Chadema yamgeukia Wassira; Ni kuhusu kuwa Chadema kinaweza kufutwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yamgeukia Wassira; Ni kuhusu kuwa Chadema kinaweza kufutwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 2, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  JUMAPILI, SEPTEMBA 02, 2012 07:49 NA EVANS MAGEGE

  *Ni kuhusu kuwa Chadema kinaweza kufutwa
  *Yasema anajenga uhasama kuliko uhusiano
  *Yasisitiza hQakitakubali kufutwa, kitachukua hatua
  *Wassira asema tamko lake halikulenaga Chadema

  MWENYEKITI wa Baraza la Taifa la Vijana la Chama cha Demokrasi na Maendeleo (BAVICHA), John Heche amesema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uratibu na Uhusiano, Steven Wassira kuwa ni kiongozi anayejenga uhasama zaidi kuliko uhusiano.
  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Heche alisema Wassira alinukuliwa na vyombo vya habari hivi karibuni wilayani Bunda akitoa kauli ya vitisho ya kutaka CHADEMA kifutwe.

  Alisema kutokana na kauli hiyo wanachama wa chama hicho kamwe hatawakubali kurudi nyuma na watachukua hatua kali zaidi kama kweli kuna mpango wa kufutwa.

  "Hizi ni dalili za kuweweseka…namshangaa mzee Wassira na ukongwe wake wa siasa kutoa kauli kama hii, hakika nawaambieni CHADEMA haitarudi nyuma na vitisho vyake.

  "Nina uhakika kauli ya Wassira haina uwezo wa kukifungia chama chetu…tutachukua hatua zote za kujilinda, hiki ni chama kikuu cha upinzani. Maneno haya yanaonyesha wazi waziri huyu amenaza kuweweseka kwa sababu anatambua tunataka kushika dola.

  "Mzee Wassira, kama hataki kustaafu vizuri na kwa amani, basi asubiri tu mwaka 2015 vijana wa CHADEMA tunakuja kumstaafisha," alisema Heche.

  Alisema pamoja chama hicho kuendelea kubanwa na vyombo vya dola kamwe hakitarudi nyuma kutetea haki za wananchi.

  Akizungumza na Mtanzania Jumapili kwa simu jana, Waziri Wassira alikanusha kuwa anataka Chadema ifutwe.

  Wassira alisema alichofanya ni kuwa alikuwa akijibu swali la wananchi waliohoji mwenendo wa Chadema na mstakabali wa amani ya nchi.

  Alisema yeye aliwajibu kuwa ikiwa Chama kinakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa kwa kuhatarisha amani hakina budi kifutwe.

  "Namshangaa sana huyo Heche … kwanza ni kijana mdogo anatakiwa ajue siasa ni kama mchezo wa mpira wa miguu lazima awepo msimamizi(referee).

  "Kwa hiyo ukifanya madhambi unapewa onyo kwa kadi ya njano na ukizidisha inabidi ulimwe kadi nyekundu na huu ni ukweli kwa chama chochote kikionekana kwenda kinyume na sheria ya vyama vya siasa.

  "Kwa hiyo mimi sikulenga moja kwa moja kuituhumu Chadema ifutwe ila nilikuwa najaribu kuwaelimisha wananchi walioniuliza swali hilo na ukweli juu Sheria ya Vyama vya Siasa," alisema Wassira.

  Wakati huohuo, Heche akizungumia msimamo wa chama chake juu ya kutokuwa na imani na tume iliyoundwa kuchunguza mauaji ya kijana Ally Zona yaliyotokea mkoani Morogoro, Heche alisema kamwe hakitakubaliana nayo.
  Alisema kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi wa mwili wa marehemu Zona, chanzo cha kifo chake ni jeraha lililotokana na kupigwa na kitu kilichokuwa katika mwendo wa kupaa (risasi au bomu la machozi).

  MIKUTANO
  Katika hatua nyingine, CHADEMA kinatarajiwa kuanza kuutikisa mkoa wa Iringa leo, kitakapofanya uzinduzi wa mikutano ya hadhara ikiwa ni mfululizo wa Oparesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).

  Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika Wilaya ya Mfindi, baada ya kusimamishwa kwa siku tano na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema kupisha kazi ya Sensa ya Watu na Makazi ambayo imemalizika jana.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa jana, Kamanda wa Operesheni hiyo, Benson Kigaila alisema mikutano hiyo itafanywa katika Jimbo la Mufindi Kusini katika kata 15 za jimbo hilo.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Hivi kila MTU ndani ya CCM ana NGUVU ya UPOLISI, MAHAKAMA, UWAZIRI ? Sababu Nape alipokuwa KIGOMA alifutia wananchi KODI ya Nyanya na Vitumbua

  Sasa huyu Waziri anataka kuwa anaweza kukifungia CHADEMA; CHADEMA huu ndio wakati wa kuomba International Observers... HADI katibu kata wa CCM

  Naona Ana NGUVU zaidi ya Vyama PINZANI
   
 3. S

  SHEMGUNGA JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 653
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  peoooopleees! hik kizee kinazeeka vibaya sura yenyewe duu kama anakula ndimu kwiiiikwiii
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Labda anafikiri yupo na wale ndugu zake wanaopenda matunda wa kule Kigoma anawakemea
   
 5. t

  tenende JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Huyu amesema kile kilichomo ndani ya mikakati ya chama cha mabwepande!.. Muziki wa CDM umekuwa mzito hawa wazee wameshindwa kuucheza. Amepima upepo ameona ngoma nzito!.. Kila njia ya kuizuia CDM imegoma. Pipoooooz! ......... P...O....W.....E....R!.
   
 6. BEDO NYALUTOGO

  BEDO NYALUTOGO JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,324
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  2mechoka na hawa wa2 maana badala ya kutafakar naama ya kusaidia watz wanapanga mipang ya kill cdma! hawataweza people.....2015, Akina Wasira Hao Watakufa Bp 2 Mzik We2 Si Mchezo Vjanaaaaaaa!
   
Loading...