Chadema yashinda nafasi ya mwenyekiti wa halmashauri wilaya ya Hai

Nakwambia leo huko ni vikao kwa vikao kutafuta 'aliyesaliti'. Walinipiga Moshi wakachukua uenyekiti sasa upepo umegeuka pambaf zao!! Nilipata kura 22 mgombea wao akapata 23 wakati sisi (pamoja na TLP) tuko 23 na tulishakubaliana na TLP kugawana nafasi ili Halmashauri ibaki upinzani!! Akifa itakuwa hasara kwa upinzani maana huyu mzee ametupiga sana tafu kwa ujinga wake na kuropoka hovyo!!

Hivi Gurudumu umewahi kujiuliza kwamba Dr. Slaa na Makamba wote ni makatibu wakuu??? Unaweza kuwalinganisha??

Watabana lakini wataachia tu, kweli nimeamini makamba anaijenga Chadema

ccm wanapenda kuteua viongozi dhaifu ili kuwatiisha. Hawakutegemea kungekuwepo critical upinzani tz, walizoeana na mke wao wa ndoa wakajisahau.

Washa simu zako za voda nikupigie
 
Hongereni sana Chadema, Arusha pia lazima uchaguzi urudiwe na mwenye haki atashinda tu. Big up CDM
 
CDM hongereni sana, Kwayu chapa kazi tunakujua sekondari nyingi zilizojengwa Hai mkono wako ukiwepo na zinaendelea watoto wetu wanasoma kwa raha zaidi. Mungu akutangulie na akufunike kwa damu yake.
 
Posted on Zitto Kabwe's FB profile:

We have taken Hai District Council today. That makes a 7th Council to be governed by CHADEMA. As i said in Mwanza, we will run these Local Government Authorities as we planned to run the central government so that we show a difference. Hongera Hai, Hongera Rt. Hon. Freeman Mbowe, MP and Party Leader.
 
Butola, nimetoa maelezo yafuatayo kwenye thread nyingine (Mary Chitanda ni Nani);

Kifungu cha sheria hapa chini kinaeleza vizuri kuhusu ujumbe wa baraza la madiwani kwa wabunge wa viti maalumu.

(e) any other member of parliament whose nomination originated from organs of political parties within the area of jurisdiction of the municipal council.

CHADEMA upatikanaji wa viti maalumu hutokea Kamati Kuu ya Taifa ('an organ of a political party). Mamlaka (Jurisdiction) ya kamati Kuu ya Taifa ni nchi nzima. Hivyo basi Kamati Kuu ya Taifa CHADEMA inaweza kumpangia Mbunge wake wa Viti Maalumu Halmashauri yoyote kulingana na mahitaji ya Chama.

Ukisoma kipengele hicho hakuna mahali popote ukazi 'residence' umetumika kama kigezo cha ujumbe wa Halmashauri kwa wabunge wa viti maalumu. Kwa suala la mary Chitanda CCm Mkoa arusha walikuwa wanatumia 'ukazi' kama kigezo!!

Hata kama wewe sio mwanasheria tafadhali kisome hicho kifungu halafu toa tafsiri yako.

Utaratibu wa CCM ni tofauti na wa CHADEMA. Wao CCM wabunge viti maalumu wanapendekezwa (nomination) na organ za chama chao kwenye Mikoa. Organ ya CCM iliyompitisha Mary Chitanda iko Tanga (sina uhakika ni jumuiya ya wanawake au nini) lakini sio organ iliyopo Arusha. Mbunge wa Viti Maalumu wa Arusha kupitia CCM ni Catherine Magige na yupo.

Huyu ametokea Arusha lakini anaishi Dar sasa kama tukitumia tafsiri ya ukazi ilitakiwa awe Dar na sio Arusha.

Tatizo lilipo ni mapungufu ya sheria i.e sheria kushindwa kuwa wazi kuhusu ujumbe. Tafsiri iliyotolewa si sahihi. Kama Mary Chitanda anaingia kwenye Halmashauri ya Arusha kwa sababu ni mkazi wa Arusha basi si sahihi kwa Mh. Grace na Mh. Lucy kuingia Halmashauri ya Hai kwa sababu si wakazi wa Hai.

Huo ni mkanganyiko wa wazi wazi. Ni kutokana na siasa za maridhiano na kuponya madonda sheria inapindishwa haifuatiliwi!!

Utata hu ungemalizwa kirahisi sana na mahakama endapo tu haya mawili yasingekuwepo (without prejudice and with due respect);

1. Upendeleo (imaprtiality) wa mahakama zetu

2. Kucheleweshwa (delay) kwa maamuzi

Ndio maana CHADEMA wakarudi kwenye Nguvu ya Umma kutaka suluhisho.

Kifungu husika cha sheria (kinachofanana na sheria namba 8 ya 1982

43. Decision of questions as to membership of council
(1) All questions arising as to whether a person has been lawfully elected a member or not, or the right of any person to be or remain a member of a district council, shall be determined by a court of a Resident Magistrate upon the application of or election petition presented by, any one or more of the following persons, namely–

(a) a person who lawfully voted or had a right to vote at the election to which the application or election petition relates;

(b) a person claiming to have had a right to be nominated or elected at an election;

(c) a person claiming to have been a candidate at the election;

(d) a person claiming to have a right to be or remain a member of a district council;

(e) the Attorney-General.

Kwa hiyo tatizo ni tafsiri ya sheria na tabia ya watendaji (Attorney General na Mkurugenzi wa Halmashauri) kushindwa kufanya maamuzi sahihi kwa sababu tu wamepokea maelekezo kutoka kwa watu fulani badala yake wanalazimisha mamabo. Kwa nini wasingelipeleka suala hilo mahakamani ili kupatiwa ufumbuzi badala ya kulazimisha uchaguzi? Kulikuwa na haraka gani??

Ni lazima sheria ziheshimiwe na pale ambapo tutaanza kutafsiri sheria ili mradi itusaidie malengo fulani yaliyotokea Arusha yatatokea tena na tena!!


alichoongea Tambwe Hiza ni porojo!!

Mosi;

Mkurugenzi wa Hai alikataa kuwakubali Mh. Grace na Mh. Lucy mpaka juzi ijumaa. Alidai kwamba mpaka apate maelekezo kutoka TAMISEMI hivyo akadharau ushauri wa AG.

Pili;

Sababu za Mh. Grace na Mh. Lucy kwenda Hai ni tofauti na sababu wanazotumia CCM kwa Chitanda. Suala la kuangaliwa ni process ya 'nomination' ya mtu kuwa Mbunge wa Viti maalumu.

natumaini nimeeleza kwa kina, nisikuchoshe ndugu na maelezo marefu!!

Good legal analysis.
 
Hivi umewafanya hao TLP ni mazezeta kiasi hicho wakakubaliana nawe huku wakijua mnawaangalia katika jicho la uadui? Dogo acha unanga kubali kuwa huku imekula kwenu kutokana na hulka zetu za ubinafsi na kudharau wengine.

Halafu pia hii lugha yako inaonyesha nini kilichojificha ndani yako.......

Kilichojificha ndani yangu kiweke wazi kiongozi!!

pia ni vyema ukanikanya mapema kuhusu tabia ya kudharau wengine na ubinafsi! Nipe maelekezo na nitajirekebisha mapema mno lakini unijulishe nimemdharau nani na ubinafsi wangu ni nini!!
 
CHADEMA imeshinda kiti cha Mwenyekiti wa Halmasahuri Wilaya ya Hai. Hatimaye CCM wamesalimu amri baada ya CHADEMA kukinyakua kiti hicho. Wilaya ya Hai ilikuwa ni mojawapo ya maeneo ambayo kulikuwa na mvutano mkubwa wa uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti na baada ya mshikemshike wa Arusha CCM wamesalimu amri kama ilivyokuwa Mwanza! Aluta Continua!!!

Wezi wamefikia ukingo, na lolote wanalotaka kupora umma unamawapo unyo na kipigo.
CCM Kushindwa Umeya Mwanza na Hai ndio kwanza mapambazuko, haki haipotei ng'o, yaweza kucheleweshwa na mafidhuli tu, na hiyo ndiyo nguvu ya umma, na bado nchi inazidi kukombolewa, na hakuna cha kuzuia.
 
Thank you Msando..

Na vipi kuhusu hii kauli ya Tambwe Hizza, unasemaje mkuu?

.......Alisema anasikitishwa na CHADEMA kuhoji uhalali wa Mbunge wake wa viti maalumu, Bi. Mary Chatanda, kuwa mmoja wa wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo wakati sheria ziko wazi kuhusu eneo gani mbunge wa viti maalumu atawakilisha.

"Tarehe 10.12.2010 CHADEMA wenyewe walimwandikia barua Mwanasheria Mkuu wa serikali kuomba ufafanuzi wa kisheria kuhusu wajumbe wa halmashauri kisheria na katika majibu yake kupitia barua yenye kumbukumbu na. JC-A.130-74 ya 16.12.2010 aliwapa ufafanuzi kuwa ni maamuzi ya chama husika kuamua mbunge wake wa viti maalumu atawajibika halmashauri ipi.

"Na hii waliuliza baada ya wao CHADEMA kuamua wabunge wake wawili, Bi. Grace Kiwelu na Bi. Lucy Owenya wawakilishe Halmashauri ya Hai na Mkurugenzi wa Wilaya hiyo kuwakatalia, lakini baada ya ufafanuzi huo wale wabunge waliruhusiwa, sasa wanachohoji ni nini kama si kupotosha tu wananchi kwa makusudi ili wajitafutie umaarufu bure," alisema Bw. Tambwe.

..........................

Haya maelezo ya Tambwe kama ni sahihi, kwanini CHADEMA waendelee kulalamika juu ya Mary Chitanda???????

 
Back
Top Bottom