QUALITY
JF-Expert Member
- Sep 27, 2010
- 853
- 115
Hivi Karibuni Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefanya ziara wilayani Ngara na kusimika uongozi rasmi wa wilaya hiyo na kuzindua matawi 16 na kufungua ofisi za kata na matawi zipatazo 6. Ziara hiyo iliongozwa na mwenyekiti wa Mkoa wa Kagera ndugu Wilfred Lwakatale akisindikizwa na mwenyekiti wa wilaya hiyo ndugu Hosea Chiza na mwenyekiti wa Biharamulo ndugu George Kasaiza.
Katika ziara hiyo zaidi ya wanachama 300 walijiunga na CHADEMA na wanachama wa CCM, CUF na NCCR Mageuzi 88 walirudisha kadi na kujiunga na CHADEMA.
CHADEMA pia iliendesha semina kwa viongozi na wanachama wa chama hicho mjini Rulenge katika ukumbi wa walimu (Teachers' Resource Centre = TRC) ambapo zaidi ya wanachama 90 walihudhulia kujifunza sera, itikadi, wajibu wa wanachama n.k
Baadhi ya picha tulizoweza kupata kutoka Ngara ni kama ifuatavyo.

Attachments
-
UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA RULENGE-MK MKOA-LWAKATARE (18).JPG683.1 KB · Views: 181
-
UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA RULENGE-MK MKOA-LWAKATARE (13).JPG638.5 KB · Views: 114
-
UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA RULENGE-MK MKOA-LWAKATARE (1).JPG571.4 KB · Views: 107
-
SEMINA YA CHADEMA RULENGE NA MK MKOA-LWAKATARE (3).JPG353.9 KB · Views: 98
-
UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA RULENGE-MK MKOA-LWAKATARE (16).JPG738.5 KB · Views: 103
-
CHADEMA KIKAO CHA NDANI KABANGA- NA MK MKOA-LWAKATARE (17).JPG291.1 KB · Views: 100