Chadema yaunguruma Dodoma; Operesheni Sangara yapaa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yaunguruma Dodoma; Operesheni Sangara yapaa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Henry Kilewo, Mar 18, 2010.

 1. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #1
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  CHADEMA yaendeleza harakati za ukombozi wa raslimali za umma dodoma, wakazi wajitokeza kwa wingi kuunga mkono, wa muahidi MBOWE wapo tayari kwa lolote litakalo tokea kwa mabaya au kwa mema mpaka ukombozi upatikane wasema raudi hii chama cha chukua chako mapema hakina nafasi, waingiwa na imani kubwa na harkati za chadema ZIKIONGOZWA NA MBOWE, wazee wasema tupo nyuma yako mwenetu tusaidie kutupatia ukombozi wa kimaendeleo na siyo chuki fitna kama tunavyo fanyiwa kwasasa,
   
 2. Mwananzuoni

  Mwananzuoni JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2010
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 288
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Ni Operesheni Sangara ya Chadema?.
   
 3. Mwananzuoni

  Mwananzuoni JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2010
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 288
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Kumpukeni Sheria ya kutumia "Mpunga" imesainiwa kwa "mbwembwe", Lakini bila "Mpunga" operesheni kama Sangara zitafanikiwa?
   
 4. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #4
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  kaka tulia uone ukombozi unavyo fanywa kwa watu waliyo na dhamira ya kweli kumkomboa mtanzania kuna milima na mabonde lazima wanaharakati kama hawo wayapitie yote
   
 5. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  MIKUTANO maarufu inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imeanza mkoani Dodoma kwa kumshughulikia Mbunge wa Mtera, John Samwel Malecela.
  Mwenyekiti wa chama hicho, Freema Mbowe, alisema Malecela ambaye amekuwa akitumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kampeni mbalimbali, ndiye anaongoza mipango ya kuiba kura.
  "Huyu sina naye ugomvi, lakini napenda kuwaambia kwamba yeye ndiye anayeandaa michoro ya wizi wa kura ndani ya CCM katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika nchini," alisema Mbowe.
  Alisema kokote ambako CCM imekuwa ikishiriki uchaguzi, CCM imekuwa ikimtumia ili awasaidie kufanikisha malengo yao, jambo ambalo linamjengea sifa mbaya kiongozi huyo mkongwe.
  "Sina ugomvi na Malecela, namheshimu sana mzee wangu, ila tatizo langu kwake ni wizi wa kura unaofanywa kila mahali anapopelekwa katika chaguzi," alisema.
  Mbowe alitoa kauli hiyo kwenye viwanja vya Barafu wakati wa uzinduzi wa mikutano hiyo mjini hapa ambako mamia ya wananchi wa Dodoma walifurika.
  Mbowe aliwasili katika viwanja hivyo majira ya saa 11 jioni jana, ambapo alitumia muda mwingi kuponda sera za CCM zinazoonekana kuwakandamiza wananchi na zimekuwa zikilea mafisadi.
  Huku akishangiliwa na wananchi waliosikika wakisema: "Hakuna kushuka mpaka kieleweke," Mbowe aliwaambia wananchi kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo lipo Dodoma linalea mafisadi ambao wanapaswa kuchukuliwa hatua.
  Kuhusu mfumo wa ugawaji wa viwanja katika mji wa Dodoma unaofanywa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), Mbowe alisema umelenga zaidi viongozi kuliko wananchi.  Source: Tanzania daima 18/03/2010
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mwenye picha jamani tunaomba mtuwekee tuone jinsi Mbowe alivyo vuna watu wengi kuja kumsikiliza.
   
 7. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  BiG up CHADEMA
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  HIVI ulitegema mwandishi wa gazeti la simba kuacha kuremba timu yake?
   
 9. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mwenye picha jamani, big up chadema
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ulitaka aandikeje kama kweli Simba ni bingwa au ulitaka usikie Yanga bingwa kwa vile wewe ni mpenzi wa Yanga tha is the reality
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  usiichukulie negative... point yangu ni kwamba habari hiyo ipo gazeti moja tu!!! ni ishara tosha kwamba uenezi kwa chadema unaanza kuchoka sio kama sangara ilivyoanza!!!
  there are many ways to kill a man... i was delivering the message to CHADEMA kwamba uenezi wao umeishia zero grazing... na good analysists hawawezi weka mkazo kewnye gazeti la mbowe linaposifia mbowe

  Time for change is passing by!!!
   
 12. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  OK De Nono hili nalo ni gazeti la Mbowe

  Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ameuponda utaratibu unaotumika nchini katika kuwateuwa wakuu wa mikoa na wilaya kwa sababu hauzingatii maslahi ya wengi.
  Akizungumza wakati akizindua operesheni Sangara katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma jana, Mbowe, alisema kuwa utaratibu huo haupi mamlaka wananchi kuchagua kiongozi ambaye anafaa.
  “Mimi sina shida wala ugomvi na Dk. Nsekela (Mkuu wa Mkoa wa Dodoma), ugomvi wangu ni utaratibu unaotumika katika kuwapata viongozi hawa,” alisema.
  Mbowe alisema utaratibu mzuri ambao unazingatia maslahi ya wengi ni wa kuwaacha wananchi kuwachagua viongozi hao kwa kutumia utaratibu wa kupiga kura.
  Idadi kubwa ya watu walijitokeza katika mkutano huo kusikiliza, ingawa ulichelewa kuanza.
  Mkutano huo ulianza saa 11:00 jioni na baada ya muda unaoruhusiwa kisheria kumalizika saa 12:00 wananchi walimsihi Mbowe aendelee kuhutubia, lakini aliwaambia kuwa alikuwa ameongozana na wabunge ambao ndio watungaji wa sheria, hivyo inamlazimu ausitishe hadi leo.
  Leo chama hicho kitafanya mikutano katika Jimbo la Dodoma Mjini na kesho watakwenda Mtera, ambalo ni Jimbo la mwanasiasa mkongwe, John Malecela.
  Aidha, watu wengi walijitokeza na kununua kadi za uanachama wa chama hicho.

  CHANZO: NIPASHE
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Operesheni Sangara Dodoma

  [​IMG]Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akisalimiana na baadhi ya wananchi wa mji wa Dodoma, mara baada ya kuhutubia mkutanowa uzinduzi wa Oporesheni Sanga mkoani Dodoma,uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu jana.
  [​IMG]Mwenyekiti wa Chamacha Demokrasiana Maendeleo (CHADEMA), FreemanMbowe,akishirikiana na baadhi ya wabunge wa chama hicho,kuandikisha kadi kwawanachma wapya waliojiunga na chama hicho,mara baada ya mkutano wa uzinduzi wa Oporesheni Sangara mkoani Dodoma,uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu jana.
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  safi sana luteni... hapa tuko pamoja... na mimi nachukua hii habari ya NIPASHE aisee, nimependa kwamba ipo kwingine

  Hapa mezani nina CITIZEN, GUARDIAN na DAILY NEWS... sioni kitu ya namna hiyo... meaning, kazi bado sana!! coverage ni muhimu mno kipindi hiki
   
 15. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Asante Fidel80
   
 16. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ni kweli De Novo hizo habari hazimo kwenye CITIZEN, GUARDIAN na DAILY NEWS ukiangalia ni wangapi huko vijijini hata mijini huwa wananunua magazeti achilia mbali magazeti hayo ya kiingereza
   
 17. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Asante sana fidel80
   
 18. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hakuana cha CCJ wala nini, ni CHADEMA tu ndiye mkombozi
   
 19. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #19
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  nikweli alitegemea tuandike uongo kama wanacyo fanya labda alitaka tuandike MBOWE akosa watu ndiyo angeridhika kwa ufinyu wa upewo wake wa kuona mbali tanzania ya sasa siyo ya kudanganywa kwenye ukweli ni ukweli uongo hauna nafasi, tuiunge chadema mkono kwenye harakati kama hizi jamani wameonyesha zamira ya kweli
   
 20. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #20
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  hongera kamanda kwa kufanikisha picha tupo pamoja katika ukombozi CHADEMA CHAMA MBADALA WA TAIFA HILI
   
Loading...