CHADEMA yavuna wanachama zaidi ya 1,800 toka CCM mikoa ya Simiyu na Njombe!

Rose Mayemba

JF-Expert Member
May 7, 2012
721
1,017
ZAIDI ya wanachama 1300 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka mikoa ya Simiyu, Morogoro na Njombe wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katika mkoa wa Njombe pekee, wana CCM 600 walijiunga na CHADEMA na wengine 421 kutoka mkoa wa Simiyu wakati wa ziara iliyofanywa na timu ya baadhi ya wabunge wa chama hicho.

Katika mkoa wa Njombe, licha ya kufungua matawi matatu na ofisi moja ya kata.

Huko Simiyu, wanachama waliojiunga wanatoka katika wilaya za Maswa na Meatu juzi katika mikutano tofauti ya hadhara iliyofanyika katika mji wa Nyalikungu wilayani Maswa na Mwanhuzi wilayani Meatu iliyohudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Mikutano hiyo ilihutubiwa na wabunge, Meshack Opulukwa wa jimbo la Meatu na Slivester Kasulumbayi wa Maswa.
Huyu Msigwa ni mzee wa kukomaa kama wamwitavyo wananchi wake katika nchi yake, alikimaliza chama cha magamba kwa kukiita ni chama kilichojaza panya serikalini. JK na wafuasi wake wote ni panya kwa mujibu wa hotuba yake, aliidhihirishia Tz kwamba hata kusini wameamka na wanatambua wajibu wao.

Ni baada ya kuhamasisha mchango kufanyika kwa dk 7 na kupatikana kwa zaidi ya mil moja. Kwa mvuto wake wa kichungaji aliwabatiza wazee 3 kwa maji matakatifu ya CHADEMA na kuwavua magamba yaliyowatesa kwa miaka mingi.

Be blessed mzee
 
ZAIDI ya wanachama 1300 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka mikoa ya Simiyu, Morogoro na Njombe wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katika mkoa wa Njombe pekee, wana CCM 600 walijiunga na CHADEMA na wengine 421 kutoka mkoa wa Simiyu wakati wa ziara iliyofanywa na timu ya baadhi ya wabunge wa chama hicho.

Katika mkoa wa Njombe, licha ya kufungua matawi matatu na ofisi moja ya kata.

Huko Simiyu, wanachama waliojiunga wanatoka katika wilaya za Maswa na Meatu juzi katika mikutano tofauti ya hadhara iliyofanyika katika mji wa Nyalikungu wilayani Maswa na Mwanhuzi wilayani Meatu iliyohudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Mikutano hiyo ilihutubiwa na wabunge, Meshack Opulukwa wa jimbo la Meatu na Slivester Kasulumbayi wa Maswa.
 
Ole wenu mnaoanzisha thread za wana magamba kukimbia chama chao, mtapambana na rungu la chiligati.
 
Good Story. We must Change. Kuna njia ya ukombozi wale wenye kiu ya kuifuata wameanza kuifuata tunasubiri nini ss. Imekaribia kufungwa.
 
Huyu ni mzee wa kukomaa kama wamwitavyo wananchi wake katika nchi yake,alikimaliza chama cha magamba kwa kukiita ni chama kilichojaza panya serikalini,jk na wafuasi wake wote ni panya kwa mujibu wa hotuba yake,aliidhihirishia Tz kwamba hata kusini wameamka na wanatambua wajibu wao,ni baada ya kuhamasisha mchango kufanyika kwa dk 7 na kupatikana kwa zaidi ya mil moja.kwa mvuto wake wa kichungaji aliwabatiza wazee 3 kwa maji matakatifu ya chadema na kuwavua magamba yaliyowatesa kwa miaka mingi.be bless mzee

Loh cdm siku hizi mnabatiza wafuasi, mnatupeleka pabaya ee mungu tuepushe
 
hongereni sana wote wanaoujua ukweli na kuukimbia uongo / ufisadi kwani kukaandi pamoja na mafisadi kuunga mkono ufisadi hata kama hufisadi wewe ndiyo maana wanajitapa kuwa wana wachama 5,000,000. nchi nzima.

Naomba kikosi cha statistics wafanye hesabu hadi sasa wamesalia wanachama wangapi baada ya hili wimbi la kukimbiwa na makundi ya wanachama wao
 
Well done commanders, wapukutisheni mpaka wabaki miti mitupu, wakati wa mavuno ndiyo huu, songeni mbele kwa juhudi, maarifa, akili na bidii kubwa!
 
Big up brothers and Sisters....keep it up....jamani mbona Zitto na Said Arf (Mpanda mjini) siwasikii kwenye majimbo yao....where are they??? Kama vile wamelala....Pls kama kuna Mwanajamvi yopo Mpanda anijuze kama mbunge wetu yupo jimboni.
 
Back
Top Bottom