CHADEMA yavamia Jimbo la Ngara, Kagera

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
Hivi Karibuni Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefanya ziara wilayani Ngara na kusimika uongozi rasmi wa wilaya hiyo na kuzindua matawi 16 na kufungua ofisi za kata na matawi zipatazo 6. Ziara hiyo iliongozwa na mwenyekiti wa Mkoa wa Kagera ndugu Wilfred Lwakatale akisindikizwa na mwenyekiti wa wilaya hiyo ndugu Hosea Chiza na mwenyekiti wa Biharamulo ndugu George Kasaiza.

Katika ziara hiyo zaidi ya wanachama 300 walijiunga na CHADEMA na wanachama wa CCM, CUF na NCCR Mageuzi 88 walirudisha kadi na kujiunga na CHADEMA.

CHADEMA pia iliendesha semina kwa viongozi na wanachama wa chama hicho mjini Rulenge katika ukumbi wa walimu (Teachers' Resource Centre = TRC) ambapo zaidi ya wanachama 90 walihudhulia kujifunza sera, itikadi, wajibu wa wanachama n.k

Baadhi ya picha tulizoweza kupata kutoka Ngara ni kama ifuatavyo.
 

Attachments

  • UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA RULENGE-MK MKOA-LWAKATARE (18).JPG
    UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA RULENGE-MK MKOA-LWAKATARE (18).JPG
    683.1 KB · Views: 181
  • UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA RULENGE-MK MKOA-LWAKATARE (13).JPG
    UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA RULENGE-MK MKOA-LWAKATARE (13).JPG
    638.5 KB · Views: 114
  • UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA RULENGE-MK MKOA-LWAKATARE (1).JPG
    UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA RULENGE-MK MKOA-LWAKATARE (1).JPG
    571.4 KB · Views: 107
  • SEMINA YA CHADEMA RULENGE NA MK MKOA-LWAKATARE (3).JPG
    SEMINA YA CHADEMA RULENGE NA MK MKOA-LWAKATARE (3).JPG
    353.9 KB · Views: 98
  • UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA RULENGE-MK MKOA-LWAKATARE (16).JPG
    UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA RULENGE-MK MKOA-LWAKATARE (16).JPG
    738.5 KB · Views: 103
  • CHADEMA KIKAO CHA NDANI KABANGA- NA MK MKOA-LWAKATARE (17).JPG
    CHADEMA KIKAO CHA NDANI KABANGA- NA MK MKOA-LWAKATARE (17).JPG
    291.1 KB · Views: 100
asante mkuu kwa kutujuza.huu ndo mda wa kujipanga.rwakatale asiishie rulenge na kabanga tu.inabidi kata zote afike.nyamiaga,rusumo,ntobeye,ntungamo,mugoma,mabawe,kanazi,kanyinya,mgikomero nguvu kazi n.k.hongera sana chadema hongera sana rwakatale.mia
 
Tuwaone na kauli zao za "Vyama vya msimu". Well done, a long journey starts with a single step.
 
Hongera sana Kamanda Lwakatare vyama vingine fanyeni hivi. tukiwa na vyama vya upinzani vyenye nguvu ni rahisi kuungana na kusimamisha mgombea mmoja na kushinda, kuliko sasa ambapo vyama vya upinzania bado sio imara sana hasa huko vijijini. Keep it up CDM.
 
Futile attempt
Your post is lacking serious value, substance, or a sense of responsibility and hence WELL describes who you are..!! If you explain something of which you do not know.......... you will end up explaining (SHOWING) how much YOU DO NOT KNOW
 
Wilaya ya Missenyi nayo bado inapwelea kwa CHADEMA. Wapo wapenzi wengi lakini hakuna uongozi kuanzia vijijini mapaka Wilaya. Hata kwenye uchaguzi mkuu uliopita baadhi ya vituo vilikosa mawakala wa CHADEMA.
 
Hongera sana Kamanda Lwakatare vyama vingine fanyeni hivi. tukiwa na vyama vya upinzani vyenye nguvu ni rahisi kuungana na kusimamisha mgombea mmoja na kushinda, kuliko sasa ambapo vyama vya upinzania bado sio imara sana hasa huko vijijini. Keep it up CDM.

Hakuna vyama vya kuungana navyo sana sana mtaishia kuchumbiwa na CCM tu.CDM wapambane kivyao na wanao watu wengi nyuma yao, kuungana ni strategy mufu not healthy at all
 
Back
Top Bottom