CHADEMA yamtelekeza mbunge aliyemvua hijabu mkuu wa wilaya(hii ndo chadema zaidi ya huijuavyo)

Nimetoa majibu hayo ili ujifunze kuwa njia za muongo ni fupi na sikutaka kusema mengine maana ningekuweka kwenye wakati mgumu hata kurudi hapa jamvini.

Mkuu Mpaka Kieleweke,

Naomba rekebisha bandiko la majibu yako, maana ulivyoyaweka ndani ya quote ya mtoa tuhuma, kuna wengine wanaweza wasiyaone. Ama weke quote za kila kipengele au tumia rangi. Hiyo ni kwa manufaa ya wanaotaka kufahamu ukweli wa sakata hilo.
 
Wacha tu wamwache ndio atakoma kuvua hijabu akina mama..suzan udini tu unamsumbua..lol
 
Baada ya kufuatuatilia hii thread kwa mara ya kwanza nimefikia uamuzi wa kuingia moja kwa moja kama mchangiaji ktk JF.

Jambo nililoliona kutoka kwa mleta hoja ni kuwa ana lengo la kutaka jamii ielewe kinachoendelea ndani ya CDM, ingawa nisilolijua ni kwa nia na madhumuni gani, kama ni yakizalendo ama ya kiitkadi na kwa manufaa ya nani ukweli anaujua yeye zaidi. Ila nina hakika yakuwa huyu bwana mkubwa si msemaji, kwa vyovyote vile, wa mh kwani hilo amelithibitisha yeye wenyewe aliposema kuwa kama kunilaumiwa basi alaumiwe kwa umbea. Nakuwa amemnukuhu mh alipokuwa anazungumza na katibu wa mkoa kabla ya kikao kwa malengo ya kuleta hili hoja kwa jamii kupitia JF tarehe 11.12.2011 ikiwa ni siku takribani nne(4) tangu siku ya tukio lenyewe, tarehe 07.12.2011 na inavyoonyesha tarehe 07.12.2011 mleta hoja alijiunga na JF ila hakuipost hii hijo siku hiyo, ingawa naamini alijiunga baada ya tukio maana alimnukuhu mh saa nne(4) asubuhi. Kama yeye ni mwanachama wa CDM ama mwadishi wa habari wa kujitegemea au mkereketwa anafahamu yeye zaidi. Ila vitu ambavyo ni dhahiri zaidi ni kwamba;

1. Jamaa amemsikia mh akiongea na katibu wa mkoa, ila hiyo haitoshi kuthibitisha nukuhu kuwa ni sahihi, na nidhahili kuhusu swala la Lema ni hoja binafsi ya mleta hoja na amepata nafasi ya kuitolea, nadhani si vibaya ila anapaswa kusimamia hoja yake kwa uwazi zaidi ili wachangiaji wengine waele nini kinaendelea. Ama kwamba alimnukuhu mh akieleza kuwa chama kimetumia gharama nyingi kwa ajili ya kesi ya Lema? Aeleze wana JF...

2. Mtoa hoja hakufanya juhudi yeyote kuongea na mh kujua mtazomo wake ktk swala zima la ukabila ktk chama, na kama mh anadhani kunaumuhi wa kuliongelea hili suala kwa jamii kwa malengo yeyote yale ya kimsingi. Ni hakika mleta hoja alikurupuka akielewa fika mh asingesapoti upupu huu ambao kimsingi hauna faida yeyote kwa jamii ya kitanzania.

3. Na kwasababu kuu hizo mbili kichwa cha habari kinapotosha, sio kwamba ni lazima kiwe na uongo, ila ni hakika kinaupungifu kulingana na hii hoja, vinginevyo ingekuwa vyema kurudi shule ya msingi kujifunza kwa mwalimu wa Kiswahili jinsi ya kuandika vichwa vya habari, kwa maana taarifa yenye upungufu inaleta malumbano, kejeli na kufitiniana.

4. Hoja madhubuti huwasilishwa kwa muda muafaka, chanzo sahii, utimilifu wa taarifa, na yeye mantiki kwa walengwa. Bali kwa kuangalia kwa karibu mazingira ya hoja hii kuna ulakini mkubwa wa kwanini siku nne baada ya tukio ikiwa mleta hoja alikuwa na nafasi ya kufanya hivyo siku ya tukio? Ameileta hoja hii yeye kama nani au inamuhusu vipi? Kichwa cha habari hakiwakilishi kilichopo kwenye hoja, hakuna uthibitisho wa kutosha kujenga hoja ya kuwa mh anamtazamo wa kuwa chama kimemtelekeza. Hoja hii ina mantiki gani ktk vipaumbele vya jamii kwa sasa? Maana alisema alihitaji jamii kulifahamu ukabila ulio ndani ya CDM, je, kwa usahii gani wa hoja iliyotolewa ili kuwawezesha jamii iweze kuitegemea ktk kufanya maamuzi?

5. Fitina, chuki na majungu haziwezi kamwe kuikomboa jamii ya kitanzania, anayepandiliza vitu vya namna hiyo hakika yake haitamfaidia kitu mwisho ya siku wala mtu mwingine yeyote. Ni vema na faida kumbwa sote mmoja mmoja na kwa pamoja tukafanya jitihada zetu zote ktk kuhakikisha tanzania yenye amani idumuyo, uhuru wa kweli, umoja, upendo, pamoja na maendele ya kijamii na kiuchumi.

FANYA SEHEMU YAKO- PLAY YOUR PART, PERIOD.
 
mkuu angalia hapo kwenye red. hivi leo ni tarehe ngapi?
mkuu inavyoonekana hauko makini kama uko makini unataka kupotosha watu,kitu cha msingi changia mada na sio kutafuta makosa yasiyo ya msingi juu ya mada,acha mambo ya ubabaishaji,angalia tarehe aliyoitaja hapo juu ni tarehe 7 na siyo 17.
 
mwongo utamjua tu!anaota huyu!anataka kutwambia kuwa yeye ni msemaji wa huyu mbunge. Si kuna taratibu za chama za kufanywa na mbunge ili apate haki yake!
Kwani habari zote mnazozipost huwa mnazitoa kwa wasemaji husika? au wasemaji wa wabunge?
 
Nimetoa majibu hayo ili ujifunze kuwa njia za muongo ni fupi na sikutaka kusema mengine maana ningekuweka kwenye wakati mgumu hata kurudi hapa jamvini.
JE je unafahamu kuwa upande wa walalamikaji ulishamaliza kutoa ushahidi? hao akina lissu hayo maswali watamuuliza nani? pi a nimemtaja mbunge wa masw magh ili na nyinyi mshiriki kukubaliana na mimi ktk hoja yangu ya msingi
 
Nawaachia wafuatao watoe comments maana ndio wanapenda threads zenye mawazo majitaka kama haya;
  1. Ritz
  2. Njiwa
  3. Faizafoxy
  4. Rejao
  5. Malaria sugu
  6. Korosho nk
Neno langu moja....karibu JF ila kajifunze namna ya kuongea hapa kwenye JUKWAA la watu makini...stori za facebook na Twitter huko huko....
tunaangalia nguvu ya hoja na sio kutumia nguvu kuitoa hoja.wanachadema msikurupuke bila kuchunguza ukweli wa hoja kwani ni kweli kuwa chadema ina matatizo makubwa sana kuliko hata ninyi wanachama mnavyoyafaamu. waliopo jikoni wanajua ninachokiongelea.
 
mkuu inavyoonekana hauko makini kama uko makini unataka kupotosha watu,kitu cha msingi changia mada na sio kutafuta makosa yasiyo ya msingi juu ya mada,acha mambo ya ubabaishaji,angalia tarehe aliyoitaja hapo juu ni tarehe 7 na siyo 17.
Mtoa mada inawezekana alirekebisha tarehe baada ya wenzake kumkosoa. Hukuona kuwa taarifa hiyo imekuwa "edited"? Wewe huwa hujui hilo kwamba marekebisho yanayofanyika katika taarifa ya awali inawefanya wachangiaji wengine wanaofuata kupoteza mwelekeo?
 
Back
Top Bottom