Chadema yamtambua kikwete?

Kadogoo

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,073
341
Hii picha ya kamati kuu ya chadema imenishtua kidogo baada ya kuona picha ya rais kikwete ikiwa imetundikwa ukutani na chini ya picha hiyo ya rais wamekaa viongozi wa chadema ktk mkutano wao huko dodoma akiwemo mgombea urais wa chadema dr. W. Slaa!!!

nashindwa kuelewa nini tafsiri yake? Ndio chadema wanaanza kumtambua jk taratibu? Naomba ufafanuzi wa hii picha au hiki kikao kilifanyika ktk ukumbi upi?

nauliza kwa nia njema kabisa, matusi na hasira naomba tuache!

angalia hii picha: View attachment 16780
 
Wewe Je? Unamtambua rais mwizi?
 
Jiulize kuwa huo ukumbi ni wa nani kwanza halafu ndo utapata majibu vizuri hapo sio kweye afisi ya chadema mkulu hence huwezi kuamua utundike picha gani hapo aisee fikiria kwanza vitu vingine jamani
 
kaka hiyo ni ofisi ya bunge......so hawana ujanja, ni kama atavyokuja kufungua bunge lazima wawepo....
 
jiulize kuwa huo ukumbi ni wa nani kwanza halafu ndo utapata majibu vizuri hapo sio kweye afisi ya chadema mkulu hence huwezi kuamua utundike picha gani hapo aisee fikiria kwanza vitu vingine jamani

si ndio maana nauliza? Wewe kama unajua huo ukumbi ni wa nani si utuambie basi?
 
hujawahi kukuta picha za JKN, Mwinyi, Mkapa et al? Picha yake inaweza kukaa hata ofisi za Chadema zikiwa na maneno "J.M Kikwete - rais wa awamu ya nne".
 
Picha haiwezi kubadili ukweli zitatundikwa hadi c.h.o.o.n.i but ukweli utabaki pale pale
 
nafikiria kujiondoa jf, maana great thinker uwezi kureta thread za kiudaku kama hizi, nadhani hivi vitu vingine muwe mnampostia eric shigongo, kule kwenye magazeti ya udaku ndiko kunakostahili. Ofisi yoyote ya serikali lazima kuwe na picha ya rais aliyepo madarakani. Swala la wizi wa kura ni swala lingine, kimsingi kwa mujibu wa katiba yeye ndio rais, sababu ameshaapishwa. Period.
 
Hii picha ya kamati kuu ya chadema imenishtua kidogo baada ya kuona picha ya rais kikwete ikiwa imetundikwa ukutani na chini ya picha hiyo ya rais wamekaa viongozi wa chadema ktk mkutano wao huko dodoma akiwemo mgombea urais wa chadema dr. W. Slaa!!!

nashindwa kuelewa nini tafsiri yake? Ndio chadema wanaanza kumtambua jk taratibu? Naomba ufafanuzi wa hii picha au hiki kikao kilifanyika ktk ukumbi upi?

nauliza kwa nia njema kabisa, matusi na hasira naomba tuache!

angalia hii picha: View attachment 16780

Hilo jengo wanalofanyia kikao ni la nani?
 
Sina shaka kamati hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa hotel fulani. Hizo sio ofisi za Chadema, sasa kama mwenye jengo ameweka picha ya Kikwete waiondoe? Akili ya ajabu kabisa. Wewe ngojea matamko na sio picha.
 
Back
Top Bottom