CHADEMA yashtuka kampeni chafu

SO now is not Upinzani against CCM; its Upinzani against Upinzani; Hehehe very interesting; nilishangaa CUF wakikusanyana Dar badala ya rasilimali zao kuzipeleka Mbeya vijijini; ngoja tuone mwisho wake

Chadema amesahau kama CUF ni Chama nambari mbili ndani ya Tanzania,anachojaribu kutaka kufanya Chadema ni kutumia sloganz za ufissadi kupiku wengine kwa kutumia hilo anataka kila sehemu aachiwe yeye japo hakubaliki,vyama vimepatana kuwa pale mgombea anapokubalika basi wapinzani wajiunge na kumchagua anaekubalika, mpinzani ambae amekubalika katika uchafuzi mkuu uliopita kwa upande wa Mbeya nambari mbili alikuwa ni mgombea wa CUF sasa Chadema walikuwa na kitu gani cha kukataa kumuunga mkono kama si uchoyo,ina maana kila unapotokea uchaguzi basi muungwaji mkono awe ni kutoka Chadema tu haya ndio yale yale ya Raisi wa Zanzibar lazima atoke Unguja na hilo ndilo amuzi la CCM na ndio Chadema wanavyotaka kwa jinsi inavyoonekana,hapa walikuwa Chadema waonyeshe uungwana lakini umewashinda .
 
Do you mean its smooth that 2005=2009? (Untrue)
So no political growth? ( Untrue)
So namba mbili 2005 aachiwe tena awe namba mbili 2009? (ni kukubali kushindwa tena)
CUF Tarime iliunga mkono kwa mkakati upi kama chama? (walishakataa wao kabla kwa maneno ya Lipumba/Mbatia/Mrema wakimsingizia mbowe kuhusika na kifo cha Wangwe)
Kwa nini rasilimali za mkutano wa manzese zisipelekwe Mbeya? Wakishindwa je
 
Chadema amesahau kama CUF ni Chama nambari mbili ndani ya Tanzania,anachojaribu kutaka kufanya Chadema ni kutumia sloganz za ufissadi kupiku wengine kwa kutumia hilo anataka kila sehemu aachiwe yeye japo hakubaliki,vyama vimepatana kuwa pale mgombea anapokubalika basi wapinzani wajiunge na kumchagua anaekubalika, mpinzani ambae amekubalika katika uchafuzi mkuu uliopita kwa upande wa Mbeya nambari mbili alikuwa ni mgombea wa CUF sasa Chadema walikuwa na kitu gani cha kukataa kumuunga mkono kama si uchoyo,ina maana kila unapotokea uchaguzi basi muungwaji mkono awe ni kutoka Chadema tu haya ndio yale yale ya Raisi wa Zanzibar lazima atoke Unguja na hilo ndilo amuzi la CCM na ndio Chadema wanavyotaka kwa jinsi inavyoonekana,hapa walikuwa Chadema waonyeshe uungwana lakini umewashinda .

Mbona TARIME CUF waliwatosa CHADEMA
 
Kama siyo ubinafsi wa watu fulani, Chadema ndio kingekuwa chama bora kabisa hapa nchini tangu mwaka 1995.

Baada ya kutoka CCMS, Mrema alikuwa tayari kujiunga na Chadema endapo angehakikishiwa nafasi ya kugombea Urais nafasi ambayo mzee Mtei alikuwa akiiwania pia. Hatimaye Mtei na Chadema wakakosa vyote - Mrema na kugombea Urais.

Ikumbukwe vizuri kuwa wakati huo chama kilichokuwa kimejipanga vizuri kiuongozi kilikuwa chadema chini ya akina Mzee Mtei, Bob Makani, Eric Mchata, Edward Barongo, Brown Ngwilulupi na wengineo pamoja na uwezo mzuri wa kiuchumi. NCCR Kilikuwa kimejipanga na timu ya wasomi ambao hawakuwa na nguvu za kiuchumi - Mrema aliamua kwenda huko na kukiongezea nguvu na umaarufu chama hicho. CUF walikuwa Zanzibar tu na nguvu kidogo kanda ya ziwa iliyojengwa na Mzee Mapalala. Hata Lipumba mwenyewe alikuwa bado hajulikani kabisa katika medani za kisiasa.

Bob Nyanga Makani pengine ndiye aliyepata kuwa kiongozi mwenye dhamira njema ndani ya Chadema. Mwaka 2000 alikubali Chadema isisimamishe mgombea na kukiunga mkono chama cha CUF katika ngazi ya Urais na kuachiana majimbo. Hata hivyo hili halikuwa na nguvu za kisheria bali makubaliano nyenye nia njema.

Ni muhimu kusema hapa kwamba tofauti ya kutosimamisha mgombea mwaka 1995 na 2000ni kuwa wakati mwanzoni Mzee Mtei alijiona hana uwezo wa kushinda kutokana na nguvu ya Mrema, Makani alifanya hivyo kwadhamira njema tu kwakuwa nguvu ya Lipumba haikuwa kubwa kiasi hicho. Mtei hakuacha kwa kupenda bali kulazimishwa na hali.

Unaweza kuishambulia CCM kwa njia ya Mbwa mwitu kwa Simba. Hili dude kubwa na sio rahisi kulishinda mara moja. Njia pekee ilikuwa ni kuachiana maeneo kwa chama chenye nguvu katika eneo husika.

Ilitia faraja katika chaguzi za Kiteto na Tarime kwamba angalau kulikuwa na kuachiana hata hivyo yaliyotokea Mbeya yanathibitisha usanii na unafiki wa wanasiasa wetu. Wasichokitambua Chadema ni kuwa kwa usanii wao wa Mbeya wamewasaliti wananchi sio vyama vingine vya upinzani.

Kosa kubwa walilofanya Chadema ni kujiona tayari wana nguvu kubwa wakati wana wabunge wakuchaguliwa wasiofika kumi kati ya wabunge mamia!

Kwa Mbowe kufuata ubinafsi wa mkwe wake amekinyima Chadema nafasi nyingine ya kuwa chama kinachokubalika zaidi hapa nchini.

NN
 
Nugunungu,
OK, CUF wanyakue hii nafasi wawe chama kitakachokubalika zaidi Tanzania
 
Umejaza uongo weeeee. Kiteto hakuna chama ambacho kingeweza hata kusogeza mguu wakati ule, Kimesera alikuwa na nguvu hivyo vyama vililazimika kumuunga mkono. CUF haikuwepo kabisa kule. Pamoja na kutangaza kumuunga mkono Kimesera si Lipumba, Mrema wala Mbatia waliokwenda kule. Waliishia Dar na kuacha CHADEMA ipambane yenyewe.

Tarime ndio kabisa, si Lipumba wala Mrema waliounga mkono CHADEMA. Wote walimuunga mkono Mbatia. CHADEMA ikawashinda peke yake na NCCR ikapata kura za aibu kwenye ubunge na CUF ikapata kura za aibu kwenye uchaguzi wa udiwani Tarime mjini.

Acha historia yenye kupotosha, Nungu Nungu umeibuka sasa ukidhani utaichoma choma CHADEMA kumbe miiba yako imepita pembeni

Asha
 
Kumbukumbu zangu zinanieleza kuwa tayari vyama vya NCCR, TLP na CUF vilishasitisha ushirikiano wa vyama kwenye chaguzi mpaka kwanza kanuni za ushirikiano zisainiwe. Walifanya hivyo ili kutoa mwanya kwa NCCR kusimamisha mgombea Tarime na kuungwa mkono na CUF na TLP bila ya kuihusisha CHADEMA. Sasa kama hali ni hivyo, mbona wameshirikiana Mbeya Vijijini bila kwanza kuwa kanuni za ushirikiano? Halafu mbona wanailazimisha CHADEMA iwepo? Kama CHADEMA haina nguvu mbeya vijijini kwanini wanahainga nayo badala ya kuhangaika na CCM?

Mbowe akataa kusaini maazimio

2008-08-20 13:01:24
Na Dunstan Bahai

Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, amekataa kusaini maazimio ya kikao cha wenyeviti wa ushirikiano wa vyama vinne vya siasa kutokana na kutokubaliana na yaliyomo kwenye maazimio hayo.

Katika barua yake aliyowaandikia wenyeviti wenzake wa NCCR-Mageuzi, CUF na TLP, ambayo Nipashe imepata nakala yake, Bw. Mbowe alisema katika maazimio hayo kuna kipengele ambacho hakukipenda.

``Katika taarifa hiyo, pamoja na masuala mengine, ina mstari mmoja wenye azimio kwamba katika kipindi hiki ambacho kanuni zinakamilishwa, vyama hivyo (vyama vyetu) vitaendelea kubadilishana mawazo kwa lengo la kulitumikia taifa.

``Kutokana na azimio hilo, nimesita kusaini tamko husika na narejesha kwenu ili lifanyiwe tena marekebisho yanayostahili kutokana na sababu (nilizonazo)�`` alisema kwenye barua yake hiyo.

Miongoni mwa sababu hizo, alizitaja kuwa ni azimio hilo kutokuwa sehemu ya maazimio ya kikao chao cha Agosti 13, mwaka huu na hakuna kitu kama hicho kilichojadiliwa.

Kitu kingine kilichomfanya asisaini, alisema ni wasiwasi wake kuwa taarifa hiyo iliandaliwa baada ya Agosti 14, kabla ya kumfikia yeye siku mbili baada ya wenzake kusaini.

``Taarifa hiyo ikitolewa kwa vyombo vya habari na kwa umma inaweza kutafsiriwa kwamba tumeamua kusitisha ushirikiano katika mambo mengine isipokuwa `kubadilishana mawazo tu,`` ilieleza barua hiyo ya Bw. Mbowe kwa wenyeviti wenzake.

* SOURCE: Nipashe
 
Kama siyo ubinafsi wa watu fulani, Chadema ndio kingekuwa chama bora kabisa hapa nchini tangu mwaka 1995.

Baada ya kutoka CCMS, Mrema alikuwa tayari kujiunga na Chadema endapo angehakikishiwa nafasi ya kugombea Urais nafasi ambayo mzee Mtei alikuwa akiiwania pia. Hatimaye Mtei na Chadema wakakosa vyote - Mrema na kugombea Urais.

Ikumbukwe vizuri kuwa wakati huo chama kilichokuwa kimejipanga vizuri kiuongozi kilikuwa chadema chini ya akina Mzee Mtei, Bob Makani, Eric Mchata, Edward Barongo, Brown Ngwilulupi na wengineo pamoja na uwezo mzuri wa kiuchumi. NCCR Kilikuwa kimejipanga na timu ya wasomi ambao hawakuwa na nguvu za kiuchumi - Mrema aliamua kwenda huko na kukiongezea nguvu na umaarufu chama hicho. CUF walikuwa Zanzibar tu na nguvu kidogo kanda ya ziwa iliyojengwa na Mzee Mapalala. Hata Lipumba mwenyewe alikuwa bado hajulikani kabisa katika medani za kisiasa.

Bob Nyanga Makani pengine ndiye aliyepata kuwa kiongozi mwenye dhamira njema ndani ya Chadema. Mwaka 2000 alikubali Chadema isisimamishe mgombea na kukiunga mkono chama cha CUF katika ngazi ya Urais na kuachiana majimbo. Hata hivyo hili halikuwa na nguvu za kisheria bali makubaliano nyenye nia njema.

Ni muhimu kusema hapa kwamba tofauti ya kutosimamisha mgombea mwaka 1995 na 2000ni kuwa wakati mwanzoni Mzee Mtei alijiona hana uwezo wa kushinda kutokana na nguvu ya Mrema, Makani alifanya hivyo kwadhamira njema tu kwakuwa nguvu ya Lipumba haikuwa kubwa kiasi hicho. Mtei hakuacha kwa kupenda bali kulazimishwa na hali.

Unaweza kuishambulia CCM kwa njia ya Mbwa mwitu kwa Simba. Hili dude kubwa na sio rahisi kulishinda mara moja. Njia pekee ilikuwa ni kuachiana maeneo kwa chama chenye nguvu katika eneo husika.

Ilitia faraja katika chaguzi za Kiteto na Tarime kwamba angalau kulikuwa na kuachiana hata hivyo yaliyotokea Mbeya yanathibitisha usanii na unafiki wa wanasiasa wetu. Wasichokitambua Chadema ni kuwa kwa usanii wao wa Mbeya wamewasaliti wananchi sio vyama vingine vya upinzani.

Kosa kubwa walilofanya Chadema ni kujiona tayari wana nguvu kubwa wakati wana wabunge wakuchaguliwa wasiofika kumi kati ya wabunge mamia!

Kwa Mbowe kufuata ubinafsi wa mkwe wake amekinyima Chadema nafasi nyingine ya kuwa chama kinachokubalika zaidi hapa nchini.

NN

Mkuu Nungunungu.
Umeelezea vizuri kupitiliza saaaaana.
Chadema imefanyakazi nzuri ya kuwafichua mafisadi bila uoga lakini pengine hii inaweza ikawa ni sababu ya wao kujiona ni chama pekee cha upinzani.
Chadema wanahitaji kuelewa kwamba ushirikiano wa vyama vya upinzania si jambo la kuchagua bali nila lazima kama kweli wanataka kuiondoa CCM madarakani.
{1}CCM bado ni chama chenye nguvu na kina mtandao mkubwa ulioenea kila kona ya Tanzania.
{2}CCM ina Asset nyingi na vyanzo vingi vya mapato
{3}CCM ina dola
{4}Tume ya uchaguzi ni mali ya CCM

Chadema lazima waelewe si kazi rahisi kuiondoa CCM madarakani bila kuunganisha nguvu ndogo waliyonayo wapinzani.
Lazima ni seme kweli kwamba ushirikiano wa wapinzani una matatizo lakini hatupaswi kukimbia matatizo tunatakiwa kuyatatuwa.
 
Umejaza uongo weeeee. Kiteto hakuna chama ambacho kingeweza hata kusogeza mguu wakati ule, Kimesera alikuwa na nguvu hivyo vyama vililazimika kumuunga mkono. CUF haikuwepo kabisa kule. Pamoja na kutangaza kumuunga mkono Kimesera si Lipumba, Mrema wala Mbatia waliokwenda kule. Waliishia Dar na kuacha CHADEMA ipambane yenyewe.

Tarime ndio kabisa, si Lipumba wala Mrema waliounga mkono CHADEMA. Wote walimuunga mkono Mbatia. CHADEMA ikawashinda peke yake na NCCR ikapata kura za aibu kwenye ubunge na CUF ikapata kura za aibu kwenye uchaguzi wa udiwani Tarime mjini.

Acha historia yenye kupotosha, Nungu Nungu umeibuka sasa ukidhani utaichoma choma CHADEMA kumbe miiba yako imepita pembeni

Asha

Asha
Kama Kimesera alikuwa na nguvu mbona alishindwa.
 
Mkuu Nungunungu.
Umeelezea vizuri kupitiliza saaaaana.
Chadema imefanyakazi nzuri ya kuwafichua mafisadi bila uoga lakini pengine hii inaweza ikawa ni sababu ya wao kujiona ni chama pekee cha upinzani.
Chadema wanahitaji kuelewa kwamba ushirikiano wa vyama vya upinzania si jambo la kuchagua bali nila lazima kama kweli wanataka kuiondoa CCM madarakani.
{1}CCM bado ni chama chenye nguvu na kina mtandao mkubwa ulioenea kila kona ya Tanzania.
{2}CCM ina Asset nyingi na vyanzo vingi vya mapato
{3}CCM ina dola
{4}Tume ya uchaguzi ni mali ya CCM

Chadema lazima waelewe si kazi rahisi kuiondoa CCM madarakani bila kuunganisha nguvu ndogo waliyonayo wapinzani.
Lazima ni seme kweli kwamba ushirikiano wa wapinzani una matatizo lakini hatupaswi kukimbia matatizo tunatakiwa kuyatatuwa.

Kama Ushirikiano wenyewe ndio kama ule wa Tarime basi ni akheri kushindana na kushinda bila ushirikiano. Mbona CHADEMA ilishinda bila ushirikiano Tarime? Na hata huko Mbeya wallah inaelekea wangeshinda kama si pingamizi maana CCM tayari ilishagwaya.

Sasa umefika wakati watanzania turuhusu kanuni ya darwin ifanya kazi yake, wenye nguvu watashinda wenyewe.

CUF ina nguvu Zanzibar, itashinda huko hata CHADEMA isipokwenda kuiunga mkono. Likewise, CHADEMA itashinda maeneo ambayo ina nguvu bara hata kama CUF haitaunga mkono. TLP na NCCR are dead parties. Hao wakina PPT na nani sijui ndio tusiwazungumzie kabisa.

CHADEMA waendelee na kazi yao nzuri wanayofanya, CUF nao waendelee na jitihada zao. Haya masuala ya ushirikiano sijui nini ni kupoteza muda wa watanzania tu...wizi mtupu!

Asha
 
Asha
Kama Kimesera alikuwa na nguvu mbona alishindwa.

Alishindwa kidogo sana, unadhani CUF wangesaidia nini kwenda kumuunga mkono kule wakati ambapo hawakubaliki kule? Si wangempunguzia kura tu! Hebu tufikirie nje ya boksi jamani

Kwenda kuungwa mkono na Mbatia na Mrema katika uchaguzi na maneno yao yasiyokuwa serious kunafanya upinzani wote uonekane Ze Original Komedi tu.

Sasa waone huko Mbeya Vijijini, badala ya kuzungumza sera za kumkomboa mtanzania dhidi ya ufisadi wa CCM wao ajenda ni CHADEMA na Mbowe tu hawa ndio unategemea wawashinde wakina Malecela na Nape Nnauye kule. Let us be serious guys...

Asha
 
Nugunungu,
OK, CUF wanyakue hii nafasi wawe chama kitakachokubalika zaidi Tanzania

Sijasema kwa kushinda Mbeya ndio chama kinakuwa bora. Bali, kumbuka kabla ya suala la Mbeya Chadema kilikuwa ndicho chama kinachotajika huku bara na hasa ukizingatia kusuasua kwa CUF kujitangaza zaidi bara.

Kushinda kiti kimoja viwili hakuwezi kukikuza chama. Kumbuka hao CUF wenyewe unaowataja wamewahi kushinda Kigamboni na Bukoba mjini, leo wana nini!

Kilichotokea Mbeya kimewafanya wananchi waamini kuwa Chadema hawakusudii kuimarisha upinzani nchini. Chadema walikuwa bado na nafasi ya kujiweka pazuri mbele ya macho ya wananchi licha ya mgombea wao kuenguliwa lakini walichokifanya hakiwajengi bali kuwabomoa.

Nungu Nungu mzee wa propaganda, wewe usivyoipenda CHADEMA na kuiombea mabaya leo unajifanya kipenzi ukizungumza kwa niaba ya watanzania! Haloo halooooo

Kwa hiyo ulitaka CHADEMA ifanye nini baada ya CUF kutokuwa na mgombea lakini kutaka kuungwa mkono na baadaye CUF kunyakua mgombea alishindwa kura za maoni CCM na kugombea kupitia chama cha CUF? Kwa hiyo ulitaka CHADEMA ifanye nini baada ya mgombea huyo huyo kushirikiana na wa CCM kumwekea pingamizi wa CHADEMA? Ulitaka CHADEMA ifanyeje baada ya unafiki wa CUF, TLP na NCCR Tarime? Ndio maana mi nakumpongeza Dr Slaa kwa kuweka msimamo wazi kuwa ushirikiano wa vyama ulifia Tarime, naona hao wakina Mbowe, Zitto wanazunguka zunguka tu-waseme wazi kabisa nini kwanini hawaungi mkono CUF jamani

Asha
 
Kuna mwenye tape ya mazungumzo ya siri kati ya Mrema, Lyimo na Balille kwa maelekezo ya Rostam ambayo yaliandikwa kidogo na gazeti la Mwanahalisi? Ni vyema undani wa mazungumzo hayo ukatolewa, utasaidia kujua mengi kuhusiana na mwelekeo wa ushirikiano bungeni. Naona ile habari niliyowajulisha siku chache zilizopita kuhusu wasi wasi wa kambi ya upinzani kuvunjika bungeni hatimaye imeandikwa na gazeti la Nipashe. Nitawajulisha kinachofuata, lakini kwa ujumla mafisadi wanachekelea sana

PM
 
Acha historia yenye kupotosha, Nungu Nungu umeibuka sasa ukidhani utaichoma choma CHADEMA kumbe miiba yako imepita pembeni

Kama fikra zako ni kuwa nipo hapa kuichoma Chadema au chama chochote umepotea vibaya sana!

Mimi sio mgeni wa siasa wala JF na katika niliyosema yapo yanayoweza kukisaidia Chama chako. Mimi najua mapungufu mengi ya vyama vya siasa. Ya CCM wala sina haja ya kuyataja kwasababu yapo wazi zaidi.

Kitu unachopaswa kukifahamu huwezi kuishinda CCM kwa kwenda kila mahala nchi nzima. Mtakaa mdanganyane. Labda kwa kukusaidia tu ili uweze kuimarisha upinzani kama vyama vya upinzania alau vingekuwa na mpango mkakati vingejikita zaidi (na kuwekeza nguvu, muda na pesa) kulingana na maeneo vinapokubalika alau kwa kiwango kizuri.
1. Kaskazini - Chadema.
2. Ukanda wa Pwani - CUF.
3. Kanda ya Ziwa, Magharibi na Nyanda za Juu - Kuachiana.
4. Kati - wapinzani wasipoteze sana muda CCM ina nguvu zaidi.

Lakini kama kuna anayejiongopea kwamba chama chake kinaweza kuipiku CCM nchi nzima ndani ya kipindi cha miaka mitano anaota ndoto za mchana.

NN.
 
Kwa mujibu wa Lissu, mkakati wa kwanza ambao kundi hilo la mtandao limeamua kuutumia kuisambaratisha CHADEMA ni kwa kuanza kumpaka matope Mwenyekiti wao, Mbowe, na kumhusisha na kashfa za kila aina ili kumwondolea heshima kubwa aliyojijengea katika jamii kwa muda mrefu sasa.
Nasikia kwa mkakati huu watawatumia hata Ze Komedi kufikisha ujumbe kwa njia ambayo wanajua wadanganyika wataikubali.

Yangu mie macho
 
Leo katika igizo lao vijana machachari wa Orijino Komedi wameaniki unafiki wa Mbowe, Dr Slaa na Zitto wa kuisema CCM kuwa chama cha mafisadi wakati CHADEMA ni chama cha "WIZI MTUPU" wa fedha wanazopata toka nje. Wamesema CHADEMA haina hata gari moja la chama kazi yao kukodi magari na helikopta kuzunguka nchi nzima wakati fedha za kununulia helikopta wamepewa toka nje na kuzila. Wamesema uwizi huo umefanywa na Mbowe na Dr Slaa kwa kumtumia Zitto.

....ndiyohiyo
 
Huo ni upupu wa Orijino Komedi at its best baada ya safari ya kulogwa akili Uingereza. Can they substantiate their claims? Poor guys
 
Back
Top Bottom