CHADEMA yamtelekeza mbunge aliyemvua hijabu mkuu wa wilaya(hii ndo chadema zaidi ya huijuavyo)

Mpunumpunyenye

Senior Member
Dec 7, 2011
114
50
nimesikitishwa sana na ubaguzi uliopo ndani ya chadema,hivi karibuni ktk harakati za chadema kuhakikisha kuwa wanashinda uchaguzi igunga, mbunge wa viti maalumu na wenzake walimdharilisha kwa kumvua hijabu mkuu wa wilaya igunga kwa kuhisi alikuwa anapigia kampeni ccm.

mbunge huyo susan kiwanga amefikishwa mahakamani na wenzake kwa kosa hilo, mbunge huyo alikuwa akilalamika hayo muda mfupi kabla ya kuanza semina ya viongozi wa cdm tarehe 7/12/2011 mjini morogoro ktk ukumbi wa BZ hotel, namnukuu "nimetoka tabora kwenye kesi hivyo sikupata haya mafunzo, kesi yenyewe chama kimeniachia mwenyewe.. na hata wakili anayenitetea ni wa kujitolea na ni mzee sana hivyo huwa muda mrefu huwa anasinzia mahakamani kwa hiyo mambo ni magumu kwangu kwa upande wa kesi, unajua sisi wabunge ambao hatutoki kaskazini hatuthaminiwi kabisa ndani ya chama japokuwa mimi nilijitolea kuzunguka nchi nzima ktk kampeni za urais na slaa" .

hata hivyo kuonyesha kukata tamaa kwa mbunge huyo hata alivyoingia ndani ya ukumbi wakati wa kujitambulisha alisema "huwezi kuwa kiongozi bila kufungwa" susan aliponda sana mfumo wa chama kuwajali hasa wabunge wa kichaga kama lema, kiwia ambaye ndiye alikuwa mkufunzi siku hiyo.
 
Habari kama hi ni ya kuchangiwa na akina Rejao, FAizaFox na wengine wenye hulka ya kiitikadi. Hakuna uthibitisho wa kauli yako kwa ulichokileta hapa.
 
mkuu tupe source ili tupate authority ya kucoment. mimi nataka tu uthibitishe kama kweli alisema kuwa wabunge wa kasikazini ndio wanathaminiwa ndani ya CDM; hilo tu basi. sitajali kwamba hii ni post yako ya kwanza ama tatu au mia mbili kwani hata mbuyu ulianza kama mchicha
 
Tupatie picha za na video za huyo mbunge wakati anatoa hizo comments.
 
nimesikitishwa sana na ubaguzi uliopo ndani ya chadema,hivi karibuni ktk harakati za chadema kuhakikisha kuwa wanashinda uchaguzi igunga, mbunge wa viti maalumu na wenzake walimdharilisha kwa kumvua hijabu mkuu wa wilaya igunga kwa kuhisi alikuwa anapigia kampeni ccm.mbunge huyo susan kiwanga amefikishwa mahakamani na wenzake kwa kosa hilo, mbunge huyo alikuwa akilalamika hayo muda mfupi kabla ya kuanza semina ya viongozi wa cdm tarehe 17/12/2011 mjini morogoro ktk ukumbi wa BZ hotel, namnukuu "nimetoka tabora kwenye kesi hivyo sikupata haya mafunzo, kesi yenyewe chama kimeniachia mwenyewe.. na hata wakili anayenitetea ni wa kujitolea na ni mzee sana hivyo huwa muda mrefu huwa anasinzia mahakamani kwa hiyo mambo ni magumu kwangu kwa upande wa kesi, unajua sisi wabunge ambao hatutoki kaskazini hatuthaminiwi kabisa ndani ya chama japokuwa mimi nilijitolea kuzunguka nchi nzima ktk kampeni za urais na slaa" . hata hivyo kuonyesha kukata tamaa kwa mbunge huyo hata alivyoingia ndani ya ukumbi wakati wa kujitambulisha alisema "huwezi kuwa kiongozi bila kufungwa" susan aliponda sana mfumo wa chama kuwajali hasa wabunge wa kichaga kama lema, kiwia ambaye ndiye alikuwa mkufunzi siku hiyo.

Mkuu angalia hapo kwenye red. Hivi leo ni tarehe ngapi?
 
Tatizo la waongo huwa sahaulifu sana na hawana umakini, hiyo tar 17/12/2011 walifanyia mkutano ndotoni au sayari ingine ambayo tarehe zao ziko mbele ya dunia?

Hata kama unaongea cha ukweli unaonyesha kama umetumwa tu wewe
 
mkuu tupe source ili tupate authority ya kucoment. mimi nataka tu uthibitishe kama kweli alisema kuwa wabunge wa kasikazini ndio wanathaminiwa ndani ya CDM; hilo tu basi. sitajali kwamba hii ni post yako ya kwanza ama tatu au mia mbili kwani hata mbuyu ulianza kama mchicha
Kwa vyovyote vile source ni Nape! La, sivyo source ni Malaria Sungu!
 
mkuu tupe source ili tupate authority ya kucoment. mimi nataka tu uthibitishe kama kweli alisema kuwa wabunge wa kasikazini ndio wanathaminiwa ndani ya CDM; hilo tu basi. sitajali kwamba hii ni post yako ya kwanza ama tatu au mia mbili kwani hata mbuyu ulianza kama mchicha

Mwambie akitunga uongo awe makini na taarifa zake. Tarehe 17/12/2011?
 
mkuu tupe source ili tupate authority ya kucoment. mimi nataka tu uthibitishe kama kweli alisema kuwa wabunge wa kasikazini ndio wanathaminiwa ndani ya CDM; hilo tu basi. sitajali kwamba hii ni post yako ya kwanza ama tatu au mia mbili kwani hata mbuyu ulianza kama mchicha

Mbona thread ya Invisible juu ya Shimbo kuiba trillion 3 hukuomba source?
 
Habari kama hi ni ya kuchangiwa na akina Rejao, FAizaFox na wengine wenye hulka ya kiitikadi. Hakuna uthibitisho wa kauli yako kwa ulichokileta hapa.
Siku hizi nikikuta siredi inachangiwa na hawa jamaa huwa sina haja ya kuifuatilia ni kupoteza muda najua mwisho wake ni mipasho kwa kwenda mbele.
 
umetumwa na suzi au? hamu nyingine bwana labda iltaka akina lema waku........england
 
Back
Top Bottom