Chadema yawanusuru wananchi wa Nzasa-Chanika, Waziri Tibaijuka awarejeshea ardhi yao...!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yawanusuru wananchi wa Nzasa-Chanika, Waziri Tibaijuka awarejeshea ardhi yao...!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Maranya, Jun 18, 2012.

 1. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ni baada ya mkutano wa hadhara ulioitishwa na Chadema jimbo la Ukonga tarehe 13/05/2012, mkutano uliofanyika mbele ya ofisi ya mwenyekiti wa mtaa wa Nzasa-Kata ya Chanika, na mgeni rasmi alikuwa mwanasheria nguli nchini Mh. Mabere Marando.

  Katika mkutano huo wananchi walielezea kero kubwa waliyokuwa nayo ni serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii kupora ardhi yao na kuwahamisha kwa nguvu takribani miaka zaidi ya kumi iliyopita, katika kile serikali ilichodai kwamba walikuwa wamevamia eneo la hifadhi ya msitu wa kazimzumbwi, wakati ukweli ni kwamba eneo hilo ni lao la asili ambalo wamekuwa wakiishi hapo tangu nchi haijapata uhuru.

  Ndipo Mh. Mabere Marando alipojitolea kufungua kesi (bila kutaka malipo yoyote toka kwa wananchi hao) mahakama kuu divisheni ya ardhi kudai serikali iwarejeshee ardhi yao na kuwalipa fidia ya uharibifu wa mali na mateso waliyopata toka kwa vyombo vya dola wakati wakihamishwa kwa nguvu.
  Mh. Mabere Marando alianza kazi hiyo mara moja baada ya kukamilisha kazi ya kupokea na kuchambua documents mbalimbali kutoka kwa wananchi na vyanzo vingine, na kuanza ufuatiliaji katika Halamshauri ya Manispaa ya Ilala, Wizara ya maliasili na utalii, wizara ya ardhi, na hatimaye kutoa taarifa ya kusudio la kufungua kesi.

  Serikali ilipopata taarifa kwamba Mabere alikuwa yuko katika hatua za mwisho za mchakato wa kufungua kesi mahakama kuu kwa ajili ya wananchi wa Nzasa ndipo mara moja waziri wa ardhi mama Tibaijuka akakurupuka kwenda Nzasa kuonana na wananchi na kuwaahidi kwamba suala lao lilikuwa linafahamika wizarani kwake na yeye alikuwa analifuatilia na angelitolea uamuzi mapema iwezekanavyo. Hivyo kuwaomba wasiendelee kumpa ushirikiano wowote mh. Marando katika azma yake ya kuifungulia mashataka serikali. Na kwakuwa wananchi wengi wameteseka kwa muda mrefu na tegemeo lao ni ardhi yao, basi waliridhia ombi la Waziri Tibaijuka na kumtaarifu mh. Marando kwamba asiendelee na mchakato wa kufungua kesi dhidi ya serikali kwakuwa waziri wa ardhi amewaahidi kulipatia ufumbuzi tatizo lao.

  Hatimaye sasa wananchi wale wameruhusiwa kurudi katika maeneo yao ya asili, waliyokuwa wamefukuzwa na serikali huku wengi wakiathirika kwa kupata vipigo toka kwa vyombo vya dola na wengine walifungwa kwa sababu ya kutetea ardhi yao. Bila shaka wale waliobahatika kuangalia taarifa ya habari ya itv jana saa mbili usiku walishuhudia wananchi wa Nzasa wakiwa wamerudi katika makazi yao ya asili waliyokuwa wameondolewa kwa ubabe wa serikali ya ccm.

  Ushauri wangu kwa mama Tibaijuka ni kwamba asisubiri kusukumwa na Chadema ili atekeleza wajibu wake kwani migogoro ya ardhi imetapakaa kila kona ya nchi hii, awe pro active katika kufanya shughuli zake.
  Lakini pia niwapongeze viongozi wote wa Chadema jimbo la Ukonga kwa kazi nzuri wanayoifanya kutetea maslahi ya wananchi wa jimbo la Ukonga. Na mwisho nimkumbushe mama Tibaijuka kwamba wale wananchi wanahitaji kulipwa fidia ya uharibifu wa mali zao pamoja na mateso waliyoyapata ya kupigwa na kufungwa kwa ajili ya kutetea ardhi yao, hivyo basi asimamie na kukamilisha zoezi la kuwalipa fidia waathirika wote wa kadhia ya Nzasa/Kazimzumbwi.

  UPDATES:
  Baada ya wananchi kushitukia hadaa za serikali kuwarudisha nzasa bila barua ama tangazo rasmi la serikali (GN) wananchi wa nzasa wanaendelea kuwasiliana na wakili mabere marando na sasahivi yuko katika hatua za mwisho kabisa za kuifikisha serikali mahakamani (mahakama kuu kitengo cha ardhi) ili pamoja na mambo mengine, serikali iwalipe fidia wananchi wote walioondolewa katika maeneo yao huko nzasa na kuharibiwa mali zao, lakini pia kuitaka serikali iwarudishe wananchi hao katika maeneo yao kwa maandishi ili wasijekuwafanyia uhuni huko mbele ya safari.
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Waziri wa Ardhi Tibaijuka, kafanya yake kama waziri makini wewe unaleta porojo za Chadema!
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Zaidi ya miaka 10 Mabere alikuwa wapi? Mafia?
   
 4. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ritz na Zomba.. CHADEMA inaiongoza hii nchi M.kwere kazi yake kuzurura na kutalii tu
   
 5. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Inaniuma sana....

  Wanachi wa Nzasa wamepigwa chenga ya mwili. Move waliyoanza nayo mwanzo ilikuwa ni sahihi sana. Walikuwa na uhakika wa kurudishiwa maeneo yao, kulipwa fidia ya uharibifu wa mali zao na kulipwa fidia ya mashambulizi na maumivu katika viungo vyao baada ya kushinda kesi. Mama Tibaijuka alijua kuwa kweli Serikali katika kesi husika haiwezi kushinda, ndiyo sababu akaingilia kati ki-namna. Sawa kafanya vizuri, lakini wananchi wa Nzasa wamepata moja tu.

  Sina uhakika barua ya kuwakaribisha tena katika maeneo yao ya awali imakaa vizuri au kimtego-mtego.
   
 6. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kafanya yake nini?
  Alikuwa wapi siku zote hadi aliposikia Marando ameamua kulivalia njuga ndipo akakurupuka kwenda kuwalaghai wananchi kwamba anawarudisha katika maeneo yao. Wakati serikali yenu legelege inawahamisha kwa maguvu ya policcm haikujua kwamba ile ni ardhi yao tangu kwa mababu zao?
   
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Zaidi ya miaka kumi serikali legelege ya nyinyiem ilikuwa inafanya nini kutojua kwamba lile ni eneo lao la asili na si hifadhi ya msitu wa kazimzumbwi?
  Mkimsikia mabere marando nyinyiem wote masaburi yanagongana.
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Sio kuzurura Manyanza, anapenda sana kufanya umatonya huko ulaya na marekani wakati rasilimali zote tunazo hapa hapa kwetu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kazi afanye Tibaijuka, wapinzani warukie hoja, kwi kwi kwi teh teh teh.
   
 10. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mnyamahodzo
  Ni kweli hiki ndicho tunachofikiria, si jambo rahisi kiasi hicho waziri Tibaijuka kukimbia haraka haraka kuwarudisha katika maeneo yao. Bado nafuatilia kujua kama wanazo barua rasmi za kuwarudisha, nilichokiona ni tangazo la wizara ya ardhi kwenye vyombo vya habari.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Hadi asukumwe kama gari ya kizamani isiyokuwa na startermotor!!??
   
 12. m

  mamajack JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  kwani hujui serikali siku hizi inafanya kazi kulingana na madai ya chadema,wameshaona mambo mabaya lazima wawatekelezee.
  with chadema,haki itatendeka tu,hata mkubisha.
   
 13. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Kweli ccm inaongozwa na cdm huwezi niambia tiba alikua anajua akaendelea kukaa kimya, bila marando wasingerudishiwa leo
   
 14. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hahaaa kwanini afanye umatonya ulaya wakati wamamtukana si bora akasimama pale Askari Monurement na bakuli lake watu watamchangia, mbona CHADEMA kwenye mikutano yao hua wanakusanya michango kutoka kwa wananchi waliohudhuria mkutano? au watanzania wanamdharau bab MwanaAsha?
   
 15. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kufanya umatonya ulaya na marekani dili ati. Anapata muda wa kupiga picha na mamodels, wanamuziki, wanasoka, siunajua zileee!!
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Asukumwe leo, apitie kesi ;eo atowe majibu leo. Hata dikteta wetu maarufu alikuwa hafanyi hivyo.

  Wapinzani wamekurupuka, Tibaijuka akawazima, kuwa hayo mambo mbona tayari. halafu humu mnakuja kudanganya watu. hivi tutawapa uongozi wa nchi muiendeshe kwa uongo> Maaweee!, tulidanganywa kwa miaka 24 mfululizo, sasa basi.
   
 17. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #17
  Jun 18, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,660
  Likes Received: 3,310
  Trophy Points: 280
  Na vile vile alisaidia serikali ya ccm kuwapora raia hao mali yao na kuwajeruhi,leo kwa kuona upepo mkali wa chadema unaelekea upande wake anajifanya eti suala hilo analijua kwa muda mrefu eti analishughulikia,ujinga huu!!yaani unin'goe meno kwa makusudi then ujifanye mwema kuniwekea ya bandia?jiulize wananchi hao wamerudishwa nyuma kimaendeleo kwa kiasi gani kwa upumbavu wenu kutetea ushenzi unaofanywa na hilo lichama lenu la kiuaji!!kweli bora tu jf iendelee kuficha ID za watu,vinginevyo tungetafutana,nisingeweza kuvumilia upumbavu kama huu wako.
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Njoo mtaa wa Livingstone na Mafia kuna duka kubwa linaitwa GGS, uliza tu Zomba yupo, mwenzako mmoja namsubiri leo wiki sijamuona.
   
 19. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #19
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  ukweli ni kuwa chadema kinaongoza nchi na ccm inatawala
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mabere huyo Wakili wa Jeet Patel na Yusufu Manji?
   
Loading...