CHADEMA yawasha moto Arusha. Mbowe azindua Mkakati mpya

Havai barakoa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) , leo kimeanza kupanga mipango mipya ya kukisogeza karibu zaidi na Wananchi , ambapo Mwamba Mwenyewe Freeman Mbowe ameanza kwa kufungua kikao cha Kamati ya Utendaji Mjini Arusha


CHAMA CHA SIASA NI MABARABARANI NA MAJUKWAANI - JK NYERERE
FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, tarehe 27 Mei 2021 siku ya Alhamisi, anatarajiwa kuzindua ‘Operesheni Haki,‘ ambayo itafanyika nchi nzima.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne tarehe 25 Mei 2021 na Chadema, kupitia ukurasa wake wa Twitter, kampeni hiyo itazinduliwa jijini Arusha.

Taarifa ya Chadema imesema kuwa, lengo la operesheni hiyo ni kudai katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, pamoja na uimarishwaji misingi ya haki nchini.

Sambamba na hilo, taarifa ya Chadema imesema, Mbowe ameendesha kikao cha Kamati Tendaji ya chama hicho, katika Kanda ya Kaskazini, kilichofanyika leo jijini Arusha.

“Leo Mei 25, 2021, Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe, ameendesha Kikao cha Kamati Tendaji ya Kanda ya Kaskazini, jijini Arusha,” imesema taarifa ya Chadema.
 
hahahaaabado ana nia ya kwenda ikulu? asahau ataendelea kuwa chama cha upinzani milele
Tukazanie katiba mpya.
Tukiipata hiyo hatutahofu nani yupo ikulu. Tunajua atalazimika kufata matakwa ya wananchi, hilo ndilo lengo kuu la kupata katiba mpya iliyo bora.
 
Lumumba hali si swali, hadi muda huu tunaingia mitamboni walikuwa bado wanafuatilia nini mwamba kakisema !!
Lumumba kubwa kaka. Unayoisema weye umefika ukawauliza au ukawaona hali yao sio shwari. Au ndo mambo ya kushiba dona na kipande cha ngulu halafu unang'ata njiti.
 
Mungu na waungwana, shetani na wahuni! Ni fahari kuwapigania waungwana, ni aibu na fedheha kuwapigania ccm.

Mungu ibariki Chadema, tusaidie kuwachukua ccm wote waliobaki kama ulivyomchukua yule dikteta muuaji
expand...huyo tapeli na jizi la haaayi lilitakiwa kuwa jela kabisa wala si kutapeli tena watanzania nyambaf kbs
 
Back
Top Bottom