CHADEMA yamtelekeza mbunge aliyemvua hijabu mkuu wa wilaya(hii ndo chadema zaidi ya huijuavyo)

nimesikitishwa sana na ubaguzi uliopo ndani ya chadema,hivi karibuni ktk harakati za chadema kuhakikisha kuwa wanashinda uchaguzi igunga, mbunge wa viti maalumu na wenzake walimdharilisha kwa kumvua hijabu mkuu wa wilaya igunga kwa kuhisi alikuwa anapigia kampeni ccm.mbunge huyo susan kiwanga amefikishwa mahakamani na wenzake kwa kosa hilo, mbunge huyo alikuwa akilalamika hayo muda mfupi kabla ya kuanza semina ya viongozi wa cdm tarehe 7/12/2011 mjini morogoro ktk ukumbi wa BZ hotel, namnukuu "nimetoka tabora kwenye kesi hivyo sikupata haya mafunzo, kesi yenyewe chama kimeniachia mwenyewe.. na hata wakili anayenitetea ni wa kujitolea na ni mzee sana hivyo huwa muda mrefu huwa anasinzia mahakamani kwa hiyo mambo ni magumu kwangu kwa upande wa kesi, unajua sisi wabunge ambao hatutoki kaskazini hatuthaminiwi kabisa ndani ya chama japokuwa mimi nilijitolea kuzunguka nchi nzima ktk kampeni za urais na slaa" . hata hivyo kuonyesha kukata tamaa kwa mbunge huyo hata alivyoingia ndani ya ukumbi wakati wa kujitambulisha alisema "huwezi kuwa kiongozi bila kufungwa" susan aliponda sana mfumo wa chama kuwajali hasa wabunge wa kichaga kama lema, kiwia ambaye ndiye alikuwa mkufunzi siku hiyo.

....................................
 
Hawa Magwanda kila habari mbaya inayowahusu huwa wanaipinga tu. Yaani wanashangaza sana! Nyie mnataka msifiwe tu kila siku. Nyie kina nani? Tabia gani hii mnayoionyesha humu? Angalieni mambo yenu! Mkikosolewa mkubali na mjue kuwa anayekosoa naye hukosolewa kama ambavyo nyinyi mnavyowakosoa Magamba.
 
Tatizo la waongo huwa sahaulifu sana na hawana umakini, hiyo tar 17/12/2011 walifanyia mkutano ndotoni au sayari ingine ambayo tarehe zao ziko mbele ya dunia?

Hata kama unaongea cha ukweli unaonyesha kama umetumwa tu wewe

Kwani wewe hiyo 17/12/2011 umeisoma wapi? Taarifa ya wali inasomeka 7/12/2011. Huyo aliyesema ni 17/12/2011 anapima umakini wenu!!!
 
Mwambie akitunga uongo awe makini na taarifa zake. Tarehe 17/12/2011?


Kweli nimeamini wapenzi wa CDM kiboko mnachakachua hadi tarehe. Kwenye post jamaa kaandika tarehe 7/12/2011 nyinyi mnajifanya amuoni mnaandika tarehe 17 kweli Tanzania kila kitu kinawezekana una mquote mtu na kuongeza namba yako dah sijui tumelogwa?
 
Kweli nimeamini wapenzi wa CDM kiboko mnachakachua hadi tarehe. Kwenye post jamaa kaandika tarehe 7/12/2011 nyinyi mnajifanya amuoni mnaandika tarehe 17 kweli Tanzania kila kitu kinawezekana una mquote mtu na kuongeza namba yako dah sijui tumelogwa?

Aliandika tarehe 17,fuatilia post za mwanzo utaelewa,ameedit ndo mana inaonekana hivyo ilivyo.
 
Ha ha haaaaa!JF inanifurahisha sana,yaani vyama vyote visemwe lakini siyo MAGWANDA duh!Jamani MAGWANDA siyo miungu wanakosea pia,na mnachokifanya mnakosea maana hamuwakosoi bali mnaunga mkono tu hata kama ni upupu!Malalamiko ya kupendelea wakaskazini hata role model wangu marehemu CHACHA WANGWE alishawahi kukaliliwa akiyatoa,kama kweli yapo ni kuwakanya wabadilike siyo kuendelea kukumbatia matatizo.Kuna wabunge wa MAGWANDA walitudanganya kuwa wanashindwa kukataa sitting-allowance kwakuwa wanawekewa kwa lazima ktk account zao mpaka Mhe.Zitto alipokuja kukata mzizi wa fitina kuwa ni mpaka usign kwanza.Jamani MAGWANDA ni chama kinachoonyesha muelekeo ambao wengi tunautaka hivyo tukubalikukinyoosha panapoonekana kunatatizo siyo kutetea kila kitu tu! Huo ni mtazamo wangu tu wadau msijenge chuki!!
 
mmmmmmmh yawezekana ni kalenda ya freemason maana tulisikia tetesi za kuizindua hivi punde
 
Ndugu,Kama uliweza kuhudhiria Kongamano lile maana yake u mwanachama wa CHADEMA.Na Kama ni mwanachama wa CHADEMA unayonafasi yankuyapeleka haya mahali panapostahili Na sio hapa kwa kuwa tuhuma hizi ni nzito kwa chama hasa Kama kweli kimesemwa Na Mbunge mwenzangu wa CHADEMA.Kuanza kukishambulia chama kwa kusikia habari zaupande mmoja sio sahihi.Andika and then tuma kwa Ofisi za Chama Makao Makuu kwa utekelezaji wa ulichokisema,si kila jambo ni la kuandika JF.
Nadhani nimeeleweka Kamanda!



=mpunumpunyenye;2962063]SIAJKURUPUKA
habari hii nimeithibitisha mimi mwenyewe, siku hiyo ya tarehe 7 majira ya saa 4 asubuhi tukiwa mimi, mbunge huyo susan,katibu wa chadema mkoa wa morogoro ambaye alikuwa diwani wa zamani wa matombo bwana luanda na malalamiko haya alikuwa akimweleza diwani huyo nje ya ukumbi wa bz hotel wakati tukiwasubiria wakufunzi wa semina hiyo kutoka dsm ambaye alikuwa katibu wa vijana mkoa wa dsm na mbunge wa ilemela bw kiwia, na alisisitiza kuwa "TUNDU LISU HANA MUDA WA KUCHEZEA KAENDA ZAKE ULAYA" . (kama kuhukumiwa nihukumiwe kwa kosa la umbea)
[/QUOTE]

Naona haina haja ya kuuliza tena source!! Naona kila kitu kipo wazi
 
Kweli nimeamini wapenzi wa CDM kiboko mnachakachua hadi tarehe. Kwenye post jamaa kaandika tarehe 7/12/2011 nyinyi mnajifanya amuoni mnaandika tarehe 17 kweli Tanzania kila kitu kinawezekana una mquote mtu na kuongeza namba yako dah sijui tumelogwa?

Tatizo lako umedandia Gari kwa mbele,hivyo huwezi kujua kilichokuwa kimepostiwa mwanzo,acha kukurupuka wewe.
 
Nitajisikia raha pale mbunge mmoja tu wa magwanda atawekwa ndani. kwa uropokaji, udhalilishaji, upayukaji na uhaini.
 
Aliandika tarehe 17,fuatilia post za mwanzo utaelewa,ameedit ndo mana inaonekana hivyo ilivyo.

Mkuu inaonekana alifanya kosa la kiuandishi tu na akarekebisha lakini inaonekana kwamba alichosema kina ukweli ndani yake. Angalia alichokisema Regia hapo juu utajua kuwa analalamika baada ya jamaa kumwaga mchele kwenye kuku wengi!!
 
Mleta mada ni muongo kabisa, huyu anataka kupotosha watu tu. Nimefuatilia jambo hili kwa mkurugenzi halmashauri na bunge cdm amenihakikishia chama kipo bega kwa bega na Mh. Susan na kamwe hakitamuacha.

Mpuuzeni huyu mtumwa wa magamba na mada yake mfu.
 
hbr yako ningeinunua ila kwenye tarehe ndio imeshushd thamani!hv mzee mabere marando hafai kwenda mahakamani kwa kuwa amezeeka?ukimuona nyani amezeeka jua kakwepa mikuki mingi
 
Back
Top Bottom