CHADEMA yapiga kambi jimbo la Nyang'hwale kuisambaratisha CCM

Big up kamanda ! Mfikishie Rogerz ujumbe huu, mavuno ni mengi mno Nkome but hakuna wavunaji, njooni huku tufungue ofsi, mabalozi wa ccm hawapo tena. Mola awa tangulie ktk harakat za ukomboz wa pili wa Taifa letu.

Pamoja sana kamanda na ujumbe utafika na Nkome tutakuja.
 
Kamanda jimbo la msalala la bure kabisa mmeliacha sana maige pale ameishia kuwagawia soda tu wananchi kama alivyofanya kipindi cha krismasi fikeni SEGESE pale mpige mambo na mmpe nguvu yule aliyekuwa mgombea diwani anahangaika peke yake ameibomoa CUF pale na sehemu ya ******* ila jimbo ni kubwa lile
 
Asante kwa ushauri wako kamanda...pia ondoa wasiwasi....mpaka kufikia mwezi december mwaka huu...kila kijiji mkoani Geita kitakuwa kimefikiwa na makamanda...hakuna kulala mpaka kieleweke..
 
Hongereni sana.

Lakini suala la kupokea wanachama kwa mtindo huo si bora na lenye manufaa kwa chama.
Mara zote nasema,ni kheri chama kiwe na wanachama wachache wenye kujua misingi na itikadi za chama vilivyo,kuliko kuwa na wanachama wengi for the sake ya kuwa nao!

Utaratibu huo tukiachie C.C.M. CHA.DE.MA. kiwe na utaratibu wa kuwafunda misingi na itikadi wale wanaotaka kuwa wanachama kabla ya kuwapa uanachama. Hii itakua ni njia ya kuepuka kupata mamluki na wanachama wasio na manufaa endelevu kwa chama.

Vile CHA.DE.MA. kijitahidi katika kuhimiza michango kutoka kwa wanachama. Michango ni muhimu katika kujenga chama na kufanya wanachama wawe na uchungu na chama.
 
Big up kamanda ! Mfikishie Rogerz ujumbe huu, mavuno ni mengi mno Nkome but hakuna wavunaji, njooni huku tufungue ofsi, mabalozi wa ccm hawapo tena. Mola awa tangulie ktk harakat za ukomboz wa pili wa Taifa letu.

Kamanda...wabunge wote vijana kupitia CHADEMA...watakuwepo Nkome tarehe 04 March,2015.Kazi kwenu wana Nkome.
 
Endeleeni hivyo hivyo,mie pia huku jimbo la Bariadi Mashariki naendelea kutoa elimu ya uraia vijiji vya Lugulu,Zanzui,Kabale na Kinamweli,hakuna kulala mpaka kieleweke.
Big up CDM, wakati CUF wakisubiri kushiriki tu kwenye chaguzi na kutoa matusi CDM waendelee kutoa elimu ya uraia, mkuu hapo kwenye bold unanikumbusha enzi zangu za utotoni, namwambia Cheyo ajiandae sana tunakuja kumshika.
 
Hongereni makamanda. Kweli nikisikia na kuona juhudi zenu napata nguvu mpya mwilini mwangu. Naomba makamanda wa kila mkoa na wilaya zake waamke, na wapige kazi. Ukombozi wa Tanzania unahitaji kujitoa, na kujituma. Hii si kazi ya mtu mmoja, bali ya kushirikiana.

Zaidi sana, natamani kila mahali CHADEMA wanapofika, wajaribu kufanya harambee kwa ajili ya kutatua matatizo ya wananchi wa mahalia. Mfano, wakija Mwanza, wafanye harambee wakati wa mkutano wa hadhara ili kujenga daraja la Mabatini, kununua madawati n.k. Huku ndiko kuwaonesha wananchi kuwa Chama kipo pamoja nao katika shida na Raha. Mwananchi achangie chochote alicho nacho. Hata mwenye Tsh. 200 atoe ili matatizo ya wananchi yatatuliwe. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Tanganyika, Mungu ibariki CHADEMA.

"Tanzania bila uonevu, ukandamizaji na dhuluma inawezekana" Timiza wajibu wako.
 
Back
Top Bottom