Chadema yatoa masharti kurudi bungeni

Ustaadh

Ustaadh

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2009
Messages
413
Likes
7
Points
0
Ustaadh

Ustaadh

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2009
413 7 0
ILI waingie bungeni, wabunge wa Chadema wameweka masharti ambayo yakitekelezwa na Serikali watakuwa hawana tatizo tena.

Masharti hayo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ni Serikali kutoa tamko kuhusu hoja yao ya kutungwa Katiba mpya, kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na kutoa msimamo juu ya madai ya kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi mkuu wa hivi karibuni.

Katika mahojiano maalumu na HABARILEO jana, Mbowe alisema: “Matendo ya leo yanaleta matukio ya kesho.

Suala la msimamo wetu kushiriki vikao vya Bunge lijalo utategemea na mapokeo ya hoja zetu.

“Kwa sisi kugomea hotuba ya Rais, tunajua ujumbe wetu umefika kwa wahusika wakiwamo bwana mkubwa mwenyewe (Rais Kikwete), viongozi wa mashirika na taasisi mbalimbali na mabalozi, kuonesha kuwa kuna tatizo la msingi ambalo Chadema inataka lishughulikiwe.

“Tunajua kuna watu wameudhika, na tunajua kuwa hatukumfurahisha Rais, lakini ujumbe wetu umefika.

Kuna baadhi ya watu wamepotosha kuwa tunampinga Rais. Haikuwa nia yetu kutaka avuliwe urais au aondolewe ofisini, tulitaka aone kuwa kuna tatizo ambalo linatakiwa kushughulikiwa na yeye ndiye mhusika.”

Mbowe alisema hoja ya kwanza ya Chadema ni kuona umuhimu wa kuwa na Katiba mpya
itakayoliwezesha Taifa kujenga misingi imara ya demokrasia na kuifanya nchi kuwa na amani, itakayokalika na kila mtu bila kujali kabila, dini au chama chake cha siasa.

“Tunataka Katiba ambayo itamfanya kila Mtanzania aishi kwa amani na upendo, mfano mzuri ni Zanzibar, walikuwa na tatizo kama hilo lakini sasa wamelishughulikia, kwa kuwa na Katiba nzuri na wamekubaliana kuendesha mambo yao … si unaona kila mtu anafurahia hili na wote wanaishi kwa amani kabisa?” alihoji.

Mbowe alisema kilio chao cha pili ni kuundwa kwa Tume ya Uchaguzi iliyo huru ili kufanya uchaguzi ujao usiwe na dosari.

“Ndiyo uchaguzi umekwisha, lakini tunataka Tume ya Uchaguzi iliyo huru, hatutaki kasoro zilizojitokeza uchaguzi huu zijitokeze katika uchaguzi mwingine, hatutaki Tume ambayo mpaka watu waandamane au wakeshe ndipo watangaze matokeo

Alisema hoja ya tatu ni kuundwa kwa Tume huru itayochunguza malalamiko yao kuhusu kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi mkuu na kutoa mapendekezo ya kufanyiwa kazi dosari zitakazokuwa zimebainishwa.

“Tuna madai ya msingi kabisa, na tumetumia njia hiyo ili kufikisha ujumbe wetu kwa kufuata taratibu na tumewasilisha kilio chetu kwa amani kabisa, hatujatukana mtu, lakini baadhi ya watu wanatubeza na wengine wanasema tuundiwe azimio la kufukuzwa bungeni, sijui kama wanaelewa taratibu na kanuni.”

Aliongeza: “Katika vipaumbele 13 vilivyotolewa na Rais, hatujasikia suala la marekebisho ya Katiba ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa takribani miaka 15 sasa, na hakuna hatua inayochukuliwa, sasa tunataka haya tunayoyadai yawemo kwenye hivyo vipaumbele.

Alhamisi iliyopita, wabunge wa Chadema waliondoka kwenye ukumbi wa Bunge mara baada ya Rais Kikwete kuanza kuhutubia kwa mara ya kwanza tangu kufanyika uchaguzi mkuu, Oktoba 31.

Akizungumzia madai ya kuwapo mgawanyiko ndani ya Chadema, katika kufikia uamuzi huo wa kususia hotuba ya Rais, Mbowe alisema uamuzi huo ulipitishwa ndani ya kikao cha chama hicho.

“Uamuzi ule umetokana na kikao halali cha chama, katika masuala kama hayo, si lazima watu wote wakubali na diyo maana unaweza kufikia hatua ya kupiga kura, lakini mwisho wa yote uamuzi wa wengi ndio unaofuatwa
 
F

Fishyfish

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
231
Likes
0
Points
0
F

Fishyfish

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2010
231 0 0
I fear for the future of CCM :(
 
Ukwaju

Ukwaju

JF Bronze Member
Joined
Oct 19, 2010
Messages
8,871
Likes
1,348
Points
280
Ukwaju

Ukwaju

JF Bronze Member
Joined Oct 19, 2010
8,871 1,348 280
Du kidogo inaingia akilini sasa, kwa Mwenyekiti kuuelewesha umma ngoja tulinunue hilo gazeti
 
U

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2010
Messages
6,947
Likes
13
Points
0
U

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2010
6,947 13 0
Sasa watu tunaanza kuelewa zaidi kwa kumbe hapa nchini kwetu KUNA VICHWA ambavyo ikija kwenye MASLAHI YA TAIFA hawajifichi kwa woga na unafiki. CHADEMA, endeleeni kuonyesha that brand of QUALITY LEADERSHIP, Dunia sasa inawaelewa kuliko wakati mwingine wowote ule .......!!!!!!!!!!!!!
 
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2008
Messages
13,598
Likes
524
Points
280
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined May 11, 2008
13,598 524 280
Ili waingie bungeni wanatoa masharti?
Ili waingie bungeni walichohitaji ni kura za wananchi.
Maana ya demokrasia ndio hiyo, huwezi kulazimisha Bunge au serikali kufanya mambo kwenye majukwaa ya kisiasa wakati wewe ni mbunge, kaliongeeni bungeni. Kama kura zenu Bungeni hazitoshi, changamoto ni kutafuta kura hizo kwenye chaguzi zijazo.
Hii ya kusema hamuingii Bungeni mpaka mtekelezewe masharti, ni hysteria.
Na mtawaangusha waliowapigia kura kwa kiasi kikubwa kwa sababu hamjawaambia kuwa kususa ndicho mnachoenda kufanya.
 
Kalunguine

Kalunguine

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2010
Messages
2,545
Likes
9
Points
135
Kalunguine

Kalunguine

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2010
2,545 9 135
Hiki kichwa cha habari kimekaa sawa kweli? Masharti ya kurudi bungeni au kukaa bungeni akiwemo JK aliyeshindishwa kwa kura za wizi wa NEC?
 
N

NgomaNgumu

Senior Member
Joined
Nov 20, 2010
Messages
193
Likes
2
Points
0
N

NgomaNgumu

Senior Member
Joined Nov 20, 2010
193 2 0
Nafikiri hoja kubwa iliyojadiliwa ilikua je ni makosa kwa wabunge wa chadema kutoka bungeni au no. Lakini inaonekana kua wanataka kurudi tena bungeni. ambacho sijaelewa ni kusema wanatoa masharti. Mawazo yangu ni kua ni afadhali wakatumia lugha nyingine kuliko hiyo huwezi kwani huwezi kuweka masharti ya kurudi sehemu ambayo hukufukuzwa na ulipoondoka hukuombwa kurudi.
 
W. J. Malecela

W. J. Malecela

Tanzanite Member
Joined
Mar 15, 2009
Messages
14,056
Likes
3,423
Points
280
W. J. Malecela

W. J. Malecela

Tanzanite Member
Joined Mar 15, 2009
14,056 3,423 280
ILI waingie bungeni, wabunge wa Chadema wameweka masharti ambayo yakitekelezwa na Serikali watakuwa hawana tatizo tena.

Masharti hayo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ni 1. Serikali kutoa tamko kuhusu hoja yao ya kutungwa Katiba mpya, 2. kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na 3. kutoa msimamo juu ya madai ya kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi mkuu wa hivi karibuni.

Katika mahojiano maalumu na HABARILEO jana, Mbowe alisema: "Matendo ya leo yanaleta matukio ya kesho.

Suala la msimamo wetu kushiriki vikao vya Bunge lijalo utategemea na mapokeo ya hoja zetu.

"Kwa sisi kugomea hotuba ya Rais, tunajua ujumbe wetu umefika kwa wahusika wakiwamo bwana mkubwa mwenyewe (Rais Kikwete), viongozi wa mashirika na taasisi mbalimbali na mabalozi, kuonesha kuwa kuna tatizo la msingi ambalo Chadema inataka lishughulikiwe.

"Tunajua kuna watu wameudhika, na tunajua kuwa hatukumfurahisha Rais, lakini ujumbe wetu umefika.

Kuna baadhi ya watu wamepotosha kuwa tunampinga Rais. Haikuwa nia yetu kutaka avuliwe urais au aondolewe ofisini, tulitaka aone kuwa kuna tatizo ambalo linatakiwa kushughulikiwa na yeye ndiye mhusika."

Mbowe alisema hoja ya kwanza ya Chadema ni kuona umuhimu wa kuwa na Katiba mpya
itakayoliwezesha Taifa kujenga misingi imara ya demokrasia na kuifanya nchi kuwa na amani, itakayokalika na kila mtu bila kujali kabila, dini au chama chake cha siasa.

"Tunataka Katiba ambayo itamfanya kila Mtanzania aishi kwa amani na upendo, mfano mzuri ni Zanzibar, walikuwa na tatizo kama hilo lakini sasa wamelishughulikia, kwa kuwa na Katiba nzuri na wamekubaliana kuendesha mambo yao … si unaona kila mtu anafurahia hili na wote wanaishi kwa amani kabisa?" alihoji.

Mbowe alisema kilio chao cha pili ni kuundwa kwa Tume ya Uchaguzi iliyo huru ili kufanya uchaguzi ujao usiwe na dosari.

"Ndiyo uchaguzi umekwisha, lakini tunataka Tume ya Uchaguzi iliyo huru, hatutaki kasoro zilizojitokeza uchaguzi huu zijitokeze katika uchaguzi mwingine, hatutaki Tume ambayo mpaka watu waandamane au wakeshe ndipo watangaze matokeo."

Alisema hoja ya tatu ni kuundwa kwa Tume huru itayochunguza malalamiko yao kuhusu kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi mkuu na kutoa mapendekezo ya kufanyiwa kazi dosari zitakazokuwa zimebainishwa.

"Tuna madai ya msingi kabisa, na tumetumia njia hiyo ili kufikisha ujumbe wetu kwa kufuata taratibu na tumewasilisha kilio chetu kwa amani kabisa, hatujatukana mtu, lakini baadhi ya watu wanatubeza na wengine wanasema tuundiwe azimio la kufukuzwa bungeni, sijui kama wanaelewa taratibu na kanuni."

Aliongeza: "Katika vipaumbele 13 vilivyotolewa na Rais, hatujasikia suala la marekebisho ya Katiba ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa takribani miaka 15 sasa, na hakuna hatua inayochukuliwa, sasa tunataka haya tunayoyadai yawemo kwenye hivyo vipaumbele.

Alhamisi iliyopita, wabunge wa Chadema waliondoka kwenye ukumbi wa Bunge mara baada ya Rais Kikwete kuanza kuhutubia kwa mara ya kwanza tangu kufanyika uchaguzi mkuu, Oktoba 31.

Akizungumzia madai ya kuwapo mgawanyiko ndani ya Chadema, katika kufikia uamuzi huo wa kususia hotuba ya Rais, Mbowe alisema uamuzi huo ulipitishwa ndani ya kikao cha chama hicho.

"Uamuzi ule umetokana na kikao halali cha chama, katika masuala kama hayo, si lazima watu wote wakubali na diyo maana unaweza kufikia hatua ya kupiga kura, lakini mwisho wa yote uamuzi wa wengi ndio unaofuatwa."

- Unajua serikali ya CCM itakua inajimaliza yenyewe kama itajihusisha na any of this, kwanza siamini kwamba ninachosoma hapa ni kweli kwamba Mwenyekiti wa Chadema amesema haya, kwamba eti ametoa masharti ya kurudi Bungeni? Ametoa masharti kwa nani? Kwani wameombwa na nani warudi bungeni? Walisusia bunge au hotuba ya rais wanayedai hawamtambui ambayo ni kawaida sana?

- Habari haijakaa sawa sana hiii, I mean Chadema wameombwa na nani warudi Bungeni?William.
 
Kalunguine

Kalunguine

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2010
Messages
2,545
Likes
9
Points
135
Kalunguine

Kalunguine

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2010
2,545 9 135
- Unajua serikali ya CCM itakua inajimaliza yenyewe kama itajihusisha na any of this, kwanza siamini kwamba ninachosoma hapa ni kweli kwamba Mwenyekiti wa Chadema amesema haya, kwamba eti ametoa masharti ya kurudi Bungeni? Ametoa masharti kwa nani? Kwani wameombwa na nani warudi bungeni? Walisusia bunge au hotuba ya rais wanayedai hawamtambui ambayo ni kawaida sana?

- Habari haijakaa sawa sana hiii, I mean Chadema wameombwa na nani warudi Bungeni?

William.
Umesoma #6? Malecela bwana.
 
Kalunguine

Kalunguine

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2010
Messages
2,545
Likes
9
Points
135
Kalunguine

Kalunguine

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2010
2,545 9 135
- Unaweza kunisaidia kuelewa inasema nini hasa mkuu?

William.
Ndiyo maana huwa nakwambia ukomae kwanza kwa hoja kabla ya kutafuta popularity nadhani ya kuingia kwenye siasa za bongo. Siyo lazima ku-pragiarise, ili ukue katika hoja soma wengine wameandika nini na unukuu siyo kuhamisha.
 
W. J. Malecela

W. J. Malecela

Tanzanite Member
Joined
Mar 15, 2009
Messages
14,056
Likes
3,423
Points
280
W. J. Malecela

W. J. Malecela

Tanzanite Member
Joined Mar 15, 2009
14,056 3,423 280
icon1.gif
Re: Chadema yatoa masharti kurudi bungeni

Ndiyo maana huwa nakwambia ukomae kwanza kwa hoja kabla ya kutafuta popularity nadhani ya kuingia kwenye siasa za bongo. Siyo lazima ku-pragiarise, ili ukue katika hoja soma wengine wameandika nini na unukuu siyo kuhamisha.
- Umenivunja mbaavu mkuu ha! ha! ha! ha! ha!, yaanini mimi niige hoja zako are you kidding me or what? ha! ha! ha! Hilarious! Anyways, sina muda wa kujibu hizi zisizo na masilahi ya taifa kwa hiyo sitajibu tena!

William.
 
Mtazamaji

Mtazamaji

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
5,971
Likes
44
Points
0
Mtazamaji

Mtazamaji

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
5,971 44 0

- Unajua serikali ya CCM itakua inajimaliza yenyewe kama itajihusisha na any of this, kwanza siamini kwamba ninachosoma hapa ni kweli kwamba Mwenyekiti wa Chadema amesema haya, kwamba eti ametoa masharti ya kurudi Bungeni? Ametoa masharti kwa nani? Kwani wameombwa na nani warudi bungeni? Walisusia bunge au hotuba ya rais wanayedai hawamtambui ambayo ni kawaida sana?

- Habari haijakaa sawa sana hiii, I mean Chadema wameombwa na nani warudi Bungeni?William.
Sentesi ya kwanza Mbowe aliyosema ni
Mbowe alisema: "Matendo ya leo yanaleta matukio ya kesho.

Suala la msimamo wetu kushiriki vikao vya Bunge lijalo utategemea na mapokeo ya hoja zetu.
Hapa anamaanisha nini?
Jibu ni kwamba Wakiiningia bungeni hizo ndizo hoja kuu wao CHADEMA watakazoziwashilisha.

hope umeelewa
 
kitungi

kitungi

Senior Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
134
Likes
14
Points
35
kitungi

kitungi

Senior Member
Joined Nov 3, 2010
134 14 35
Ili waingie bungeni wanatoa masharti?
Ili waingie bungeni walichohitaji ni kura za wananchi.
Maana ya demokrasia ndio hiyo, huwezi kulazimisha Bunge au serikali kufanya mambo kwenye majukwaa ya kisiasa wakati wewe ni mbunge, kaliongeeni bungeni. Kama kura zenu Bungeni hazitoshi, changamoto ni kutafuta kura hizo kwenye chaguzi zijazo.
Hii ya kusema hamuingii Bungeni mpaka mtekelezewe masharti, ni hysteria.
Na mtawaangusha waliowapigia kura kwa kiasi kikubwa kwa sababu hamjawaambia kuwa kususa ndicho mnachoenda kufanya.
Acha u sisiemu! wameingia bungeni ili kutetea wananchi, na wananchi wengi ambao ni vijana kama sisi tunaitaji katiba mpya coz sheria nyingi za nchi zilizopo sasa IVI ni za kizamani, i mean hazitushilikishi sisi vijana wa kisasa zinaitaji marekebisho.kama hakitaeleweka sasa ivi ujue hata 2015 itakuwa ivyo ivyo, ''DIFFERENT DAYZ SAME MO' SHIT''
 
W. J. Malecela

W. J. Malecela

Tanzanite Member
Joined
Mar 15, 2009
Messages
14,056
Likes
3,423
Points
280
W. J. Malecela

W. J. Malecela

Tanzanite Member
Joined Mar 15, 2009
14,056 3,423 280
Sentesi ya kwanza Mbowe aliyosema ni
Hapa anamaanisha nini?
Jibu ni kwamba Wakiiningia bungeni hizo ndizo hoja kuu wao CHADEMA watakazoziwashilisha.

hope umeelewa
- Sasa tatizo lako lipo wapi? Kazi ya wabunge ni nini hasa? I mean mbona unahangaika lakini haieleweki mkuu? Unasema nini hasa kwamba wakiingia bungeni wabunge 46 watalazimisha muswaada sijakuelewa bado?

William.
 
kitungi

kitungi

Senior Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
134
Likes
14
Points
35
kitungi

kitungi

Senior Member
Joined Nov 3, 2010
134 14 35
unajua EU wanamatatizo sana ya wapoland kwamba wengi wao hawakubali coz wanafanya kazi kwa bei rahisi, but gov. ndani ya nchi za EU ndio zimesharuhusu Poland kuji mix, tatizo linakuja kwa wananchi wanalalamika na wanaanza kuwachukia wa Poland lakini ukiangalia serikali zao ndio chanzo coz serikali ndizo zimeruhusu iyo issue kwa iyo serikali ndio inaanza kujenga matabaka.kwa iyo kiangalia hii issue ki-undani zaidi utagundua kuwa muda mwingine serikali zetu huwa zinachezea sana wananchi bila wananchi kutojua, mie kwa mtazamo wangu kwa hiki kipindi inabid hao CDM wawe makini sana coz ni kipindi kigumu sana na issue nyingi sana zitajitokeza bila wao wenyewe kuonyesha ushirikiano nadhani 2015 hawatofika!!
 
Hassan J. Mosoka

Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Messages
657
Likes
22
Points
35
Hassan J. Mosoka

Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2010
657 22 35
Habari hii siimani mpaka niisome magazeti kama matano tofauti, kwa sababu nijuavyo mimi CDM hawajagoma kuingia Bungeni hata siku moja na walikula kiapo kuwatumikia watanzania wiki iliyopita. Na kwa kuwa habari hii imeandikwa na "Habarileo" Nadhani wamependisha lugha kama kawaida yao, maana hilo gazeti halina maana kabisa kwa uma wa wabongo. Haya maneno Mbowe alishasema kuwa ndiyo viapumbele vyao Bungeni siku chache zilizopita na sote tunajua sasa hii ya "Mashart ya kurudi Bungeni" I can believe this statement
 
mfereji maringo

mfereji maringo

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Messages
1,003
Likes
31
Points
135
mfereji maringo

mfereji maringo

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2010
1,003 31 135
chadema kazeni watz tupo nyuma yenu, mtabezwa kama mlivyobezwa mlipoanzisha hoja ya ufisadi, baadae wakanywea na wakairukia hoja hiyo na leo wanadai eti waliianzisha wao, siku si nyingi watageuka na kujifanya hoja ya katibampya ni yao. tumewazoea hao.
 
Gosbertgoodluck

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Messages
2,865
Likes
32
Points
0
Gosbertgoodluck

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2008
2,865 32 0
Ndugu,
Awali ya yote nitamke bayana kwamba habari hii siingizi akilini na kuitilia maanani mpaka nisome kwenye chanzo cha uhakika. Nina muda mrefu tangu nilipoacha kutumia magazeti ya ccm na serikali yake (uhuru, mzalendo, habari leo na daily news) kama chanzo cha habari zinazohusu siasa hapa nchini. Kama kawaida yao, habari zinazoandikwa na hayo magazeti kwa kawaida ''huchakachuliwa'' kwanza ndipo huchapishwa. Wahariri wa magazeti hayo utadhani walisoma chuo kimoja kinachofundisha uchakachuaji wa habari.

Kihusu wabunge wa CDM kutoingia bungeni, kwanza siamini kama huo ndiyo msimamo wao. Ninachojua mimi ni kuwa CDM wameeleza bayana kuwa wabunge wao wataelekeza hoja zao kwenye bunge katika maeneo makuu matatu ambayo yakipatiwa ufumbuzi utakuwa ni ukombozi mkuwa na wa kihistoria kwa wapiga kura wao na watanzania kwa ujumla. Maeneo hayo ni 'katiba mpya', 'tume huru ya uchaguzi', na 'tume huru ya uchunguzi wa mchakato mzima wa uchaguzi ulioisha hivi karibuni'.

Mimi naamini habari kwamba eti CDM hawataingia bungeni mpaka masharti hayo yatekelezwe imechakachuliwa makusudi na magazeti ya ccm na serikali yake ili kuvuruga msimamo wa CDM. Na hilo wameng'oa kwani CDM haiongozwi na maaskari wastaafu wala waganga wa kienyeji. CDM ni chama makini kinachoongozwa na wasomi waliobobea katika fani zote. CCM hamuwawezi kamwe.
 
Magogwajr

Magogwajr

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2010
Messages
223
Likes
1
Points
35
Magogwajr

Magogwajr

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2010
223 1 35
nimesoma hiyo thread vizuri bt cjaona kama mbowe ametoa masharti ya kurudi bungeni bali ameeleza nini kifanyke kurekebisha mapungufu na kuelekea uchaguzi huru na wa haki. navyo vinawezekana tu kwa kuwana katiba mpya iliyotungwa nawatanzania na sio waingereza. habari leo wmwpotosha kwa kuwaka heading isiyoendana na maelezo ya ndani. nashindwa kutifautisha habari leo na magazeti kama ya uwazi, ijumaa,
 
Forum statistics

Threads 1,238,907
Members 476,226
Posts 29,336,526