Elections 2010 CHADEMA yashindwa uchaguzi mkuu 2010

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Nini maoni yako ,ikiwa Chadema itashindwa uchaguzi mkuu katika ngazi ya Uraisi ila imepata viti vingi vya ubunge ,uchaguzi ambao unaotarajiwa kufanyika mwisho wa mwezi huu ? :rip:
 
Huu ndiyo mwisho wa CCM Hata hivyo kwa tahadhari na mikakati tu Endapo CHADEMA chama dume kitashindwa mwaka huu itabidi ianze kazi ya kuimarisha mtandao wa chama kuwanzia siku ya kwanza ya bunge. Hapa wabunge wote watapewa kazi ya kuchangia na kufuatilia kazi ya kuimarisha mtandao wa chama hadi kule chini kabisa vijijini. Kitu pekee cha halali kinachoweza kuidhulumu CHADEMA ushindi wake mwaka huu ni kukosekana kwa mtandao wa chama hadi vijijini.
 
That will never happen...........Kwa hiyo siwezi kutoa maoni kwa ndoto za alinacha.................................

DR. SLAA GO......................GO TO IKULU AND CHADEMA WINS MOST SEATS IN THE HOUSEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
 
Mkuu!! kama unaijua vizuri hali ya nchi hii na wapiga kura wake nina shaka isiye kuwa kinyume chake ndio ndoto za alinacha.

Ok...may be ni tactics tu za mapambano ili kutowakatisha tamaa askari walio vitani.
 
Tendwa ataka vyama kukubali matokeo

17th October 2010

JohnT%286%29.jpg

Msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa

Msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa amevitaka vyama vinavyowania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano na Zanzibar kukubali matokeo katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 31.
Akizungumza na Nipashe Jumapili katika mahojiano maalum, Tendwa alisema kitendo cha kukubali matokeo ndio ustaarabu na kuonyesha ukomavu wa kisiasa.
Alisema kwamba hadi sasa kampeni za uchaguzi zinakwenda vizuri Tanzania Bara na Zanzibar, licha ya kujitokeza matukio madogo madogo ya wanachama kupigana.
"Napenda kusema baada ya uchaguzi ni vizuri vyama vya siasa (CHADEMA)vikakubali matokeo kwa sababu ndio ustaarabu na ndio uungwana,"
-----------------------------------------------------________________________________________---------------------------------

Hizi ndio ngoma zinazoanzwa kupigwa ,halafu mnasema never ever....aloo siulizi kwa utani ni lazima mjitayarishe kukubali kushindwa ,ili msije mkapata shindikizo la moyo ,jeshi limeshawekwa standby kuwakabili.
 
kupunguza kujiamini na kukubali critique hata kama si unachotaka kusikia. akikushinda kwa kura hata mkikichafua mtachezea kichapo kama kenya tu.
kujipanga ni muhimu zaaidi kuliko kufikiriafujo witchcraft, kwanza wana hasira nyie mkikichafua kidogo patachafuka kuliko kenya manake bongo uchaguzi kuna na kaudini na ukabila ndani yake
 
Tendwa ataka vyama kukubali matokeo

17th October 2010

JohnT%286%29.jpg

Msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa

Msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa amevitaka vyama vinavyowania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano na Zanzibar kukubali matokeo katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 31.
Akizungumza na Nipashe Jumapili katika mahojiano maalum, Tendwa alisema kitendo cha kukubali matokeo ndio ustaarabu na kuonyesha ukomavu wa kisiasa.
Alisema kwamba hadi sasa kampeni za uchaguzi zinakwenda vizuri Tanzania Bara na Zanzibar, licha ya kujitokeza matukio madogo madogo ya wanachama kupigana.
"Napenda kusema baada ya uchaguzi ni vizuri vyama vya siasa (CHADEMA)vikakubali matokeo kwa sababu ndio ustaarabu na ndio uungwana,"
-----------------------------------------------------________________________________________---------------------------------

Hizi ndio ngoma zinazoanzwa kupigwa ,halafu mnasema never ever....aloo siulizi kwa utani ni lazima mjitayarishe kukubali kushindwa ,ili msije mkapata shindikizo la moyo ,jeshi limeshawekwa standby kuwakabili.

Unajua Mwiba, kauli ya mtu kama Tendwa wala si ya kutilia maanani kwa kuwa Tendwa ni Mwanachama wa CCM na bila aibu amejikuta akijionyesha dhahiri kwamba yeye ni wa CCM na yupo kwa maslahi ya CCM badala ya nchi. Huyu Tendwa hana tofauti na gazeti la habari leo, daily news, TBC na Shimbo. Wamewekwa katika mamlaka kwa maslahi ya taifa lakini bila kujijua wamejikuta watumwa na wanatekeleza matakwa ya familia ya Kikwete na Makamba. Nina imani kwamba CHADEMA watapuuza kauli hii ya Tendwa kwa kuwa ni vuvuzela tu la Kikwete.

Nina imani kubwa kwamba iwapo kutakuwa kuna fair election, hakika Slaa hataona shida kukubali matokeo kwa maslahi ya nchi na kwa ajili ya amani ya nchi yetu. Na iwapo kutakuwa na wizi wa kura kama ambavyo CCM imepanga na imeanza kufanya, basi nawaambieni kwamba si Slaa wala CHADEMA watakaoanzisha fujo, bali ni wananchi hukohuko kwenye vituo vya kupigia kura ndiyo watakaoanzisha fujo. Ninaamini kabisa, katika kila kituo cha kupigia kura, kukitokea hali ya wasiwasi tu, fujo zitaanza immediately bila hata ya Slaa kujua ni nini kinaendelea huko. Ni kama ilivyokuwa kibera kule Kenya ambako watu walianza wenyewe bila ya kuambiwa waanze. Na hata Odinga alipotaka kurudisha nyuma majeshi kwa ajili ya amani ya nchi, wananchi walimjia juu kumtaka aendelee na msimo wake.

Ni vizuri zaidi nyie CCM mkatambua nguvu na mamlaka ya wananchi. Msimwangalie Slaa kama adui yenu katika kuzuia maulaji yenu, bali waangalieni wananchi wanaomfuata Slaa. Slaa hajawahi kwenda kuwapakia wananchi kwenye malori ili waje kwenye mikutano yake, ni wao ndo huwa wanamfuata. Kwahiyo achani hiyo mitizamo yenu finyu ya kuamini kwamba fujo zitaanzisha na Slaa au CHADEMA kama chama.
 
We either win or you lose. Unfortunately there are only two options and you better aclimatize now
 
Tendwa ataka vyama kukubali matokeo

17th October 2010

JohnT%286%29.jpg

Msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa

Msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa amevitaka vyama vinavyowania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano na Zanzibar kukubali matokeo katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 31.
Akizungumza na Nipashe Jumapili katika mahojiano maalum, Tendwa alisema kitendo cha kukubali matokeo ndio ustaarabu na kuonyesha ukomavu wa kisiasa.
Alisema kwamba hadi sasa kampeni za uchaguzi zinakwenda vizuri Tanzania Bara na Zanzibar, licha ya kujitokeza matukio madogo madogo ya wanachama kupigana.
"Napenda kusema baada ya uchaguzi ni vizuri vyama vya siasa (CHADEMA)vikakubali matokeo kwa sababu ndio ustaarabu na ndio uungwana,"

Suala si kukubali matokeo tu. Cha muhimu sana ni kuangalia mchakato mzima. Kama mchakato ni wa huru na haki atakayeshindwa kukubali matokeo atakuwa ni punguani.

Tunataka uchaguzi uwe HURU na HAKI na vyama vikubali matokeo ya uchaguzi wa mazingira hayo.

Kama ukikazania matokeo ukapuuzia mchakato una lako jambo.
 
Back
Top Bottom