CHADEMA yapata pigo Bumbuli, BAVICHA kimya chenu kitawaponza

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Wanachama 200 wakiwamo viongozi wa Chadema katika Kitongoji cha Kwemghogho wilayani hapa wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM .

Akizungumza baada ya kuwapokea wanachama hao jana, mbunge wa Bumbuli, January Makamba alisema uamuzi wao unatokana na CCM kutekeleza ahadi nyingi za maendeleo.

Makamba alisema CCM imefanya mengi hivyo haoni ajabu kuwapokea wanachama kutoka vyama vingine vya siasa.

Alisema chama hicho kina kazi kubwa ya kuleta maendeleo ambayo yanahitaji umoja na mshikamano na siyo migogoro, fitina na majungu.

Makamba alisema moja ya mambo yanayochangia kurudisha nyuma maendeleo ni baadhi ya watu kukaa vijiweni na kurushiana maneno, lakini kwa wana-CCM muda huo sasa haupo.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Kitongoji cha Kwemghogho, Shabani Kahema aliwahamasisha vijana kujiunga na CCM kwa kuwa ilani yake inatekelezeka kwa wakati

Chanzo: Mwananchi
 
Kila jambo na wakati wake.

Siasa ikifanywa muda wote kazi zitafanyika muda gani?

Uchaguzi ukifika si kuna muda wa kampeni huwa unatolewa? Au tatizo ni nini?
Hivi unajua maana ya kampeni?
 
Wanachama 200 wakiwamo viongozi wa Chadema katika Kitongoji cha Kwemghogho wilayani hapa wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM .

Akizungumza baada ya kuwapokea wanachama hao jana, mbunge wa Bumbuli, January Makamba alisema uamuzi wao unatokana na CCM kutekeleza ahadi nyingi za maendeleo.

Makamba alisema CCM imefanya mengi hivyo haoni ajabu kuwapokea wanachama kutoka vyama vingine vya siasa.

Alisema chama hicho kina kazi kubwa ya kuleta maendeleo ambayo yanahitaji umoja na mshikamano na siyo migogoro, fitina na majungu.

Makamba alisema moja ya mambo yanayochangia kurudisha nyuma maendeleo ni baadhi ya watu kukaa vijiweni na kurushiana maneno, lakini kwa wana-CCM muda huo sasa haupo.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Kitongoji cha Kwemghogho, Shabani Kahema aliwahamasisha vijana kujiunga na CCM kwa kuwa ilani yake inatekelezeka kwa wakati

Chanzo: Mwananchi
ccm wamefanya mengi yepi ambayo hata hayatajiki?
 
huyu mbunge aliahidi malori ya kubeba matunda kwenda viwandani hadi leo sifuri.............viwanda vya kusindika matunda hadi leo hadith za alinacha....................ndiyo maana anaishia kudai ccm imefanya mengi lakini hathubutu kuyataja kwa sababu hayapo
 
Hivi mmepinga mikutano halafu mnasema kila mtu afanye siasa kwake mnategemea nini?
wabunge wameruhusiwa kutembelea wapiga kura wao.kinachokataliwa,Mnyika kutoka kibamba kwenda kuhutubia Geita,tabu yote ya nini
 
Siku zote hakuna anayerudi CCM kwa hiari yake, Pesa lazima ihusike.

Wamekula 'ten ten' hao.
 
Back
Top Bottom