CHADEMA yataka bei ya ukumbi Ikulu ili wengine nao wakiwa na vikao vyao wasisite kwenda

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka Serikali kuweka wazi utaratibu unaosemwa kwamba ulifuatwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), kufanya mkutano wao wa Chama Ikulu jijini Dar es salaam, ili kila mmoja ajue iwapo atahitaji kwenda kufanya mkutano hapo.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bwana John Mrema, amesema kama ukumbi huo wa Ikulu unaruhusiwa kifanyika mkutano na mtu yeyote, basi waweke wazi utaratibu wa bei ili wengine nao wakiwa na vikao vyao wasisite kwenda ili kuongeza pato la Taifa.

Chanzo: East Africa Television
CHADEMA ENDELEENI KUFANYA MIKUTANO YENU CHINI YA MTI KAMA MLIVYOZOEA. MSIJE MKATUHARIBIA IKULU. KUWAKARIBISHA JUICE TU MLITAKA KUGOMBANIA JE VIKAO. KAENI HUKO HUKO UFIPA.
 
Kama kibarazani pale makao makuu ya Chadema hapatoshi, muombeni Mwenyekiti wa TLP awasaidie gharama za ukumbi wa Megereza (Ukonga).
 
Point ni nini?? Kumbi zimeisha?? Wivu utawaua wana ufipa.
....Habari ya ufipa, unyanyembe, lumumba unajua wewe, mimi huku Likawage siyajui hayo. Ikulu ni majengo ya serikali ya watanzania wote, sasa kama mmeamua kuifanya kumbi za mikutano ya vyama na mengineyo basi wekeni bei sasa.
 
Arusha yeye ndiye alikiuka taratibu! Sherehe za kijeshi hufanyika chuoni Monduri kila mwaka! Walipeleka uwanja wa ccm pale Arusha kwa ajili ya kutimiza mipango yao ya kisiasa! Hata hivyo vile viwanja vilijengwa na wananchi wote enzi za wazee wetu!
Hakuna kitu kinachoniuma hapa duniani kama ccm kuhodhi mali zilizotafutwa/jengwa na watanzania wote kama viwanja vya mpira kuvifanya vyao. Ilaaniwe hata hukumu ya mahakama iliyokaa chini ya majaji wenye kadi za ccm kufanya uamuzi wa hovyo kuidhinisha mali za wananchi kuwa za ccm. Kwa uanasheria wangu sijawahi sikia duniani popote mahakama ikaendelea kuamua kesi ambayo mdai ameachana nayo, dawa ilikuwa ni kuifuta kesi na sio kuamua on merit!! Naamini lawyers mnanielewa hapo. Naamini kuna siku tutapata "Hon. Maranga" wetu wa kurudisha mali za watanzania zinazohodhiwa na miccm
 
....Habari ya ufipa, unyanyembe, lumumba unajua wewe, mimi huku Likawage siyajui hayo. Ikulu ni majengo ya serikali ya watanzania wote, sasa kama mmeamua kuifanya kumbi za mikutano ya vyama na mengineyo basi wekeni bei sasa.
Sasa kama unakubali ikulu nibya serikali, serikali kwani ninya chadema??
Alafu mliomba mkanyimwa??
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka Serikali kuweka wazi utaratibu unaosemwa kwamba ulifuatwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), kufanya mkutano wao wa Chama Ikulu jijini Dar es salaam, ili kila mmoja ajue iwapo atahitaji kwenda kufanya mkutano hapo.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bwana John Mrema, amesema kama ukumbi huo wa Ikulu unaruhusiwa kifanyika mkutano na mtu yeyote, basi waweke wazi utaratibu wa bei ili wengine nao wakiwa na vikao vyao wasisite kwenda ili kuongeza pato la Taifa.

Chanzo: East Africa Television
Ndo hoja zao. Sitashangaa kama waliita press conference, and then na uliza tu kwa mambo yetu ya kibongo hawa waandishi hawapewei bahashaaaaa.
 
Washinde Uchaguzi kwanza, hiyo ndo bei yake!
Kwa refa aina ya lubuva...unategemea watashinda uchaguzi??
Kama wanakataa kutangaza madiwani wa upinzani ..watatangaza rais??
[HASHTAG]#ushahid[/HASHTAG] wa flashi ya nassari ...
 
Safi sana Mzee wa Taratibu alidai chama chochote kinaruhusiwa kufanya mikutano yao ikulu ila naona ugumu uliopo sababu kama tuu huku uraiani kila siku wanakamatwa wakifanya mikutano ndio itakuwa ikulu....??? Utaambiwa Inteligensia ya inteligensia inaonyesha kutakuwa na uvunjifu wa amani ikulu... Hahahahahaahahahahahahahah Serikali yetu haiishi Vioja...
 
Hili Si jambo zuri likemewe kwa nguvu zote...ikulu Ni pahala swafi Si pa kuhamishia vikao vya chama...ikulu Si Mali ya ccm Bali Ni ya watanzania wote
 
"...in a week democratic country it is not possible to differentiate between state activities and ruling party activities...."

Desmond Tutu
 
Mambo mengine si ya kuyang'ang'ania sana...
Wapinzani wasiwe watu wa matukio,kila likitokea jambo lishikiwe bango!
Funika kombe mwanaharamu apite...kuna mambo mengi ya kujadili kuliko hilo jambo!
kilichobaki ni huruma ya wanachi tu ndo wanataka
 
Back
Top Bottom