CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jijini Mwanza kimemteua Diwani wa Nyakato, Josephat Manyerere, kuwa mgombea wa umeya wa jiji hilo, huku nafasi ya unaibu ikichukuliwa na Charles Machinchibera wa Mahina.
Uteuzi huo ulifanyika juzi baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya wilaya mbili za Nyamagana na Ilemela, chini ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.
Chama hicho pia kimefanikiwa kupata madiwani wanne wa viti maalumu jijini hapa, ambao ni Neema Mafuma na Pendo Mboya kutoka Nyamagana, wakati Ilemela madiwani walioteuliwa kwenye viti maalumu ni Lucy Kambulwa na Gladness Kiwia.
Kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilipata madiwani watatu wa viti maalumu na kufikisha idadi ya madiwani 12 huku CHADEMA ikiwa na madiwani 15.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kikao cha uteuzi, Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza, Wilson Mushumbusi, alisema wagombea wa umeya na unaibu waliteuliwa na chama baada ya kukidhi vigezo vinavyotakiwa.
Waliokuwa wakiomba kuteuliwa kugombea nafasi hiyo ya umeya wa Jiji la Mwanza, ambao pia wameachwa katika uteuzi huo ni Chagulani Adams na Henry Matata.
Vigezo vilivyotumika ni uzoefu katika usimamizi wa taasisi, uongozi wa chama au vyama, uadilifu na uaminifu katika kusimamia mali za umma, uelewa wa sera na ilani ya chama hicho na umri katika chama.
Akizungumzia mchakato wa uundaji wa Jiji la Mwanza, Dk. Slaa alitoa angalizo kuwa ni lazima wananchi watumikiwe kwa masilahi ya umma na si mtu binafsi.