CHADEMA yapewa saa mbili kuondoa bendera zake kwenye barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City. Polisi yafika kushusha bendera hizo

Besta Mlagila, Mi naona ingefaa kama mkutano umeisha alafu hizo bendeza zikaendelea kuwepo ndio wangepewa hiyo barua kidogo hilo tamko lingeleta mantiki.

Itafika mahali hata zile tunazoona kwenye mahotel makubwa nazo zitapigwa marufuku
 
Zina madhara gani kwa Taifa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wangetakiwa kulipia huwezi ukafika sehemu yoyote tu ukajiwekea vitu tu bila kujua hii sehemu mmiliki ni nani au Taasisi gani. Kila eneo lina milikiwa na serikali au Taasisi binafsi, au Mtu binafsi
Kwaiyo chadema wawe wanafata sheria za nchi, isiwe wanakurupuka tu.

Nakupanga bendera bila utaratibu, Rais alisemaga wamachinga wasibunguziwe wafanye biashara popote pale lakini lazima walipie kitambulisho cha mmachinga elf20,

Sasa wao CHADEMA wanapanga mabendera barabarani je wamekuwa wamachinga?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanatakiwa walipie unajua kama mabango yote unayoyaona barabarani yanalipiwa?
Kuna watu hawana akili kabisa, chadema wanamkutano wao hapo, huo mkutano haudumu hata kwa wiki 2 wanachingaika nao ni nini, wakimaliza watafungu na kuondoka, na chadema wameweka bendera kwenye uzio wa ukumbi wa mkutano sio i kama ni tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic amekiandikia barua chama cha Chadema na kukipa saa mbili kuondoa bendera zake zilizowekwa barabara ya Sam Nujoma karibu na ukumbi wa Mlimani City unakofanyika uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.

Bendera hizo ziliwekwa katika barabara hiyo takribani wiki mbili zilizopita ulipoanza uchaguzi wa mabaraza ya chama hicho. Mkutano mkuu wa chama hicho kuchagua mwenyekiti na makamu mwenyekiti utafanyika kesho Jumatano Desemba 18, 2019.

Katika barua hiyo ya leo Jumanne Desemba 17, 2019 kwenda kwa katibu mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji ambayo Mwananchi imeona, mkurugenzi huyo amesema manispaa ya Ubungo ndio inayoihudumia barabara hiyo inashangazwa kuona bendera za chama hicho zikiwa kwenye bustani.

Dominic amesema bendera zimewekwa kama matangazo kinyume na utaratibu wa kibali.

"Kwa barua hii nakutaarifu kuwa unatakiwa uondoe bendera hizo ndani ya muda wa saa mbili baada ya kupokea barua hii. Agizo hii lisipotekelezeka bendera hizo zitaondolewa kwa utaratibu mwingine," inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Meya wa Ubungo ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, Boniface Jacob alipoulizwa kuhusu agizo hilo la mkurugenzi amesema, “bendera hizo haziondolewi kwa sababu Chadema tuna haki ya kutumia maeneo ya wazi ya umma kama vyama vingine vya siasa kwa mujibu wa sheria.”
****

MWENDELEZO
Polisi wamefika eneo la Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar unapofanyika Mkutano wa CHADEMA na kuagiza bendera za chama hicho zilizowekwa kushushwa

- Awali, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic alikiandikia barua chama hicho kikuu cha Upinzani Nchini kutaka kishushe bendera hizo
 
Kuna makada wengine wa CCM siyo kwamba wanakurupuka bali hawafikirii sawasawa wakati wa kufanya maamuzi.

Mbona bendera za Yanga na Simba zimezagaa kila kona katika manispaa ya ubungo na hatujasikia katazo lolote.

Binafsi nitamuona DED wa ubungo kidume kama atazishusha bendera za Yanga.......za Simba najua ataweza maana ni wahindi wala dengu wale.

Maendeleo hayana vyama!
 
Jo leo kidogo zimekurudi
Kuna makada wengine wa CCM siyo kwamba wanakurupuka bali hawafikirii sawasawa wakati wa kufanya maamuzi.

Mbona bendera za Yanga na Simba zimezagaa kila kona katika manispaa ya ubungo na hatujasikia katazo lolote.

Binafsi nitamuona DED wa ubungo kidume kama atazishusha bendera za Yanga.......za Simba najua ataweza maana ni wahindi wala dengu wale.

Maendeleo hayana vyama!

Jr
 
Tukiwaza nje ya boksi

Mlimani city ni eneo la biashara la kimataifa

Viongozi wa kimataifa wanaenda kupata huduma pale

Je itajenga picha gani?

Kwanini wasingesogea pale mbagala kwa shigongo
 
Hii sio Haki

CHADEMA wana haki sawa na Vyama vingine

Tukitumia nguvu kubwa sana kuidhibiti Chadema kuna athari ya kukipa nguvu kubwa sana Chama cha Mabaki ya Sultan na Wahamiaji wa Kibembe ambacho ni hatare sana kwa Madhumuni ya Kulinda Muungano

Bora kuishi na Chadema kama Chama kikuu cha Upinzani kuliko ACT
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom