CHADEMA yasafisha tuhuma za Nape kupitia Channel ten - Kisha wamburuta Kwa Msajili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yasafisha tuhuma za Nape kupitia Channel ten - Kisha wamburuta Kwa Msajili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdutch, Aug 15, 2012.

 1. Mdutch

  Mdutch JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkurugenzi wa fedha na utawala wa CHADEMA Anthony Komu yuko Channel Ten akimchanachana NAPE juu ya tuhuma zake juu ya CHADEMA kupokea fedha kutoka nje na kwamba inafanya usanii katika harambee zake.

  Komu anasema ni kweli CHADEMA inashirikiana na KAS shirikia la kijerumani kama wao CCM wanavyoshirikiana na FES shirika la kijerumani.

  Komu anasema CCM wanapokea fedha kutoka NDI kama wao CHADEMA kupitia TCD lakini mpaka leo hii CCM hawajawahi kutoa mrejesho wa fedha hizo kama wao CHADEMA wanavyofanya.

  Komu ameweka wazi kuwa CHADEMA inapokea ruzuku ya shilingi milioni 230 kwa mwezi. Ameweka wazi pia mapato ya harambee zote za Arusha, Dar es salaam na michango ya Jangwani.

  Kwa maelezo na maendeleo zaidi ya Sakata,


   
 2. Mdutch

  Mdutch JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape kakurupuka kapiga simu anaambiwa ataje majina ya hao wanaotoa fedha chafu CHADEMA akabwabwaja maneno kama kawaida kwa kushindwa kuwataja.

  Mwandishi kamwambia ataje kiasi cha fedha kilichoingia CHADEMA kutoka nje akabwabwaja tena maneno kwa kushindwa kukitaja kiasi chochote.

  NAPE kaulizwa aseme vyanzo vya fedha vya CCM kabwabwaja maneno kwa kushindwa kuvisema vyanzo hivyo. Kashindwa kuwataja hata washirika wao wa CHINA na aliposhindiliwa kuwa na ushirikianao na FES ndio akakubali kishingo upande.
   
 3. KV LONDON

  KV LONDON JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 904
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Nape aje sasa, au awaite waandishi wa habari leo jioni'
   
 4. Richardtemu

  Richardtemu Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: Jun 8, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asubuh hii kwenye chanel ten, Nape amehojiwa akitakiwa kuthibitisha madai yake juu ya chadema kuchangiwa fedha namataifa ya nje. Katika maeleo yake amegoma kutaja watu wanaoichangia Chadema na kiasi cha pesa. Ila amesema kuwa alikuwa anawatahadharisha kuwa hela hela hio sio nzuri kwa maendeleo ya nchi. Amesisitiza kuwa hawezi taja hadharani sasa.

  Pia ametakiwa Kusema wao wamechukua hatua gani maana ishu ya fedha hafu ni kosa kisheria, akasema alikuwa anaitahadharisha tu chadema. Swali ni kuwa, kwanini Nape anataka kucheza na akili zetu wananchi Maana hawezi kutoa madai makubwa namna hiyo hadharani tena kwenye press conference halafu aseme alikuwa anawatahadharisha tuu chadema?
   
 5. Mdutch

  Mdutch JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KOMU kamlima kishoka NAPE kamwambia kama yeye anadhani CHADEMA inapokea fedha chafu kutoka nje basi ni uzembe wa serikali yao dhaifu inayounda serikali yenye mamlaka na BOT inayosimamia benki zote za Tanzania ambamo CHADEMA ina akaunti zake kwa kuitaka itoe hizo taarifa.

  Pia Komu kasema TRA ni chombo cha serikali chenye mamlaka ya kufuatilia vyanzo vya mapato vya CHADEMA na kuvikagua. Kama CCM wanaona kweli kuna fedha chafu zinaingizwa CHADEMA basi Tanzania haina serikali
   
 6. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Ukiwa 'smart' uko smart tuu...mjinga hata aje vipi hakusumbui. Kwa sababu mpaka sasa wote Chadema wanaomjibu Nape (CCM) wanaonekana smart, na yeye (Nape) mjinga....and too bad, that is the fact!
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mbona wamekuwa wengi sana wanaomjibu NAPE mmoja wanahofu ya nini?
   
 8. t

  thatha JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hayo aliyosema KOMU ni kauli ya CDM au ya kwakwe? wasije wakaanza kutoana manundu tena. Tusubiri tuone.
   
 9. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Nape (mmoja, unless uniambie alitumwa na CCM kama taasisi) ameshutumu Chadema...taasisi, inayoundwa na watu wengi tu! Na kila mmoja kwenye taasisi (Chadema) kwa wadhifa wake, ana jukumu la kumjibu Nape! Na majibu anayapata kweli...
   
 10. t

  thatha JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mbona unakuwa na haraka Mkuu? NAPE kiboko yao CDM si unaona wanavyotapa tapa , mpaka sasa waliozungumzia kauli ya NAPE wamefikia 3 na wote wanarudia jambo hilo hilo kwa nini? NAPE anasubiri wamalize wote kubwabwaja.
   
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Haya sasa, nawe unajitokeza ni nani tena ndani ya CDM unayejua nyadhifa za kila mmoja ndani ya CDM?
   
 12. Mdutch

  Mdutch JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wachangiaji wamemjia juu bwana mdogo NAPE kwa kumtaka kama moto wa CHADEMA umekuwa mkali kiasi hicho basi na wao wajaribu kuchangisha fedha kutoka kwa wananchi kama wanauwezo huo ili wakijenge chama chao kinachokufa.

  Kijembe kimerushwa kwa NAPE kutoka kwa mchangiaji kuwa ni kwanini CCM waliopokea fedha chafu za EPA, KAGODA na Deep Green mpaka leo wameshindwa kuwachukulia hatua. Fedha hizi zilitumika kuiingiza CCM madarakani mwaka 2005 na 2010.

  Komu kaja juu tena kwa kusema kuwa CCM wana vyanzo vingine vya mapato kwa mfano umiliki wa majengo na viwanja vya michezo ambavyo wamevipora kwa kuwa vilijengwa na umma enzi za chama kimoja lakini mpaka leo hiii hawawezi kuweka wazi mapato yao ukiacha yale ya ruzuku.
   
 13. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwataarifa,nnampata sasa.
   
 14. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nape ni Mtu Mchache sana
   
 15. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #15
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nape naye anaendelea kubwabwaja tena.
   
 16. a

  annalolo JF-Expert Member

  #16
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape ni kawaida yake refer magamba chenge, el, rostam alivyokuwa anajiapiza lazma waondoke mara baadae mwenyewe tena akakanusha so kukurupuka ni kawaida yake
   
 17. c

  chinini Member

  #17
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  kila mmoja atatoa hesabu ya maneno yake siku ya hukumu!
   
 18. Mdutch

  Mdutch JF-Expert Member

  #18
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eti NAPE amedai kuwa hajaona maswali ya wachangiaji kwa kuwa ameshatoka nyumbani kwenda ofisini.

  NAPE anarudi tena hewani na kudai kuwa CHADEMA ni dhaifu na haina social base kwa hiyo haihofii CHADEMA. Anajitetea kuwa yeye ni mkweli na ndio maana yuko tayari kukisema hata chama chake.

  Analalamika kuwa wanaosema anaiua CCM wanamuonea kwa kuwa anjaitahidi kukijenga chama chake. Anaambiwa ataje majina ya watu wanaotoa fedha chafu anacheka cheka anapata kigugumizi.

  Anasema kuwa kama CHADEMA wasipochukua hatua za kuweka wazi vyanzo vya fedha zao watachukua hatua anaulizwa ni hatua gani watachukua anashindwa kusema.

  Kauli yake hii ya kuonyesha kuihofia CHADEMA hii hapa kwamba yeye NAPE anafanya hivi kuikosoa CHADEMA kwa kuwa ni chama kinachotaka kuiongoza nchi na CHADEMA wajisafishe ili nchi yetu isije ikatawaliwa na watu dhaifu.
   
 19. fugees

  fugees JF-Expert Member

  #19
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 2,587
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Leo asubuhi nape, katibu mwenezi taifa wa chama cha mapinduzi, Simu nyingi zilizopigwa na kumuona Nape kama mpayukaji tu. Swali aliloulizwa anarukaruka tu.

  Pia ameogopa kuwataja watu ambao wanaichangia CCM kwa fedha chafu ambapo mwanzo amesema yupotayari kuwataja watu hao alipokua akizungumza kwa simu leo asubuhi chanel ten.

  Swali:

  Je, Nape ni mpayukaji ambaye hayajui maneno anayoyazungumza?

  Je, Nape anawaogopa mafisadi ndani ya chama chake?
   
 20. Mdutch

  Mdutch JF-Expert Member

  #20
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Komu ni Mkurugrnzi wa Fedha na Utawala wa CHADEMA . Kwa hiyo kauli yake juu ya hili ni kauli ya CHADEMA
   
Loading...