CHADEMA yashtuka kampeni chafu
na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetamba kunasa mtandao mpana unaoundwa na kundi la wanasiasa, wakiwamo wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na baadhi kutoka kambi ya upinzani, waliojiunga pamoja kukisambaratisha chama hicho.
Habari ambazo Tanzania Daima imezinasa kutoka ndani ya chama hicho cha upinzani zinaonyesha kwamba, tayari viongozi wakuu wa juu wa chama hicho cha upinzani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wameanza kufanya vikao vya siri wakikutana na watu mbalimbali wa ndani na nje ya chama hicho ili kuweza kukabiliana na mtandao maalumu ulioundwa kwa ajili ya kufanikisha ajenda hiyo.
Kwa mujibu wa habari hizo ambazo zimethibitishwa na mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu, zinaeleza kwamba tayari hatua kadhaa za kisiasa, kiutawala na kisheria zimeshaanza kuchukuliwa ili kudhibiti mpango maalumu wa siri unaoratibiwa na baadhi ya wanasiasa kutoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ndani ya kambi ya upinzani.
Habari zaidi zinaeleza kwamba moja ya sababu ya kuanza kuibuka kwa mkakati huo ni ushindani mkali wa kugombea kiti cha ubunge cha Tarime ambacho kiko wazi baada aliyekuwa akikishikilia, Chacha Wangwe (CHADEMA), kufariki dunia katika ajali ya gari mwishoni mwa mwezi uliopita.
Lissu, mmoja wa wanaharakati maarufu nchini, aliieleza Tanzania Daima jana kwamba, walikuwa wamefanikiwa kupata vielelezo kadhaa ambavyo wanakusudia kuvitumia ili kukabiliana na kishindo cha kundi hilo alilolitita kwa jina moja tu la mtandao, ambalo limejitoa mhanga kukimaliza chama hicho.
Kwa mujibu wa Lissu, mkakati wa kwanza ambao kundi hilo la mtandao limeamua kuutumia kuisambaratisha CHADEMA ni kwa kuanza kumpaka matope Mwenyekiti wao, Mbowe, na kumhusisha na kashfa za kila aina ili kumwondolea heshima kubwa aliyojijengea katika jamii kwa muda mrefu sasa.
Tumeshabaini mkakati mzima wa kutusambaratisha. Utakumbuka hawa jamaa walianza kumchokonoa Mwenyekiti (Mbowe) wakati ule walipomhusisha na deni la NSSF, wakakwama, baada ya hapo wakajaribu kutumia uamuzi wa chama kumsimamisha umakamu mwenyekiti marehemu Wangwe kutuvuruga, wakakwama pia. Sasa wamekuja na mbinu chafu ya kujaribu kukihusisha chama chetu na ajali na hatimaye kifo cha Wangwe, wakitumia hoja dhaifu na za kupikwa, alisema Lissu.
Habari zaidi ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka ndani ya CHADEMA zinaonyesha kwamba, mbali ya mkakati huo wa siri kuhusisha makada maarufu wa CCM, kimebaini pia kuwapo kwa kundi la wanasiasa wachache wanaotoka katika vyama viwili vya siasa vya NCCR-Mageuzi na Tanzania Labour (TLP) (majina na nyadhifa zao tunazo), ambao nao wanatajwa kushirikiana na makada maarufu wa CCM katika kufanikisha mpango wa kuisambaratisha CHADEMA.
Taarifa za maandishi ambazo gazeti hili limeziona zinaeleza kwamba, chama hicho kimeweza kunasa mawasiliano na mazungumzo ya siri ambayo yalifanywa na viongozi wawili wa juu wa TLP na mhariri mmoja mwandamizi hivi karibuni, yaliyopangwa kuchapwa kwa namna ya kupindishwa katika gazeti moja la kila wiki linalotoka kesho Alhamisi.
Tunaweza kusema kwa uhakika kwamba tumenasa mazungumzo kati ya mhariri wa gazeti hilo la kila wiki na viongozi wawili wa juu wa chama cha ....(kinatajwa), yaliyofanyika nyumbani kwa mmoja wa viongozi hao ambayo yalijaribu kuzungumzia madai yanayomhusisha mwenyekiti (Mbowe) na kile kinachoitwa sherehe aliyofanya eti kusherehekea kifo cha Wangwe...suala hili linapaswa kukabidhiwa kwa wanasheria wetu ili walifanyie kazi na ikibidi kuchukua hatua za mara moja za kisheria dhidi ya wahusika hawa, ndivyo linavyosomeka dokezo moja.
Tanzania Daima ilipowasiliana na Mbowe mwenyewe ili kujua iwapo alikuwa anazo taarifa hizo, hakuwa tayari kusema lolote zaidi ya kumweleza mwandishi wa habari hizi: Tumejipanga sawasawa kuwaeleza Watanzania ukweli wote kuhusu mambo haya yote, ili wajue ni kitu gani kinafanyika, ni kina nani wanafanya na malengo yao ni yapi.
Wakati CHADEMA ikikabiliana na tuhuma hizo zinazoelekezwa kwake, chama hicho kimeandika barua kwenda kwa Kituo cha Demokrasia (TCD) kikilalamikia habari zilizoandikwa na baadhi ya magazeti Jumapili iliyopita ambayo yaliandika habari za kumhusisha Mbowe na taarifa za kusherehekea kifo cha Wangwe.
Katika barua hiyo ya juzi Jumanne iliyosainiwa na Anthony Komu, ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya TCD, CHADEMA inaitaka taasisi hiyo kueleza ukweli wa kile kilichotokea nchini Afrika Kusini mara tu baada ya Mbowe kupata taarifa za msiba wa Wangwe.
Pamoja na mambo mengine, CHADEMA imeitaka TCD kuwaita wanasiasa wote waliokuwa katika ziara hiyo iliyoandaliwa na taasisi hiyo kuitwa na kueleza ukweli wa kile kilichotokea na iwapo kulikuwa na ukweli katika maelezo yanayodaiwa kutolewa na kiongozi mmoja wa TLP, Richard Lyimo, anayedaiwa kumwandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) akilalamikia kile anachokieleza kuwa mwenendo wa Mbowe baada ya kupata taarifa za msiba wa Wangwe.
Wakati hayo yote yakitokea, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza nafasi za uchaguzi mdogo na ubunge katika Jimbo la Tarime, iliyoachwa wazi baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Wangwe.
Mbali ya uchaguzi huo, NEC pia imetangaza uchaguzi mdogo wa madiwani katika jimbo hilo, sambamba na chaguzi nyingine ndogo ndogo katika halmashauri na kata 33, katika mikoa mbalimbali nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkurugenzi wa NEC, Rajabu Kiravu, alisema NEC imefikia hatua ya kuandaa uchaguzi mdogo katika Jimbo la Tarime baada ya kupokea taarifa rasmi kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta, kuwa jimbo hilo liko wazi.
Kiravu alisema kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, uchaguzi mdogo wa ubunge unatakiwa ufanyike baada ya siku 20 na isizidi 50 wakati uchaguzi mdogo wa madiwani, isizidi siku 30.
Kutokana na hali hiyo, Kiravu alisema tume imeandaa taratibu za uchaguzi katika Jimbo la Tarime, ambako Septemba 13, utafanyika uteuzi wa wagombea, wakati kampeni zitaanza Septemba 14 hadi Oktoba 11, mwaka huu na uchaguzi utafanyika Oktoba 12.
Akizungumzia chaguzi za kata, Kiravu alisema tume ilipokea taarifa za awamu mbili toka kwa waziri anayeshughulikia serikali za mitaa kuwepo kwa nafasi wazi katika kata 33 nchini.
Kiravu alisema taarifa ya awamu ya kwanza ilihusu kata 23, ambako uchaguzi wake utafanyika Septemba 21 mwaka huu.
Alizitaja halmashauri zitakazohusika katika uchaguzi huo na kata zake katika mabano kuwa ni pamoja na Mpanda (Katuma), Sengerema ( Nyamazugo, Busisi, Bupandwa), Geita (Kagu) Ukerewe (Bukindo) Muleba (Kibanda), Ngara (Kabanga) Bahi (Mundemu), Kigoma ( Nguruka) Urambo (Ushokora) Tabora (Ngambo, Malolo) Maswa ( Ipililo) Mvomero (Langali) Morogoro (Mtombozi) Manyoni (Kintiku) Songea (Wino) Tanga (Chongoleani Ngamiani Kati), Nachingwea ( Naipanga, na Nditi) pamoja na Tandahimba (Mahuta).
Alisema taarifa ya pili iliyohusu kata 10, uchaguzi wake utafanyika Octoba 12. Uchaguzi huo utafanyika Monduli ( Monduli juu na Elisalei) Singida ( Utemini) Serengeti ( Kisangura), Moshi ( Uru Mashariki) Magu ( Sukuma), Ludewa (Lupingu), Arusha ( Sombetini), Ludewa ( Lupingu), Arusha Mjini ( Sombetini), Mbarali (Rujewa) pamoja na Korogwe (Mnyuzi).
Aidha, Tume imetangaza watakaojaza nafasi za viti maalumu kuwa ni pamoja na Bura Venosa Stephano (Hanang), Anna Isikaka Sibajaje, (Mbeya), Neema Issa Nassoro (Arusha), Salima Abdul Mutungi (,Biharamulo), Theresia Peter Mushi (Moshi Mjini), Monica Shello Luvanda (Mufindi).
Wakati huo huo, Kiravu alisema tume imeendelea na zoezi lake la kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura na mpaka sasa mikoa 12, tayari imekamilisha kazi hiyo.
Alisema kwa sasa zoezi hilo linafanyika katika mikoa ya Shinyanga na Mara wakati mikao ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, uboreshaji wake utafanyika Septemba na Oktoba na kabla ya kazi hiyo kuhamia visiwani Zanzibar.