chadema yapania kusambaratisha ziara za ccm

Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
4,995
2,527
Katibu mkuu wa CCM Bwana Kinana ameanza ziara kutembelea mikoa yote ya Tanzania kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.

Kutokana na ungwaji mkono na wananchi wa rika zote, CHADEMA kwa makusudi kabisa wamekuwa wanawazomea mawaziri hasa wakati wanapokuwa wanawaeleza wananchi utekelezaji wa ilani ya chama tawala cha CCM.

Nawaomba CHADEMA waache mara moja kutumia mbinu chafu ambazo zinakidhalalisha chama chenyewe na viongozi wote wa CHADEMA
 
Una uhakika na hayo uliyoandika? Sidhani kama ni CHADEMA wanaozomea Kinana na CCM yenu, bila shaka ni watanzania ambao wamchoka na ufisadi na wizi wa raslimali zao ambao CCM mnawafayia.
 
Wewe ni M-pipo's power hata kwa maandishi tu %80 yanajionesha yenyewe. ha ha ha haeeee em em. so funny
 
another silly chap, tatizo ccm hamtaki kuukubali ukweli na kubadilika badala yake mnatafuta scapegoats, endeleeni kuamini kuwa CHADEMA ndio wanaowazomea,mtaumbuka
 
Kwani chama cha upinzani kipo kimoja tu Tanzania nzima?
Hebu badilikeni na muwe waelewa wana ccm.
Mnapenda kukicngizia sana CHADEMA kwa kila jambo,
kisa tu mmeona kwamba kinaleta upinzani mkubwa kuliko chama kingine chochote.
 
Ivi CDM bado kipo mi najua kilijifia baada ya kushindwa uchaguzi wa madiwani
 
Zomeazomea hizi hazina mahusiano yoyotete na Chama cha Siasa; Kumbuka zomeazomea iliyomkumba Waziri Mkuu PM. PINDA Mwanza. Unafikiri KINANA au mawaziri hao wanao umaarufu kuliko PM?.

Zomea Zomea hizo kwa CCM na serikali yake pasitafutwe mchawi kwani hiyo ni true reflection of what is going on ktk uelewa wa watanzania. Hawatazomewa iwapo tu wataweza kutimiza yale wanayoyasema, kwani imekuwa ni Utamaduni kwa CCM na serikari yake kustrategise kwenye makaratsi na mikutano lakini uhalisia ni HAKUNA lolote. Kama CCM watatenda kadri ya wasemavyo basi Watanzania ni wasitaarabu na kusomewa hakutakuwepo.

La msingi ni kwa CCM na seriakali yake Kufanya utafiti huru waweze kujua ni wapi wamejikwaa badala ya kung'ang'ana na sehemu ilipoanguka kwenye madhaifu. Wanaowazomea hao Mawaziri si wana CHADEMA tu bali hata wana CCM wenyewe kwani nao ni sehemu ya jamii inayokipata cha moto ( maisha magumu, na kutoona future yao na familia zao) . Ukiona watu wazima wanakuzomea kama Bongo zako zinacheza vizuri ( timamu) basi unabidi ujiulize kulikoni tatizo nini?, Jitafakari na kujitadhimini, nasiyo itakuwia vigumu kama kingozi kufikisha ujumbe unaoupeleka kwa jamii .

Zomeazomea hazitakoma hadi CCM na serikali yake itakapo kuwa tayari kutenda sawa sawa na maneno inayoyahubiri kwenye majukwaa na makongamano. Naona kama kuna mawaziri wawili au watatu wanaoweza kusimama kwenye majukwaa ya kisiasa kwa uapande wa serikali ya CCM wakasikizwa na wasizomewe. Ni utamaduni mpya na pia sio usitaarabu kuzomewa kiongozi, lakini basi badala ya wanachi kuangua vilio au kupiga mayowe,wawaonapo viongozi hao wameona Zomea zomea waongo ndio njia sahihi kwa kufikisha ujumbe kwa watu wasiokuwa wasikivu wenye kujali matumbo yao na familia zao.
 
Katibu mkuu wa CCM Bwana Kinana ameanza ziara kutembelea mikoa yote ya Tanzania kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.Kutokana na ungwaji mkono na wananchi wa rika zote ,cdm kwa makusudi kabisa wamekuwa wanawazomea mawaziri hasa wakati wanapokuwa wanawaeleza wananchi utekelezaji wa ilani ya chama tawala cha ccm.Tunawaomba cdm waache mara moja kutumia mbinu chafu ambazo zinakidhalalisha chama chenyewe na viongozi wote wa cdm

pole kijana mwenzetu.,kwa kulisaliti taifa.kwa kupewa ubwabwa pale lumumba kwa nowyee!
 
WAKUU!

Mimi siamini kwamba Watanzania tumekuwa wajinga na vipofu kiasi cha kutotambua MAENDELEO kama yapo, hadi Kinana azunguke nchi nzima kutuonyesha hayo maendeleo. Ukweli ni kwamba CCM wanajua hakuna walicho kifanya kwa watanzania. Zaidi ni kuasisi ufisadi na kuiangamiza Tanganyika yetu. Na kwa vile UFISADI umekuwa ndiyo sera ya kuu. Na kwao UFISADI ni maendeleo.
 
Utasikia eti CDM wamewapa wananchi viloba ili wazomee,sijaona umaana wa ziara hizi wanazofanya CCM kwani matatizo ya wananchi wanayajua na hawajawahi kutaka kuyatatua mpaka leo wanakurupuka eti wanaanza kuisimamia serikali,siku zote walikuwa wapi?
 
Ivi CDM bado kipo mi najua kilijifia baada ya kushindwa uchaguzi wa madiwani

jana Le mutuz kaanzoshaamewasifia kwa kupambana kwenye mitandao kwa kujibu mapigo ya chadema, na hizi ndo hoja zenu hongereni vijana, mtumikieni kafiri mpate mradi wenu.
 
Hao si CDM, ni wananchi waliochoshwa na Ufisadi.

Pambaneni na Ufisadi, wananchi wameshawashtukia, vinginevyo hamtaepuka zome zomea ya wananchi
 
Zomeazomea hizi hazina mahusiano yoyotete na Chama cha Siasa; Kumbuka zomeazomea iliyomkumba Waziri Mkuu PM. PINDA Mwanza. Unafikiri KINANA au mawaziri hao wanao umaarufu kuliko PM?.

Zomea Zomea hizo kwa CCM na serikali yake pasitafutwe mchawi kwani hiyo ni true reflection of what is going on ktk uelewa wa watanzania. Hawatazomewa iwapo tu wataweza kutimiza yale wanayoyasema, kwani imekuwa ni Utamaduni kwa CCM na serikari yake kustrategise kwenye makaratsi na mikutano lakini uhalisia ni HAKUNA lolote. Kama CCM watatenda kadri ya wasemavyo basi Watanzania ni wasitaarabu na kusomewa hakutakuwepo.

La msingi ni kwa CCM na seriakali yake Kufanya utafiti huru waweze kujua ni wapi wamejikwaa badala ya kung'ang'ana na sehemu ilipoanguka kwenye madhaifu. Wanaowazomea hao Mawaziri si wana CHADEMA tu bali hata wana CCM wenyewe kwani nao ni sehemu ya jamii inayokipata cha moto ( maisha magumu, na kutoona future yao na familia zao) . Ukiona watu wazima wanakuzomea kama Bongo zako zinacheza vizuri ( timamu) basi unabidi ujiulize kulikoni tatizo nini?, Jitafakari na kujitadhimini, nasiyo itakuwia vigumu kama kingozi kufikisha ujumbe unaoupeleka kwa jamii .

Zomeazomea hazitakoma hadi CCM na serikali yake itakapo kuwa tayari kutenda sawa sawa na maneno inayoyahubiri kwenye majukwaa na makongamano. Naona kama kuna mawaziri wawili au watatu wanaoweza kusimama kwenye majukwaa ya kisiasa kwa uapande wa serikali ya CCM wakasikizwa na wasizomewe. Ni utamaduni mpya na pia sio usitaarabu kuzomewa kiongozi, lakini basi badala ya wanachi kuangua vilio au kupiga mayowe,wawaonapo viongozi hao wameona Zomea zomea waongo ndio njia sahihi kwa kufikisha ujumbe kwa watu wasiokuwa wasikivu wenye kujali matumbo yao na familia zao.

Nimekugongea like ,umemaliza kila kitu .
 
Katibu mkuu wa CCM Bwana Kinana ameanza ziara kutembelea mikoa yote ya Tanzania kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.

Kutokana na ungwaji mkono na wananchi wa rika zote, CHADEMA kwa makusudi kabisa wamekuwa wanawazomea mawaziri hasa wakati wanapokuwa wanawaeleza wananchi utekelezaji wa ilani ya chama tawala cha CCM.

Nawaomba CHADEMA waache mara moja kutumia mbinu chafu ambazo zinakidhalalisha chama chenyewe na viongozi wote wa CHADEMA
Kwa hiyo nyie hamna wanachama! mnaalika wafuasi wa CDM kueleza mauongo yenu! kuzomewa ni lazima! labda mtulipe wali na nyamapori kwa kuwasikilizia uchafu wenu!!
 
Kama ni chadema wanahusika na zomeazomea hiyo kwani nyinyi ccm hamna wafuasi wa kushangilia ili kufuta hiyo zomeazomea ya chadema
 
Mkuu wafuasi wa ccm wanazidiwa kete na wafuasi wa cdm ambayo huwa na nguvu ya ziada inayotokana na unywaji wa viroba
 
Back
Top Bottom