CHADEMA yataka tume huru kumchunguza Waziri wa Mambo ya Ndani na maandamano, yasema Mtulia anarudi bungeni akinuka damu

Msiwe mnatumia maneno msiyoyajua vema! Kwani kuna puru ngapi katika mwili wako? Na tangu lini kukawa na puru ya mbele na nyuma? Nendeni darasani kusoma na sio kujifunza kutumia simu na kukua!
hivi nyie walimu wa kiswahili bado hamjaamishiwa shule ya msingi?
jinga kabisa ww
 
Kubenea anasema pengine Mtulia asingejiuzulu, Aquilina asingekufa au asingekufa kwa risasi inayotokana maandamano ya ubunge wa Kinondoni.

Kila mtu anajua hii tume sio huru kabisa, na hili wamekua wakiliongelea mara nyingi sana. Ninachojiuliza kwanini waliamua kushiriki wakati wanajua fika kuwa hii tume sio huru? Mtu mwingine anaweza kuja na hoja kuwa wasingeandamana basi huenda asingekufa kwa risasi. Kila mtu atavutia kwake na kumrushia lawama mwenzie. Tumuache marehemu apumzike. Hakuna atakayehukum kwa haki bali Mungu pekee......
 
Yani siku hizi sioni mic(maiki) za ITV, STAR TV au CHANNEL TEN kwenye press za upinzani, kulikoni Tanzania!!
Tanzania ya Magufuli ilishapoteza uhuru wa habari. Kilichobak ni kusifia kila ujinga unaofanywa na magufuli pamoja na genge la wahun wenzake.
 
Mapambano yameanza rasmi , asante kubenea , tulishasema nchi hii wakileta mchezo haitatawalika , mmejionea wenyewe .

Mmeandaa mil 80 ngapi za kusafirisha mtakaowadungua ?
kwan ni lazima yule kapewa hiyo huduma coz hakua miongoni mwa waandamanaji....andamana ufe uone kama utapewa ata sh. mia ata familia ikikataa kukuzika utazikwa na manispaa...upinzani unatakiwa kuelewa kuna baba wa familia na vijana wa familia so huwezi kua chini ya baba afu unataka kumwambia asiende kutembea kisa una mzidi pesa au elimu...wapinzan tatizo ni kujiona wao ndio wanafaa kuliko waliemkuta. hapo lazima mpigwe sana
 
Mkurugunzi ana maswali ya kuijibu...

Nini haswa kilichomsibu mpaka kupelekea kutokea haya yote yaliyotokea...


Cc: mahondaw
 
Unemsahau Bashite??

Huyo ndiyo master mind wao, anasikilizwa hivi sasa CCM zaidi ya PM!

Tetesi zilizopo ni kuwa yeye kama Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi ya Mkoa ndiye aliyeidhinisha wale askari waje na silaha za moto pale penye maandamano, na lengo ilikuwa "kuwamaliza" viongozi wa Chadema.

Lakini Bahati nzuri Mungu bado anawatetea na ndiyo sababu zile risasi ambazo "target" yake zilikuwa viongozi wakuu wa Chadema, kwa muujiza mkubwa "ikadivert" na kwenda kwenye daladala na kutwaa maisha ya yule binti ambaye hakuwa na hatia Akwilina
hakunaga risasi kupinda ikilenga imelenga acha kueleza vitu vya kitoto hapa..
 
Unemsahau Bashite??

Huyo ndiyo master mind wao, anasikilizwa hivi sasa CCM zaidi ya PM!

Tetesi zilizopo ni kuwa yeye kama Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi ya Mkoa ndiye aliyeidhinisha wale askari waje na silaha za moto pale penye maandamano, na lengo ilikuwa "kuwamaliza" viongozi wa Chadema.

Lakini Bahati nzuri Mungu bado anawatetea na ndiyo sababu zile risasi ambazo "target" yake zilikuwa viongozi wakuu wa Chadema, kwa muujiza mkubwa "ikadivert" na kwenda kwenye daladala na kutwaa maisha ya yule binti ambaye hakuwa na hatia Akwilina
Hili mbona linajulikana wazi mkuu? Huu ouvu inasemekana ndiye aliyeubariki yeye na Alli Happi.
Ukifanyika uchunguzi huru ndio mtajua kila kitu. Inasemekama azma ilikua ni kuwamaliza viongozi wakuu wa upinzani na wengine wavunjwe miguu.
 
hivi nyie walimu wa kiswahili bado hamjaamishiwa shule ya msingi?
jinga kabisa ww
Ujinga wangu ndio uelewa wako wewe mburukenge usiejua kuitumia lugha yetu adhimu ya kiswahili! Mnajifanya wasomi na maphd yenu ya kudesa ilihali hamna lolote la kujivunia zaidi ya ligamba lako la kuombea kazi lumumba! Pumbavu mkubwa!
 
Hivi hakunaga msanii aliyewahi kuurudia wimbo huu wa TUME HURU maana naona ushaanza kuchuja sasa, labda tubonge na mwanetu Msaga Sumu auandae tena (aurudie) kwenye huu muziki mpya aina ya SINGELI penginepo unaweza kuwa na mvuto tena...
 
Soweto Arusha aliyeratibu ile issue Ni nani?
Huyu mtu inawezekana aliplan Hata kummaliza ndugu yake Lissu.

Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu sana, taifa limegawanyika kabisa

Watu wanapotea na kukutwa wamekufa kweeeli!!!????
 
"Ndio maaana Maalim Seif, jabali la siasa visiwani alipoporwa matokeo yake ya Urais aliwaambia watu wake msiende barabarani, alijua watu watakufa".

Kutokana naa kauli hiyo ya kubenea, ina maana Chadema pia walijua fika kwamba watu wao watakufa lakini still wakawaambia waingie barabarani waandamane. Na ndiyo hapa tunaweza kuamini kwamba yale maandamano yalipangwa kwa makusudi ili vurugu zitokee watu waumizwe au hata kufa na hivyo wapate huruma ya wananchi katika uchaguzi. Matokeo yake vifo vimetokea na uchaguzi wameshindwa. Lakini mzigo wa lawama wanawatupia watu wengine. Kwa maoni yangu CDM wanawajibika kwa hiyo michuruzi ya Damu na vifo.
 
Mwigulu ndio mpanga njama zote za uovu wa kisiasa , akichunguzwa kaisha !
Ulimsikia Mdee na Mbowe siku ya tarehe 16/02/2018 wakati wa kampeni kule mwananyamala? Kama hujui. Mdee alisema hivi;

"Tumepata nafasi... Tumepata nafasi adimu sana!! Wengine wametoka Sumbawanga.. Wengine wametoka Mara.. wamekuja kwa nauli zao.. Kwa nguvu zao..kuungana na Wanakinondoni.. *TUKAMCHINJE MAGUFULI.., NA VIBARAKA WAKE WOTE!* - *Mhe. Halima Mdee (Mb)Kawe."

Mbowe nae akenena hivi;

“Lazima tukubali kubeba majeneza! Lazima tukubali nini...?? (MKUTANO UNAJIBU; *‘kubeba majenezaa!!’*) Matokeo ya Watanzania 100 wakataokufa wataleta haki katika Nchi hii!.. - *Mhe. FREEMAN MBOWE Mwenyekiti wa CHADEMA (Taifa)

Kwa kauli hizi... kati ya mwigulu na hawa, nani aliyepanga njama za uovu wa kisiasa?
Kutoka ofisi ya CHADEMA kanda ya Pwani zilizopo Magomeni, Anayeongea ni mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea ambae anadai tume huru kumchunguza waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba na maandamano aliyodai ya amani kwenda kwa msimamizi wa Uchaguzi. Kubenea anasema wanaungana na wote wanaomtaka waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba awajibike kwa kujiuzulu.

Anasema walikuwa na mvutano wa muda mrefu na mkurugenzi juu ya viapo, Amesema waliandamana kwa siku husika ilikua Ijumaa na siku inayofata Jumamosi ambayo pia ni siku ya uchaguzi.

Kubenea anasema alimsaidia Maulid fedha na publicity kwenye magazeti yake wakati anagombea ubunge kupitia CUF na Mungu akamjaliia kuingia bungeni bila kumwaga damu ya mtu lakini akaacha ubunge kwa makusudi akidai anampenda Rais John Magufuli na sasa wamemlazimisha kutangazwa kuwa mbunge wa Kinondoni akiwa ananuka damu.

"Leo Mtulia anakwenda Bungeni na michirizi ya damu na vifo, madaraka ya namna hii kwa mtu mwenye kujielewa, roho ya utu hayaitaji na ndio maaana Maalim Seif, jabali la siasa visiwani alipoporwa matokeo yake ya Urais aliwaambia watu wake msiende barabarani, alijua watu watakufa". Alisema Kubenea.

Kubenea aliongeza, Mauli alishakuwa mbunge na akatoka kwa hiari yake kwa fedha au chochote alichoahidiwa, leo anarudi bungeni akiwa ananuka damu na kuhoji atawahudumiaje wananchi wa Kinondoni katika mazingira hayo.

Kubenea anasema pengine Mtulia asingejiuzulu, Aquilina asingekufa au asingekufa kwa risasi inayotokana maandamano ya ubunge wa Kinondoni.

Kubenea anasema ili Jeshi la polisi lijenge heshima lazima limuhoji mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni, kwanini alizuia fomu za mawakala na kusababisha machafuka, maandamano na akasababisha mauaji.

CHADEMA imesema itakaa na mgombea wake, Salum Mwalimu kuangalia hatua gani inaweza kuchukuwa lakini hazitakuwa za kutumia nguvu ama vurugu, imekishukuru chama cha wananchi CUF katika kuwaunga mkono.
 
NDUGU MEXENE MELLO et al.,
Naomba mnipige ban ya miaka miwili mpaka 2020.siwezi kuendelea kusoma maoni ya / comment ya wana Lumumba wapumbafu na machoko.
Ila endeleeni kushangilia, wakati bado unakuja .Magufuri kaweka vyombo vya habari kwapani, mahakama kwapani, jeshi la polisi kwani, bunge kwapani,shughuli za kisiasa na democrasia kwapani, taasisi za kidini kwapani nadhani uchunguzi kakobe mmeusikia. Shangilieni ,imbeni mtakavyo weza, tukaneni vyama pinzani mtakavyo weza, nunueni madiwani na wabunge mtakavyo weza ,ueni upinzani kadiri nguvu zenu zitakavyo weza.Ule mwisho badoo, Magufuri akianza kuuwa watu wake ndani ya ccm akihisi wanamuhujumu na wengine ndani ya chama chake , ndipo ule wakati uliotabiriwa utakuwa umewadia. Mtatafuta pa kukimbilia mtakosa, mtalia na kusaga meno ,mtaomboleza lakini hamtaona msaada wala hakuta kuwa na kimbilio. Endeleeni kushangilia, endeleeni kusifia.....siku zaja.
hahahahah, ameomba akapewa hahahahahaha
 
Back
Top Bottom