Chadema yataka Jaji Mkuu mpya awe chachu ya Katiba Mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yataka Jaji Mkuu mpya awe chachu ya Katiba Mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Dec 28, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  Jaji Othman, awe chachu ya mabadiliko ya Katiba mpya - CHADEMA


  na Janet Josiah


  [​IMG] CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtaka Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, kuendeleza mapambano ya kudai na kuandikwa kwa Katiba mpya ambayo katika kipindi hiki imezua mjadala mkali. Jaji Othman aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, juzi na kuapishwa jana katika viwanja vya Ikulu, kuchukua nafasi ya Jaji Augustino Ramadhan, ambaye anastaafu kwa mujibu wa sheria kuanzia leo.
  Akizungumza na Tanzania Daima, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Erasto Tumbo, alisema chama chao kinaamini kuwa Jaji Othman ataendeleza mjadala huo kama alivyouanza Jaji Ramadhan ambaye alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa umefika wakati sasa Watanzania wakatoa maoni kuhusu uwepo wa Katiba mpya.
  “CHADEMA inamtaka Jaji Othman asiwe kikwazo katika mjadala huo, ila inamtaka awe msaada katika zoezi hili linaloendelea ili kuwapa Watanzania haki yao ya msingi ambayo tunaamini wameidai kwa muda mrefu,” alisema Tumbo.
  Tumbo alisema kutokana na wadhifa mkubwa aliopewa na Rais kama Jaji Mkuu wa Tanzania na kuongoza mahakama kama mhimili wa tatu wa dola, anayo kila sababu ya kukabiliana na changamoto alizozikuta ukiwamo mjadala huo.
  Alisema miongoni mwa changamoto hizo ni ile ya mahakama kufanya maamuzi ya kukubali kuwepo kwa mgombea binafsi, hoja ambayo ilimfanya Jaji Ramdhan apate kigugumizi na kuirudisha bungeni ambako ilishindikana.
  Kabla ya uteuzi huo Jaji Othman alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa na mtetezi wa Haki za Binadamu Kusini mwa Sudan, hadi mwezi Agosti 2011.
  Jaji Othman alizaliwa Januari Mosi, 1952 na ana shahada ya kwanza ya sheria (LLB) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na shahada ya uzamili (MA) kutoka Chuo Kikuu cha Webster, Geneva-Uswisi.
  Amewahi kuwa Makamu wa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Rwanda huko Arusha na amewahi kushika nafasi sawa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali huko Timor Mashariki.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  Sina uhakika kama Jaji Mkuu ana mchango kwenye katiba mpya................hii ni kazi yetu sote hususani wapigakura.............ambao ndiyo tuna karata turufu dhidi ya wale owte ambao mara tukiisha wachagua hujifanyia watakavyo...............
   
 3. N

  Nyota Njema Senior Member

  #3
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuendelee na mchakato uliokwisha anza wa kudai Katiba Mpya. Hawa wateule wa Mkwere ni bahati sana kuwa na mtazamo walionao wananchi wengi. Mimi pia naamini kuwa wataalam wengi wakiwemo wanasheria kama majaji wana maoni mazuri na mapenzi na nchi yetu. mfano ni jaji mkuu aliyemaliza muda wake, ameonyesha kuweka maslahi ya nchi mbele zaidi ya maslahi binafsi ya chama au kikundi cha watu flani wachache.

  Mtihani umebaki kwa huyu mtaalam mwingine wa sheria aliyeteuliwa kuongoza huu mhimili mwingine wa tatu wa dola. Akiipenda zaidi nchi kuliko maslahi ya mteuzi wake mambo yatakuwa mazuri, lakini akitepeta kama tulivyoona kwa mwanasheria mkuu wa serikali ya Mkwere basi huo utakuwa mwanzo hata wa watanzania kutoiamini sekta ya mahakama anayoiongoza. Tusubiri tuone kama tumepata mtu katika muhimili huu, maana mingine miwili imepatikana kwa uchakachuzi!
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  CHADEMA yampongeza Jaji Chande


  Na Mwandishi wetu

  SIKU moja baada ya uteuzi wa Jaji Mkuu mpya wa Tanzania, Mohamed Chande, kisha kuapishwa jana, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa pongezi, kikimuahidi ushirikiano, lakini kikitoa tahadhari pia.Akizungumza
  na Majira jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Bw. Erasto Tumbo, alisema kuwa chama hicho kinapongeza uteuzi huo na kumtakia heri Jaji Mkuu Chande katika majukumu yake mapya ya kuongoza moja ya mihimili ya dola, mahakama.

  "CHADEMA tunatoa pongezi za dhati kwa Jaji Chande kwa kuteuliwa kuwa Jaji Mkuu...lakini tunaomba uteuzi wake usije ukawa kikwazo na kuturudisha nyuma hasa katika vuguvugu la sasa la katiba mpya...aige mfano wa aliyemtangulia, ambaye aliweka bayana msimamo wake.

  "Jaji Mkuu Chande ni mtu mkubwa, atambue kuwa sauti yake ina nguvu na inasikilizwa na watu wengi, tunatarajia atakuwa jaji mkuu makini...lakini pia asiwe tatizo kama aliyepita ambaye alishindwa na kuacha kiporo suala la mgombea binafsi," alisema Bw. Tumbo.

  Alisema kuwa suala la mgombea binafsi liliwashangaza Watanzansia wengi baada ya mahakama kushindwa kutoa ufafanuzi wa kikatiba na kisheria ambayo ni majukumu ya mhimili huo, badala yake likarusha mpira kwa bunge kwa kusema kuwa katiba ni suala la kisiasa.

  "Kwa kweli hakikuwa kitu cha kawaida, wananchi wamekuwa wakitegemea kuwa mahakamani ni mahali ambako ufafanuzi wa kisheria na katiba wa masuala kama hayo unapatikana.

  "Lakini mahakama chini ya jaji mkuu aliyepita ikashindwa na kuacha kiporo suala la mgombea binafsi...tunatumaini Jaji Chande atatuongoza vizuri hasa katika kuelekea kupata katiba mpya," alisema Bw. Tumbo.
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  Nilifikiri Chadema kama Chama cha siasa kinachodai ni chama makini kingelikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kinakosoa uteuzi huu kwa sababu unakinzana na mahitaji ya harakati za kudai katiba mpya...kwa maana ya kuwa Bunge lilipaswa kushirikishwa......................hivyo kutoa pongezi hizi ni kujikaanga kwa mafuta yao wenyewe................na pengine ndiyo maana AG anapata ubavu wa kuhoji katiba Mpya ya nini?
   
 6. N

  Nyota Njema Senior Member

  #6
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu Rutashubanyuma, nakusifu kwa kuendelea na hii mada ya Jaji Mkuu mpya ingawa naona haina wachangiaji wengi kwa sasa. Tuna haja kubwa ya kuujadili huu muhilimili muhimu wa dola unaohusika na kutoa haki kwa umma. Hofu kubwa ya wengi ni yule aliyemteua, yawezekana kateua yule ambaye hatamkosesha usingizi katika utendaji wake.

  Taifa bado lipo kwenye mashaka makubwa na utawala uliopo kutokana na yale yanayotokea katika maisha ya kila siku. Hatuna viongozi wa juu kabisa wenye uwezo wa kukemea maovu yanayotokea nchini na wengine sasa wanahusishwa moja kwa moja na maovu hayo. Rais wetu na DOWANS, jaji mkuu (mstaafu) na kuachia wahalifu wenye pesa (tusubiri habari kwenye vyombo vya habari vya wiki, wiki hii), na mengineyo mengi.
   
Loading...