CHADEMA yatishia kuiumbua CCM - kuweka nje majina ya mawaziri na wabunge waliotaka kwenda CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yatishia kuiumbua CCM - kuweka nje majina ya mawaziri na wabunge waliotaka kwenda CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 11, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  • WAPONDA UTEUZI WA MA-DC

  na Waandishi wetu

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetishia kuweka hadharani majina ya mawaziri na wabunge ambao walikuwa tayari kujiunga na chama hicho.


  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uenezaji wa chama hicho, John Mnyika, alisema Chama cha Mapinduzi kisitake kuilazimisha CHADEMA iseme ukweli wote juu ya wimbi kubwa la wana CCM, wakiwemo wabunge na mawaziri ambao wanataka kujiunga nayo.

  Mnyika akijibu taarifa ya CCM iliyotolewa na Katibu wa Uenezi na Itikadi, Nape Nnauye, alisema kuwa viongozi wengi wa chama hicho tawala wanajua mchakato mzima uliokuwepo wa wabunge, mawaziri na wana CCM wengine kutaka kuhamia CHADEMA tangu wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010 lakini wakaingiliwa.


  Mnyika aliwataka viongozi wa CCM waseme kama wako tayari kupokea ukweli mchungu wa viongozi wao walio tayari kukihama chama hicho na kujiunga na upinzani “Wasitulazimishe kusema.

  Na kama wanataka waseme kama wako tayari, tufungue boksi, ikibidi hata nitaje majina ya watu na kwa nini baadaye walishindwa kujiunga,” alisema Mnyika.


  Mnyika alisema imekuwa ni kawaida ya CCM kukanusha kila kitu, na kumlinganisha Nape na aliyekuwa Waziri wa Habari wa Iraq chini ya utawala wa Saddam Hussein ambaye alikanusha kila kitu, huku akijua majeshi ya Marekani yalikuwa yamewazidi nguvu.


  “Sisi hatuwashangai wao kukanusha maana hata wakati waliokuwa madiwani wao wanahama kutoka CCM kuja CHADEMA walikanusha hivihivi, lakini leo yako wapi, madiwani kuanzia Arusha mpaka Mwanza huko wamehamia CHADEMA, hivyo hata hili la wabunge na mawaziri atakanusha sana lakini si atulie asubiri aone,” amesema Mnyika.


  Taarifa ya CCM iliyotolewa jana imekanusha madai yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, ambaye mwishoni mwa wiki jana alitangaza katika mkutano mkubwa wa hadhara jijini Arusha kuwa wabunge 70 na mawaziri kadhaa walikuwa tayari kujiunga na chama hicho cha upinzani.


  Nape alidai kuwa maneno hayo ya Mbowe ni uongo kwa vile hakuna waziri au mbunge ambaye yuko tayari kuondoka ndani ya CCM na kwamba yametolewa kwa lengo la kujipatia umaarufu wa bure.


  Hoja ya mauaji

  Akizungumzia tamko la CCM lililotolewa jana kukanusha tuhuma za kuhusika na mauaji, Mnyika alikishambulia vikali chama tawala akidai kimeshindwa, Nape anaficha ukweli juu ya kuhusika kwa baadhi ya viongozi wake na mauaji hayo.

  “Kama angetafakari kabla ya kusema angejua kuwa mpaka sasa viongozi wa serikali wanaotokana na CCM wako chini ya ulinzi wa polisi kuhusiana na mauaji ya Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Usa River. Lakini pia viongozi na wanachama wa CCM wametajwa kwa majina kuhusika katika tukio la wabunge wa CHADEMA kukatwa mapanga huko Mwanza. Na mpaka sasa wako chini ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi Mwanza,” alisema Mnyika.


  Aliongeza kuwa kuna majina ya viongozi wa CCM waliotajwa kuhusika katika vitendo vya mauaji na vingine vya utekaji kwa wanachama na makada wa CHADEMA katika maeneo mbalimbali mathalani wakati wa uchaguzi mdogo wa Kiteto, Busanda, Biharamulo na kwingine.


  Mnyika aliongeza kuwa kama kweli CCM inataka kuonyesha kuwa ina uchungu na inakerwa na wimbi la mauaji ya kisiasa yanayoendelea nchini, basi walizungumze suala hilo katika vikao vyao kuielekeza serikali kutumia sheria ya Inquest Act, sura ya 24 ya sheria za Tanzania ambayo inaitaka serikali kuchunguza vifo vyenye utata.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ni bora Chadema iwataje hao watu, ili CCM isijione kuwa ndio chama cha KIMUNGU hakuna kama CCM Tanzania

  Mawazo ya Nape na Nchemba hayafai kuongoza taifa hili hata kidogo, sijui Rais Kikwete alikuwa anafikiria nini kuwapa

  Vyeo
   
 3. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,705
  Likes Received: 17,756
  Trophy Points: 280
  Mimi pia ninalo koba la majina kama 7 hivi ila naogopa BAN coz JF Mods sometimes hawapendi CCM ife kifo kibaya
   
 4. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Pole Nape kwa ugonjwa wa degedege unaokukabili
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  This is silly and reckless, kama kweli waltaka kutoka kwanini CDM ndio iwataje? Na kulikuwa ba ulazima gani CDM kutaja mpango huo hadharani kabla haujaiva?
   
 6. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  CDM isingesema hadharani maana hata wakitajwa wanaweza wakakanusha na ikaonekana uzushi,hawa Wabunge na mawaziri wangejitaja wenyewe,ila hii kutajwa haina mashiko kabisa
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Bado sijaelewa mantiki ya CDM kuongelea hii hoja hadharani? Freeman Mbowe aliteleza, sasa Mnyika naona ameteleza zaidi? Kwa mtindo huu 'valuable fish' si watapotea? Wajifunze kutofautisha mambo ya siri na mambo ya kuongelea hadharani.
   
 8. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  hapo ndio naona CDM wamebugi step kusema hivyo.
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Wakiwataja watakuwa na ushahidi gani mwingine wa ziada kuyuaminisha kwamba walitaka kuhama au ni kuishia tu kutaja basi? Sioni kama kutajana kuna tija yoyote. Wasubiri tu watajitaja wenyewe muda ukifika.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Magwanda yanapojaa jasho hutoa harufu kali sana.
   
 11. M

  Malolella JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 367
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuna kitu kinaitwa 'political games' sasa hapa naona kuna hako kamchezo na nikawaida kwa wanasiasa. Usipojua kucheza hizo games bac ww c mwanasiasa na hutakubalika.
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hawa wakubwa wetu wakati mwingine hawajiandai na hotuba. Nadhani kule kujaa mno kwa watu kunasababisha waone kama wapo kati ya dunia mbingu!
  Hakika WAJIREKEBISHE!
   
 13. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hakuna haja ya kuwataja kwani wenye akili tunajua "wapenda madaraka" wanaona upepo unaelekea wapi ndo wakafanya booking mapema!

  Kwenye CCm hakuna watu makini, wamekwisha mpaka ameamua kuokoteza akina Kigoda, Mbatia na mapaparazi, kuchukua nafasi, sasa wajiandae kufungasha virago 2012!
   
 14. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Tofauti na mawazo yaliyotangulia mimi nasema, big up Chadema...penye mtama mwingi mwaga kuku! Fikirieni magamba yatakavoshtukiana, kaanza Nape na bado!
   
 15. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  kwishafanya kazi yako tayari!!
   
 16. T

  Thesi JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2012
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  CDM inapaswa kujua kwamba yeyote anayetaka kuhama hatopenda kutajwa kabla hajafanya mwenyewe hivo au kujitokeza kwenye mikutano au ofisi za CDM kujitangaza. Hilo litaonyesha jinsi wasivokuwa makini na hata hao wanaotaka kuhama watawashangaa na kuwaona hawafai.
  Mnyika chondechonde msifanye huo utoto.
   
 17. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Sahihi kabisa. Hakuna uhalali wa move ya namna hiyo.
   
 18. n

  ngaranumbe Senior Member

  #18
  May 11, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukiwataja watapotea katika mazingira ya kutatanisha
   
Loading...