CHADEMA yalitikisa Bunge Hotuba ya Lissu yawa ‘mwiba’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yalitikisa Bunge Hotuba ya Lissu yawa ‘mwiba’

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jul 16, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [​IMG][TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lisu

  na Happiness Mtweve, Dodoma


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) sasa wamedhihirisha wazi kuwa kero kwa uongozi wa Bunge.
  Hali hiyo imedhihirika waziwazi juzi baada ya kiti cha Spika kuchukua uamuzi mzito dhidi ya wabunge wawili machachari wa CHADEMA, Tundu Lissu na John Mnyika.
  Juzi kiti cha Spika kilichukua uamuzi mzito dhidi ya hotuba kali ya kambi ya upinzani ya bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria iliyowasilishwa bungeni mjini hapa na mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lisu na kusababisha kiongozi huyo kupelekwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.
  Hatua hiyo ilifikiwa baada ya mnadhimu huyo kukataa kufuta maneno aliyoyaandika na kuyasoma katika hotuba yake ambayo yalikuwa yakieleza kuwa baadhi ya majaji wanaoteuliwa hawana uwezo, hivyo wanashindwa kufanya kazi zao ipasavyo.
  Imedaiwa kuwa maneno hayo ni ya kashfa kwa majaji na serikali kwa ujumla.
  Awali baada ya kumalizika kwa hoja za wabunge waliokuwa wakichangia mjadala wa bajeti ya Sheria na Katiba iliyojadiliwa kwa siku moja na kupitishwa jana. Mwenyekiti wa Bunge, Jenister Muhagama, alimpa nafasi Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, ili kuzungumza kuhusiana na kauli zilizotolewa na kiongozi huyo wa kambi ya upinzani.
  Mwanasheria huyo alieleza kuwa ana wajibu wa kuwaelekeza mawakili popote walipo na hasa walioko bungeni kufuata na kusimamia misingi ya taaluma hiyo bila kuathiri wadhifa wao wa ubunge.
  “Kwa kweli nimefedheheka sana na maneno yaliyotolewa bungeni leo na jambo la kwanza ni maoni ya msemaji mkuu wa kambi ya upinzani kuhusiana na bajeti ya Katiba na Sheria,” alisema Werema.
  Aidha, Werema alitumia nafasi hiyo kumtaka mnadhimu huyo wa kambi ya upinzani kufuta maneno yake hayo ambayo alisema kuwa hayana ukweli wowote kwani majaji wote wanaoteuliwa wana uwezo mkubwa na wanateuliwa kwa kufuata misingi na taratibu husika ambazo zimewekwa za kuwapata majaji.
  “Kauli hiyo ni ya ajabu sana na sikutegemea mtu kama Lisu unaweza kuzungumza kauli kama hiyo na kuwataja watu ambao hawana uwezo wa kuingia humu ndani ya Bunge kujitetea huku ukijua dhahiri kuwa kanuni zetu zinakataza kuwataja watu wa aina hiyo.
  “Mwenyekiti namtaka mbunge afute kauli yake hiyo na vinginevyo kama akikataa basi inabidi apelekwe kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi,” alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  Baada ya Mwanasheria Mkuu kutoa muongozo huu kwa mwenyekiti wa Bunge, shughuli za kupitisha bajeti ya Katiba na Sheria ziliendelea na zilipomalizika mwenyekiti alimtaka afute maneno yake kama alivyoagizwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na baada ya kukataa kufuta mwenyekiti huyo alisema jambo hilo analipeleka kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili liweze kuchukuliwa hatua.
  “Naiagiza kamati hiyo ipitie mwenendo wa shughuli zote kwa siku ya juzi, pamoja na “Hansard’’ na mtiririko wote wa miongozo iliyotolewa na kulishauri Bunge nini lifanye katika hatima ya jambo hilo, kwa kufanya hivyo tutajenga heshima ya Bunge katika kufanya maamuzi na kushughulikia mambo mengine,” alisema Mhagama.
  Mbali na hilo, mwenyekiti huyo alisema kwenye ukurasa wa tisa wa hotuba ya kambi ya upinzani Lissu alitamka kuwa kuna baadhi ya majaji ambao waliteuliwa na rais hawana uwezo na hawakufanyiwa usaili.
  Mwenyekiti huyo alisema kauli hiyo inaingilia mambo ya mhimili mwingine ambao ni Mahakama, hivyo ni kinyume cha kanuni za Bunge.
  Alisema pia kwa kuondoa maneno hayo kutalinda heshima ya uteuzi wa majaji uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni pamoja na kuwatendea haki majaji hao kwa kutoendelea kuvunja kanuni namba 64 kwa kujadili mwenendo wa majaji hao ndani ya Bunge.
  Baada ya Mhagama kutoa nafasi hiyo Lissu alianza kwa kukilaumu kiti kwa kukiuka kanuni na kudai kuwa wanaotaka kutoa maneno hayo katika hotuba yake hawakuzingatia kanuni.
  “Mwenyekiti kwa heshima kubwa sana nimeshangazwa sana na utaratibu ambao unataka kutumika hapa, kwani haupo katika kanuni za Bunge na haupo mahali popote,” alisema.
  Lisu alisema kama kuna jambo ambalo mtu hakulipenda ama kama amesema kitu ambacho si cha kweli alipaswa kuomba utaratibu kwa mujibu wa kanuni 68 (1) ili akae na anielekeze kama nilichosema kipo kinyume na utaratibu na si vinginevyo.
  Mnadhimu huyo alienda mbali zaidi na kusema kuwa kama alisema uongo utaratibu wa kanuni upo kwenye kanuni ya 63, ambayo inazungumzia kutosema uongo bungeni na hatua za kuchukuliwa dhidi ya mtu huyo na si kutakiwa afute bila kufuata kanuni kama ilivyo hivi sasa.
  “Sasa natakiwa nifute tu bila kufuata kanuni, hapa tutagombana sana na kwa kitendo hicho cha kuniambia nifute bila kiti chako kufuata kanuni ni kuniambia mnataka kukanyaga kanuni za Bunge hili, hivyo mimi sitakuwa tayari,’’ alisema Lissu.
  Kwa upande wa Mnyika, Naibu Spika Job Ndugai alilazimika kuagiza mbunge huyo afikishwe katika kamati hiyo kwa madai ya kutoa tuhuma za uongo dhidi ya Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba akidai kuwa anakabiliwa na tuhuma za EPA.
  Agizo hilo hata hivyo lilipingwa vikali na Mnyika pamoja na kambi ya upinzani, likihoji maamuzi ya kiti hicho juu ya suala hilo.
  Mara kadhaa wabunge wa CHADEMA na wale wa NCCR Mageuzi, wameshambuliwa vikali na wabunge wa CCM, huku ikidhihirika kutetewa kwa nguvu kubwa na kiti cha Spika.
  Mathalani, wabunge wa CCM wamekuwa wakishambulia wale wa upinzani kwa maneno ya kudhalilisha, lakini kiti cha spika kimekuwa mara kadhaa kikifumbia macho, kinyume cha hali inapokuwa hivyo kwa wabunge wa upinzani.
  Itakumbukwa kwamba wakati Mnyika akichukuliwa hatua hiyo, hadi sasa mwongozo wa spika kuhusiana na kauli ya waziri mkuu kulidanganya Bunge, na lile sakata la Zitto dhidi ya Mkulo havijachukuliwa hatua yoyote kwa mwaka sasa.


  Chanzo Tanzania Daima
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. M

  Masantula2012 Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Cheze Lissu weeeeeeeeye?????!! Hivi Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wenyeviti, Spika na Naibu Spika hawazijui kanuni za Bunge wanaloliongoza?? Viva Lissu, "Baeleze" "Baelezeeee" hawa wavivu wa kuperuuuzi kanuni. FREDOM IS COMING SOON. Keep the Star Shining brother!! We are behind you!!:flypig:
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kwa taarifa yako hili la Waziri mkuu kulidanganya bunge ndilo limempokonya Lema Ubunge Arusha, sasa hivi Viongozi wa Bunge wameagizwa wasitake mtu athibitishe kauli yake mpaka pale Spika anapojihakikishia kwamba muhusika atashindwa kusibitisha, hii ni kuipunguzia aibu ambayo Serikali imekuwa ikipata kwa kuwataka wabunge wathibitishe kauli zao. Haya sasa Lema ana uwezo wa kuthibitisha kwamba Pinda ni Muongo kama mimi niwezavyo kuthibitisha kwamba Kikwete ni muongo
   
 4. i

  iseesa JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tundu ni moto wa kuotea mbali. Siku hizi hata mwanasheria mkuu wa serikali "ananusa kwapa za Tundu" kwa kujiandaa kupambana naye bila kuwa na uwezo kwa ku-quote paper za Pa-la-MAGAMBA Kabudi ambapo MAGAMBA wanajificha
   
 5. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kuna watu wasiojua "Political Chess Board" walifikiri Mh. John Mnyika mropokaji "alipochomekea" Chemba kuwa mtuhumiwa wa EPA. Hawakuona dhamira pana ndani ya gia hii ya kuchomekea gari la ccm likiwa kwenye maporomoko. Mwenye akili atang'amua: Lengo la Mh. Mnyika lilikuwa ni kuihusha na kuirejesha hoja ya EPA ambayo ni mwiba kwa ccm na serikali na ilikuwa imezikwa kiaina na kuanza kufifia. Kurudi kwake katika mjadala kwa njia ya ushahidi ambao ungejadiliwa upya Bungeni ingekuwa sawa na kupoza donda bichi kwa kumwagia maji ya mchanganyiko wa pilipili na chumvi. Ili kuepuka kadhia hii, Spika wa ccm kaamua kuitupa kwenye dustbin ya Kamati. Na ndo mwisho wa episode zamu hii
   
 6. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hakuna mwanasheria ambae kwangu nimemdharau,na hata amenifanya nianze kuona alivyoidhalilisha taaluma ya sheria.kama huyu AG.
  Hivi inaingia akilini kweli mwanasheria mzima,kukubali kupitisha sheria ya kuwaruhusu wakuu wa wilaya na mikoa kuingia kwenye kamati za nidhamu za mahakama?Hivi hiyo hapo aliyo mwambia Lissu anaingilia kazi za mhimili mwingine,hiyo sheria waliyopitisha inafanya nini?Hili kwa kweli limeniuma sana,na lilifanywa kwa makusudi na linalenga kuwaumiza mahakimu wote watakao toa maamuzi yanayokwenda kinyume na matakwa ya serikali.sasa hapo"the doctrine of separation of power"inakuaje?
  naungana na Lissukwamba appointment nyingi za majaji ni kimeo.Nakumbuka miaka ya 80's ,ukitajiwa huyu ni jaji unampa full respect.Walikua ni watu wanaoheshimika sana.Na appointments zao hazikua za fujo kama ilivyo sasa.Kila muda majaji wanaapishwa kwa fujo sana.Vetting enzi zile si ya mchezo.Wakati mwingine walikua wanapelekwa hottel, unajaziwa mavinywaji ya kila aina halafu ukiondoka watu wanafanya stock taking kuangalia pia unywaji wako kama ni wa kilevi au la.
  siku hizi kuna fununu hata maji wanakula rushwa,enzi zile ilikua haiwezekani jaji kula rushwa.kuna uwezekano mkubwa wa anachokisema Lissu.Kwani sasa appointments nyingi ziko kisiasa zaidi,na kwa mtizamo wangu,watu wanaangalia/hofia maisha yao saa hizi,na baada ya kuondoka madarakani.Kwa hiyo inabidi wa appoint majaji watakaosimamia maslahi yao.
   
 7. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Hili kuwa Lissu alisema majaji wanateuliwa kwa kutozingatia katiba na pia hawana uwezo wa hata wa kuandika hukumu kwa kiingereza sahihi Spika alitakiwa amwambie Lissu alete ushahidi sio kukimbilia kumuambia afute kauli!Werema naye kuna ukiukwaji mkubwa sana wa katiba na mkanganyiko ambao Lissu aliutaja sasa yeye badala ya kuutolea ufafanuzi wa kisheria anakimbilia kumuambia Lissu afute maneno kwenye hotuba! Tanzania tujihesabu hatuna spika wala AG hakuna hayo ni kama mabox tu!!
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Unaleta gazeti la udaku la chadema, bila kutaja hatua zilizochukuliwa? imetikisa nini sasa hiyo hotuba zaidi ya kuwatukana majaji? angoje kimbembe cha kamati ya maadili.
   
 9. nkyalomkonza

  nkyalomkonza JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 1,165
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nasikia posho yak oya mwezi ilichelewa. kidogo ugome kupost ***** humu. pole sana Mtegemea mwanume mwenzio kuishi mjini.
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  AG mwenyewe kateuliwa kishikaji nae pia hajafanyiwa vetting, wakiendelea kubisha itabidi LISU uwataje kwa majina majaji wote waliochaguliwa bila Vetting kwani hata baadhi ya majaji waadilifu wanakereka na hilo, safi sana Lisu kwa kuwawakilisha majaji waadilifu kufikisha ujumbe.
   
 11. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mi sishangai kwa lisu kusema ivyo, mbona kuna watoto wanachaguliwa kuingia kidato cha kwanza hawajui kusoma wala kuandika? inawezekana kuna watu alisoma nao darasani walikuwa vilaza na sasa ni majaji.cha msingi apewe nafasi yakudhibitisha,nakama majaji wetu wanaviwango vinavyotakiwa mbona wanashindwa kulisaidia taifa lao juu ya mikataba mibovu?
   
 12. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Lissu lazima awalize sana mwaka huu, chezea lisuuuuuuuuuu!
   
 13. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Watajuta kumrudisha Lisu Bungeni baada ya kushinda kesi!!!
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mkikosa hoja mnaanza viroja.
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hana lolote huyo, sheria zenyewe zinampiga chenga, Nakumbuka siku aliyopewa somo la sheria bungeni na mzee wa vijisenti, mpaka mwenye akasema "nakuheshimu sana" akakaa kimya.
   
 16. K

  Kigano JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 349
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbe ile hotuba ilikuwa na matusi ? au sikuelewa vizuri kiswahili ?


   
 17. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  wale akina dada waliotoa ngono ya rushwa wakapewa ujaji vipi? hivi na yule wakili wa akina ridhiwani kikwete aloyce mujahuzi alikuwa vetted kweli na mahakama kabla ya kuwa jaji?
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sasa kuwaambia wanaoteuliwa "hawana uwezo", hayo kikwenu sio matusi? Ndugu yangu hata "kichwa chako" inaweza ikawa ni tusi itategemea na matamshi. Hata "mamako" inaweza ikawa ni tusi inategemea na matamshi. Tusijidai kuwa hatuelewi Kiswahili.

  Ukosefu wa maadili ni ukosefu wa maadili, mtu akifanya zinaa ni zinaa tu haiwezekani isiwe zinaa kwa kuwa eti nafanya na mchumba. Tuwe makini.
   
 19. YEYE

  YEYE JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Una uhakika gani au wewe kazi yako ilikuwa kuwapeleka lodge?
   
 20. D

  Danniair JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  GGGGGGGGGGGGGGoooooooooooooooooooooooooooooooooooooddddddd!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Tukianzia na mwanasheria mkuu na kumalizia DPIPI. Ambao hawawezi kabisa kufungulia mafisadi
  kesi kwa mujibu wa sheria bali huishia kugongana kama mawe ndani ya debe. Kesi kubwa kama Richmond vs
  Tanesco tunashindwa kana kwamba hatuna AG.
   
Loading...