.
   
Loading...