CHADEMA yataka bei ya ukumbi Ikulu ili wengine nao wakiwa na vikao vyao wasisite kwenda

Pole pole aliongea mangapi jana kwa matukio yaliyotokea hivi karibuni...kwani huko lumumba hakuna mambo ya msingi yakufanya

Infact umesomeka mfuasi wa mkulu

Muamala umeongezeka kwa dau la buku 7..
Wala mimi sio mfuasi wa Mkuu,ila naongea ninachoamini.Mambo mengine sio ya kujadili wiki nzima!
 
waweke wazi huo utaratibu ili tujichange na kuweza kuutumia kufanya tafrija ya kumkaribisha nyumbani Mheshimiwa sana, Lissu baada ya pepo na njama zake kushindwa !

Aaaah ! Kwa hiyo mkipewa dola tutachangishwa mwanzo mwisho!
 
Mambo mengine si ya kuyang'ang'ania sana...
Wapinzani wasiwe watu wa matukio,kila likitokea jambo lishikiwe bango!
Funika kombe mwanaharamu apite...kuna mambo mengi ya kujadili kuliko hilo jambo!

Hii mada haikuletwa na CHADEMA bali ililetwa kwenye kesi ya kufoji vyeti na hivyo ikawa mada ya utetezi. Kuweni na akili pana walau kiduchu.
 
Ndio maana hawatafanikiwa kushika dola, chadema, yaani hoja zao ziko reactive sasa hivi! Hawana hoja mpaka sisiemu wafanye kitu ndo wanapata cha kusema.
Jamaa yule sasa ni wazi kuwa ni liability, kapofusha akili zote za ufipa.
Ni ngumu sana kufunga goli kama timu pinzani haijafanya makosa
 
Ukweli wanaweza kuwapa utaratibu na mkalipia lakn siku ya mkutano/kikao mkaambiwa ukumbi unashughuli maalum ni vema mkapanga siku ingine, ikawa imekula kwenu.
 
Mnapenda malumbano kila kukicha yapo mambo mengi muhimu ya kufanya kujenga taifa hili
Yaibue tuchangie aanza sasa kuibua usikae kusubir ya cdm, na wewe hunatofaut na wale viongozi wetu wanaowambia vijana msitegemee ajira za serikali jiari lakn yeye anapigana kuona mwanae anaajiriwa.
 
Haliwezi kuwa kosa kwa kipimo chako.Kwa vile hujui tofauti ya serikali na chama.Chama kitampeleka rais na watendaji wa office ya Rais.Ila kuhamishia office yao. Issue ni kwamba kwa hii akili ni ngumu wewe ndio unatembea na mavi umeshajinyea ktk chupi.
Ahaa sawa akifanya kubenea na chadema (chadeka) sawa, ccm baya!!
 
Waende kufanya booking kwa mhusika wataambiwa.
Aahhh samahani nimesahau wanaweza kufuatiliwa na gari wakalitilia mashaka ila wasishitaki polisi wawndw insta na Facebook
 
Mambo mengine si ya kuyang'ang'ania sana...
Wapinzani wasiwe watu wa matukio,kila likitokea jambo lishikiwe bango!
Funika kombe mwanaharamu apite...kuna mambo mengi ya kujadili kuliko hilo jambo!
Tatizo hawana agenda, bila matukio hawana cha kusema. Sera ziliondoka na Dr. Slaa.
 
Yaibue tuchangie aanza sasa kuibua usikae kusubir ya cdm, na wewe hunatofaut na wale viongozi wetu wanaowambia vijana msitegemee ajira za serikali jiari lakn yeye anapigana kuona mwanae anaajiriwa.
Hahaha umenena vyema mkoa wa songwe una chuma cha pua wameshindwa kukishauri chama tawala kuelekeza nguvu huko kuna mafuta ziwa rukwa nayo wameshindwa n.k ila kila kukicha malumbano tu aibu kwa taifa kuwa na upinzani huo wabadilike
 
Watu wasipo hoji Uhalali wa CCM kufanya Mikutano Ikulu unataka Wahoji nini? Kwani ikulu ni Mali ya CCM au Mali ya JAMHURI? Kwanini CCM waitumie Mali ya Jamhuri Kwa Vikao vya Chama?

Wacheni Uzezeta Huo! Munapodadidisiwa Jibuni hoja sio Mudogoshe hoja za Watu baada Ya Nyinyi Mabashite na Mabashitess kukosa majibu..
Ni wivu tu, hamna kingine!!
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka Serikali kuweka wazi utaratibu unaosemwa kwamba ulifuatwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), kufanya mkutano wao wa Chama Ikulu jijini Dar es salaam, ili kila mmoja ajue iwapo atahitaji kwenda kufanya mkutano hapo.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bwana John Mrema, amesema kama ukumbi huo wa Ikulu unaruhusiwa kifanyika mkutano na mtu yeyote, basi waweke wazi utaratibu wa bei ili wengine nao wakiwa na vikao vyao wasisite kwenda ili kuongeza pato la Taifa.

Chanzo: East Africa Television

Poleni Chadema, mmekuwa kama kunguru
 
Back
Top Bottom