CHADEMA yathibitisha kutoshiriki uchaguzi mdogo Ngorongoro, hadi Tume Huru ya Uchaguzi itakapopatikana

Hii inaonyesha kuwa bado waafrika tunachechemea kuelekea ustaarabu.
Bado tunaendelea kuwa jamii shenzi(primitive) na ambayo imeshindwa kujisimamia baada ya uhuru.
Roma haikujengwa kwa siku moja.
Maendeleo yapo lakini bado ni kidogo sana, tuendelee kustruggle hata kuufikia ustaarabu hapo baadae.
 
Mnaogopa uchaguzi kwani dhalimu wenu bado yupo?

Si mnapumua nyie?
Hatuagopi uchaguzi maana uhakika wa kupata kura toka kwa wananchi tunao. Ila ukhanithi aliouanzisha mwendakuzimu bado upo. Hivyo hatuna muda mchafu wa kupoteza kwa chama kilichochoka kushindana.
 
Hatuagopi uchaguzi maana uhakika wa kupata kura toka kwa wananchi tunao. Ila ukhanithi aliouanzisha mwendakuzimu bado upo. Hivyo hatuna muda mchafu wa kupoteza kwa chama kilichochoka kushindana.
Kwani mwenda kuzimu si amekufa?

Sasa kwanini msiende mkashiriki ili mpate mbunge?

Cha ajabu 2025 mtapeleka pua zenu na watu toka ubelgiji watakuja mbio mbio kushiriki uchaguzi.
 
Hiyo sawa. Bora kuwaachie. Ksbb hata CHADEMA ikishinda inapokwa ushindi.
 
naunga mkono hoja, tunawashauri ccm wawe wanajichaugua wenyewe wanaiandikia tume kupitisha. nchi imerudi nyuma kidemokraisia miaka 70, yaani afadhali na mkoloni aliwaruhusu kina Mwalimu wafanye mikutano yao Anatogro bila kuwavunja ngoko.
 
Kwani mwenda kuzimu si amekufa?

Sasa kwanini msiende mkashiriki ili mpate mbunge?

Cha ajabu 2025 mtapeleka pua zenu na watu toka ubelgiji watakuja mbio mbio kushiriki uchaguzi.
kwani na nyie mnashindwa vipi kuchaguana ili mpeleke jina tume na tume iandike kwa Bunge ili Mr. Zuzu amwapishe ?
 
Taarifa kwa Umma

Katibu Mkuu John Mnyika ameiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuitaarifu rasmi kuwa Chadema hakitashiriki uchaguzi wa marudio wa ubunge kwenye Jimbo la Ngorongoro na kata saba na badala yake amesisitiza kutaka iundwe Tume Huru ya Uchaguzi itakayohakikisha chaguzi zinakuwa huru, za haki na halali kuanzia katika uchaguzi wa marudio mpaka katika uchaguzi mkuu.

Kupitia barua hiyo Katibu Mkuu ameitaka Tume ya Uchaguzi iwataarifu wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi katika jimbo tajwa na kata za Handali, Bomalang'ombe, Nyalubanda, Nalasi Mashariki, Likombe , Ipwani na Naumbu kutokutoa fomu wala kufanya uteuzi kwa yoyote atayetambulishwa kinyume cha katiba ya chama na barua hii kuwa ni mgombea kupitia Chadema.

Aidha kupitia barua hiyo Katibu Mkuu ameikumbusha kwa mara nyingine Tume ya Uchaguzi kujibu barua ya Chadema ya tarehe 25 Novemba 2020 yenye kumb. Na. C/HQ/ADM/20/TU/05/14 ambapo chama kilitaka maelezo ni nani alisaini barua na fomu za waliotangazwa kuwa wabunge viti maalum na kukipatia chama nakala ya nyaraka husika kwa ajili ya kuchukua hatua kwa kuzingatia kuwa Kamati Kuu haikuwahi kufanya uteuzi wala Katibu Mkuu hajawahi kuwasilisha orodha tajwa.
View attachment 2003047
Mungu ibariki Chadema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom