CHADEMA yashauri kuwe na kodi ya Katiba Mpya ili mchakato wa Katiba uendelee

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
85,392
2,000
Kauli hii ya Kizalendo imetolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mhe. John Mnyika , wakati akiongea na Waandishi wa Habari wa ndani na nje ya nchi kuhusu Umuhimu wa Katiba Mpya kuliko jambo lingine lolote kwa sasa .

Mh Mnyika amesema kwamba ikiwa Serikali yetu haina hela za kugharamia Mchakato huu kutokana na sababu zozote zile basi kwa kupitia CHADEMA Wananchi wako tayari kuchangia pesa taslimu , ambapo AMEIOMBA SERIKALI IANZISHE KODI MAALUM ITAKAYOITWA KODI YA KUCHANGIA KATIBA MPYA , huku akidai kwamba chama chake kiko tayari kuhamasisha Wananchi , ambao nao wameahidi kuwa tayari kuchangia

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
43,433
2,000
Wapi imesemwa kuna mchakato mpya wa katiba?Na serikali haina hela?

Why wanalazimisha kutatua tatizo ambalo halipo?..

Mchakato utakapo anza kama kweli utaanza
Pesa zitakuwepo..

Kama wanataka michango wasisingizie katiba
 
SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
139,495
2,000
Katiba mpya si ipo jamani? Ni kuchukua ile ya Warioba na kuifuta mavumbi tu halafu inapelekwa bungeni kurasmishwa?

Ila JK ni mwanasiasa hatari sana. Mchakato ulikuwa karibia kwisha kabisa halafu kilaghai laghai tu huku akicheka cheka kama ilivyo kawaida yake akabadili gia angani huku mabilioni kadhaa yakiwa tayari yameshateketea.

Wananchi wakielimishwa umuhimu wa hiyo katiba watachanga japo naamini serikali haiwezi kukosa bilioni kadhaa za kusimamia mchakato huu hata kama ikiamua uanze upya. Mtihani mkubwa sana kwa mama !

Na ikishindikana CHADEMA wenyewe wanaweza kujifunga mkanda wakachangisha au kuomba wafadhili wakawasaidia. Wana uzoefu mkubwa wa kuchangisha(na) michango mbalimbali. Kwa hali hiyo mama hatakuwa na kisingizio cho chote.

IMG-20201015-WA0103.jpg
 
zithromax

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
2,105
2,000
Kauli hii ya Kizalendo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chadema Mh John Mnyika , wakati akiongea na waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi kuhusu Umuhimu wa Katiba Mpya kuliko jambo lingine lolote kwa sasa...
Ndo walichobaki nacho ili wasikike ,wew unadhani watafanya mini tena zaidi ya hicho ,halafu kuna mtu wanadhani katiba ndo itawaondolea kila kitu kuna nchi hata hiyo katiba hazina ila wanamaendaleo mazuri tu
 
Kabugula

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,268
2,000
Nashauri Chadema muanzishe pia midaharo yakwanini katiba mpya.

Midaharo hii ifanyike mahali pa wazi kupitia vyombo vya habari.

Pia anzisheni mfuko wa akaunti ili wananchi tuchangie kwa ajili yakulipia chombo cha habari kitakacho kubali kurusha midaharo wa mambo ya chama angalau kila wiki.Chama kijengwe kidigital
 
Nakala kwa John Mnyika
 
Pulchra Animo

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
1,889
2,000
Kauli hii ya Kizalendo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chadema Mh John Mnyika , wakati akiongea na waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi kuhusu Umuhimu wa Katiba Mpya kuliko jambo lingine lolote kwa sasa...

Utter nonsense! Utadhani nchi ina pesa za kuchezea! Wapinzani wanapiga hela ndefu ya posho za ujumbe wa Bunge la Katiba, kisha, mwisho wa siku, wanasusia vikao vya hicho chombo. No way; no need to entertain the selfishness of this bunch of loonies!
 
Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
2,862
2,000
Kauli hii ya Kizalendo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chadema Mh John Mnyika , wakati akiongea na waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi kuhusu Umuhimu wa Katiba Mpya kuliko jambo lingine lolote kwa sasa...
Warioba alishamaliza kazi hiyo Kikwete akaitupa jalalani.

Wakaiokote ileile ipite. Kazi iendelee.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
17,977
2,000
Lini CHADEMA mtapigania masoko ya wakulima, ajira, barabara, maji, afya, ardhi.

Maisha ya watu yakiboreka hata uwezekano wa katiba nzuri utakuwepo maana unyonge na kuyumbishwa na wanasiasa kutapungua.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
85,392
2,000
Lini CHADEMA mtapigania masoko ya wakulima, ajira, barabara, maji, afya, ardhi.

Maisha ya watu yakiboreka hata uwezekano wa katiba nzuri utakuwepo maana unyonge na kuyumbishwa na wanasiasa kutapungua.
Katiba ya Warioba imeweka yote hayo ndani yake , mkuu hakikisha katiba mpya inapatikana
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
29,526
2,000
Kama itakuwa ngumu tuifanyie marekebisho hii hii halafu Mama sitishe Uchaguzi wa awali ili tumpime anavyokubalika
 
goodlif1600

JF-Expert Member
Jun 1, 2016
418
500
Kauli hii ya Kizalendo imetolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mhe. John Mnyika , wakati akiongea na Waandishi wa Habari wa ndani na nje ya nchi kuhusu Umuhimu wa Katiba Mpya kuliko jambo lingine lolote kwa sasa .

Mh Mnyika amesema kwamba ikiwa Serikali yetu haina hela za kugharamia Mchakato huu kutokana na sababu zozote zile basi kwa kupitia CHADEMA Wananchi wako tayari kuchangia pesa taslimu , ambapo AMEIOMBA SERIKALI IANZISHE KODI MAALUM ITAKAYOITWA KODI YA KUCHANGIA KATIBA MPYA , huku akidai kwamba chama chake kiko tayari kuhamasisha Wananchi , ambao nao wameahidi kuwa tayari kuchangia

View attachment 1816688
Chadema sio bado wako busy na sabaya?
 
4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
2,404
2,000
Kauli hii ya Kizalendo imetolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mhe. John Mnyika , wakati akiongea na Waandishi wa Habari wa ndani na nje ya nchi kuhusu Umuhimu wa Katiba Mpya kuliko jambo lingine lolote kwa sasa .

Mh Mnyika amesema kwamba ikiwa Serikali yetu haina hela za kugharamia Mchakato huu kutokana na sababu zozote zile basi kwa kupitia CHADEMA Wananchi wako tayari kuchangia pesa taslimu , ambapo AMEIOMBA SERIKALI IANZISHE KODI MAALUM ITAKAYOITWA KODI YA KUCHANGIA KATIBA MPYA , huku akidai kwamba chama chake kiko tayari kuhamasisha Wananchi , ambao nao wameahidi kuwa tayari kuchangia

View attachment 1816688
Sema Iyo SHATI ya katibu na nembo yake nimeilewa ngoja niitafute iwe ndo pamba yangu ya jmosi,
Vinginevyo naunga mkono hoja za katibu ,katiba,katiba ,katiba , futa kodi ya lain za sim
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom