Chadema yatangaza maandamano Moro, Iringa, Rukwa na Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yatangaza maandamano Moro, Iringa, Rukwa na Mbeya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kilimasera, Apr 26, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kitaendelea na ratiba yake ya kufanya maandamano ya amani katika mikoa minne kuanzia wiki ijayo.
  Chama hicho kimesema kuwa ziara hiyo ya kupinga kupanda kwa gharama za maisha, kupanda kwa bei ya umeme na kupinga malipo ya fidia ya Sh. bilioni 94 kwa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans Tanzania Limited itaanzia mkoani Mbeya Alhamisi ya wiki ijayo.
  Chadema kinapinga Dowans kulipwa fedha hizo kama fidia kutokana na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuvunja mkataba wake wa kuzalisha na kuiuzia megawati 100.
  Tanesco iliamuriwa kuilipa Dowans kiasi hicho cha fedha na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC) Novemba, mwaka jana.
  Akizungumza na NIPASHE jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, alisema hakuna mabadiliko yoyote katika kufanikisha maandamano hayo.
  Mbali na Mkoa wa Mbeya, mikoa mingine ambayo Chadema kitafanya maandamano na mikutano ya hadhara ni Ruvuma, Iringa na Morogoro.
  Dk. Slaa alisema kwamba maandamano hayo yataipa serikali fursa ya kuamka na kujitafakari ili kuona ilipokosea mpaka maisha ya Watanzania yakawa magumu.
  Katibu Mkuu huyo alisema kuwa maandamano hayo yatasitishwa ikiwa serikali itatafuta njia mbadala ya kumaliza matatizo yanaoyowakabili Watanzania.
  Mkurugenzi wa Habari wa chama hicho, Erasto Tumbo, alisema maandamano hayo yatawashirikisha viongozi wa kitaifa na wabunge wote wa chama hicho.
  Ziara ya mikoa hiyo ni ya pili baada ya ziara ya kwanza iliyofanyika katika Kanda ya Ziwa inayoingwa na mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga na Kagera.
  Katika ziara hiyo iliyofanyika Februari katika makao makuu ya wilaya na mikoa hiyo kuanzia Mkoa wa Mwanza, Mara, Shinyanga na kumalizikia Kagera, wananchi wengi walihamasika na kushiriki kwa wingi katika maandamano na mikutano ya hadhara bila kuwepo na matukio yoyote ya kuvunja amani.
  Hata hivyo, maandamano hayo yalilalamikiwa na kulaaniwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa, serikali na baadhi ya taasisi kwa madai kuwa yalikuwa na lengo la kuvunja amani na kuiondoa serikali iliyoko madarakani.
  Miongoni mwa wanasiasa wa upinzani waliolaani maandamano hayo ni Mwenyekiti wa Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema; Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP), John Cheyo; Mwenyekiti wa Tadea, John Chipaka ma Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
  Katika hotuba yake ya mwisho wa Februari kwa taifa, Rais Jakaya Kikwete, pia aliyalaani maandamano hayo kwamba yana dalili za kutaka kuchafua amani nchini.
  Rais Kikwete alisema maandamano hayo hayakuwa na nia nzuri kwa kuwa uchaguzi ulikwisha kumalizika na wananchi kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM).
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiwa ziarani mkoani Kagera Machi, mwaka huu aliyalaani maandamano hayo na kusema kuwa ikiwa hali hiyo itaendelea serikali inaweza kufika mahali na kukosa uvumilivu, kauli iliyorejewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira.
  Chama tawala kupitia kwa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati (sasa Naibu Katibu Mkuu CCM Bara), pamoja na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) pia waliyalaani maandamano ya Chadema kwa madai kuwa yalikuwa na nia ya kuwachochea wananchi kuichukia serikali yao.
   
 2. Mpiga Nyoka

  Mpiga Nyoka JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Huo ndo uhusiano CHANYA kati ya Chama cha upinzani na Serikali. CDM endeleeni kuamsha serikali isiyojua kwamba kwanini watu wake ni masikini.
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Safi sana, mbele kwa mbele, mpaka wakimaliza kuvua gamba kichwa kitapondeka:A S 39:
   
 4. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2011
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  viva chadema.....msisahau zanziber na mikoa ya kanda ya kusini
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Tafadhari mleteni Slaa aongoze hayo maandamano maana hapa itakuwa ni zaidi ya TBR, ngoja nielekee moro nikazomee maana koo linawasha.
   
 6. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Tunawasubiri jamani tunawaandalia mapokezi ya nguvu.
   
 7. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,685
  Trophy Points: 280
  hahaha.....tangulia tutakukuta ukipasha koo
   
 8. M

  Mkono JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni wakati muafaka wa kumuumbua Shitambala
   
 9. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Mnawajua al shabab dawat ya hapa moro? Muambieni Slaa aje na Josephine
   
 10. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #10
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Hadi kieleweke
   
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Kwa nini Chadema hizo pesa za ruzuku za Wananchi kila siku wanazitumia kwenye Maandamano yasiokuwa na tija yoyote kwa taifa letu, si bora wangeiga mfano wa mzee Sabodo wajenge visima Tanzania nzima, mpaka sasa hivi maandamano yamekuwa Insubstantial
   
 12. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Safi sana CHADEMA..
  Hakuna kulala mpaka kieleweke
   
 13. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Unategemea nini chama kinaendeshwa na Lema et al
   
 14. z

  zamlock JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  safi sana tuko pamoja na nguvu ya umma iko nyuma yenu mbele kwa mbele
   
 15. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,958
  Trophy Points: 280
  Nafikiri hujui maana ya chama cha siasa.
   
 16. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #16
  Apr 26, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  yani we ni mushenzi kweli unataka chadema ikujengee visima? Hilo ni jukumu la serekal iloyo madarakani
   
 17. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #17
  Apr 26, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  CCM inapata zaidi ya mara nne ya wanazopata CDM. Kwa nn wanazitumia kuhonga vikundi vya kidini kutoa matamko, kukodisha mafuso ya kupeleka watu kwenye mikutano yao, wasiende kuchimba visima?
   
 18. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #18
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nani alikuambia kuwa pesa za ruzuku ya vyama vya siasa hutumika kugharamia miradi ya maendeleo ambayo hutengewa pesa na serikali. Ni lini ulisikia Chama cha Magamba kimetenga pesa za ruzuku au hata kutoka vyanzo vingine kugharamia visima japo hata kijijini kwa JK, makamba au Butiama kwa hayati JKN?
   
 19. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #19
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Waambie kwanza hao watawala wa CCM wanaotumia kodi zetu ovyo bila kutupatia huduma stahili na kuhodhi mali za wananchi kwa faida yao na vitegemezi vyao eg viwanja vya michezo, ''toeni kwanza boriti ktk macho yenu ndo muone vibanzi kwa wenzenu.'' halafu kazi ya ruzuku za chama ni kufanya kazi za siasa za chama si kujenga visima, hela zetu mnazokusanya instead ya kutoa huduma mnanunua mavx afu mnataka ruzuku ya CDM ijenge visima huo si wehu jamani..... Anyways hiyo ruzuku yenu ccm ambayo kwanza ni nyingi kuliko ya vyama vyote mnaifanyyia nini? Au mnajenga huduma za jamii? Bora tunajua ya cdm inatumika kutoa elimu ya uraia yenu? Au ndo mnahongwa kuja kuitetea ccm humu JF
   
 20. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #20
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mawazo ya walevi hayo...
   
Loading...