CHADEMA yakaribia kupasuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yakaribia kupasuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Mar 16, 2009.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sakata la Dowans linaendelea kuigawa CHADEMA na sasa inakaribia kupasuka makundi matatu. Lipo kundi linaolotaka mitambo hiyo inunuliwe likiongozwa na Zitto Kabwe. Kundi la pili ni lile lenye msimamo wa kati likiongozwa na Dr Slaa. Kundi la tatu ni lile linalopinga ununuzi wa mitambo hiyo, katika kundi hilo yuko Freeman Mbowe, Tundu Lissu, John Mnyika na John Mrema. Jitihada za haraka zinahitajika kuwatoa toka ICU

  .......ndiyohiyo
   
 2. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Nadhani kutofautiana kimawazo na kimtizamo ni jambo la kawaida na mwisho wa siku watapata msimamo wa pamoja, hili kwa CHADEMA ni jambo lakawaida kwenye siasa, hata kule kwetu huwa inakuwa kama hivi.
   
 3. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Afadhali kule kwetu, wao wakati mwenzao Zitto anaona ile mitambo ni LULU kwa watanzania, Tundu Lissu yeye anasema ni WIZI MTUPU: Mwananchi Read News na huyo Mnyika anasema ni OSAMA: JJ: Richmond, Dowans and Operesheni Safisha Mafisadi . Wana hali mbaya kwa kweli. Hivi hawana vikao?

  ......ndiyohiyo
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kijana,'
  Naona conclusion yako is more a wishful thinking than real. Kweli kuna watu wenye hali mbaya hivi sasa kuliko CCM?
   
 5. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hivi kuna ubaya gani kama viongozi wanatofautiana kimawazo? Tena demokrasia huwa inapata afya pale kunapokuwa na controlled conflicts.

  Kuwa na viongozi ambao wanaitikiana kwa kila jambo ni balaa tupu. Muhimu tu ni kumaliza tofauti zao kwenye vikao na sio kuanza kupiga kelele nje ili sisi Wambeya wa JF na sisi tufaidi.

  Mimi hii habari naona haina mpasuko wowote na badala yake inaonyesha CHADEMA wako tayari kutofautiana na maisha yanaenda mbele. Labda wameanza kupata somo toka kwenye mgogoro na na Wangwe Chacha.
   
 6. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu wangu Jasusi,

  Hivi una kadi ya CHADEMA? Kwi kwi kwi!!!
   
 7. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hakuna ubaya wowote kutofautiana kimawazo. ila msimamo wa Zito unaweza ipeleka chadema pabaya hasa ikizingatiwa dowans ni wizi na huwezi kumkarimia mkosaji mhujumu na fisadi kwa njia yeyote ile. Tukikubaliana na msimamo wa Zito na dr. idrisa maana yake ni kwamba hata ukiibia nchi wananchi wakajua bado unaweza kula fedha yao kwa mgongo wa nyuma.

  Zito anatakiwa kujua kujenga mhimili wa utawala bora na unaofuata sheria uliyojiwekea sio kazi lelemama, hata CCM hawakufika hapo walipo bali kwa watu wavivu wa kufikiri waliona bora liende sasa kila kiongozi kawa fisadi kwa sababu hawakuona mbali.

  Zito zingatia mambo mengi sio faida tu ya kimaisha na kulinda ajira. tunataka kujenga taifa linalofuata sheria ilizojiwekea bila kumbeba mtu.

  Chadema haina makundi wala haita meguka wala hakuna ufa. Ila Zito anaweza kuondoka na Chadema ikaendelea tena vizuri sana aliondoka Dr. walidd kaburu na bado Chadema inadunda .Sio rahisi kusimamia haki hasa ukiwa choka mbaya wakati mafisadi wanapita na kitita inahitaji uzalendo wa kweli wala sio wa majukwaa.

  Tanzania ya leo haihitaji wanasiasa wacharwa. Na tuzingatie kutetea ukweli wala sio mtu kwa umaarufu wake.

  Baada ya Lowasa na Rostam kumkimbiza Mohamed Gire kwa mkataba walioutengeza wa uongo deal lilikuwa kuichukua mitambo ile na wao kuwa dowans na kuiuzia tanesco umeme kama Mwinyi na vijana wake walivyofanya na IPTL. Gire akakimbizwa Rostam akachukua ukanda. Ile mitambo ilinunuliwa GE na ilikuwa imetumika na kufanyiwa Refurb. Ukiwa na akili timamu na kama ni mfanyabiashara huwezi kuinunua ile mitambo katu. haina warranty haina maisha marefu inahitaji service kubwa ya mara kwa mara ambayoitalisbabishia taifa hasara kubwa kabla haijazima.

  Zito kama unataka data zaidi ya hiyo mitumba tuwasiliane nitakupa mpaka waliyoiuza na nini walimshauri Gire kuhusu hiyo mitambo halafu baada ya hapo uendelee kuitetea. Ila kama umekula mlungula usihangaike kwani hakuna utakalo elewa.
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Mar 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kinepi_nepi,
  Mkuu hizi habari ni za tungo na simulizi.. unajua tena Wishes zipo nyingi sana kuhusiana na wapiganaji!..Hakuna kitu....
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwi!kwi!kwi!
  Bado mazee, ila huyu kijana akija na habari zinazoegemea upande mmoja lazime tumweke mstari ulionyooka. Au siyo?
   
 10. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0  Source???
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kweli ndugu yetu habari ndiyo hiyo... You may have good points to stimulate chadema to watch out lakini umeiweka kishabiki sana ewe ndugu yetu

  sio kila msigano kimaono au dira huleta mpasuko... Usipoangalia ndugu yetu utapasuka wewe uiache hiyo chadema

  ushauri wa bure: Fanya uchunguzi wako halafu justify; la sivyo tutapasua kila chama humu jf kwasababu ya tofauti ndogondogo na kuondoa maana ya "great thinkers wa kibongobongo"

  hiyo ndiyo habari sasa
   
 12. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  tofauti ya mtizamo kwenye DOWANS haiwezi kuua chama labda kuwepo na kitu kingine
   
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwanini wapasuane kwa suala ambalo hawana uwezo nalo,Zitto hawezi kuifanya serikali inunuwe huo mtambo, wala hao wengine hawawezi kuzuia isinunuliwe iwapo serikali itaamuwa hivyo, Kwanini wagombane kwani kwenye chama chao hakuna demokrasia? Wajifunze kwa CCM kinaruhusu watu wa namna zote iwe mafisadi, wanaopinga ufisadi hata wanaotuhumiwa wizi.
   
 14. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2009
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii inaweza kuwapa tabu kidogo Chadema, hasa hasa Zitto kama anaweza tena kusimama jukwaani na kukemea ufisadi, CCM wamemtega kategeka, ila kipimo ni Ubunge jimbo la Busanda maana huko nasikia sangara anatafuna kwelikweli, ukali wa menop yake tutayaou within less than 90 dayz
   
 15. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Katika Chama hiki mamluki wa Sultani CCM wamejenga kambi au wamejenga kiota ,hivi vyama vingine haviishi migogoro ,kuna Mbowe ,Slaa na Zitto ambae anaunyemelea uenyekiti wa Chama hicho ,hebu kuweni na msimamo wa kuisakama serikali baada ya kumsakama mtu mmoja mmoja ,yaani kwa mbali utaona Chadema inatumika au inatumiliwa kama switchgear ,wanamtandao wa Sultani CCM wakiamua kuvaliana njuga hutumika switchgear kuwasha tatizo na hapo malumbano huanza kwa ushahidi utaona malumbano yanayoanzishwa na Chadema zaidi hulipuka ndani ya CCM na kuwafanya wawe au waonekane kupambana wenyewe kwa wenyewe huku catalyst Chadema akionekana pembeni kuchochea ,na hatimae hutokea wengine kujiuzulu ukiangalia chanzo ni Doc:xls za serikali kupitia Chadema.
   
 16. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hiyo ni 'point' kabisa!! Angalia enzi za "zidumu fikra za mwenyekiti" Na mambo yanayokikumba chama kwa sasa! Ule unafiki umezaa mafisadi, mpaka shetani anaogopa!
   
 17. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Naona uweke kile kialama cha "Tetesi:"
   
  Last edited: Mar 19, 2009
 18. Kabwela

  Kabwela Member

  #18
  Mar 21, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muheshimiwa kichupichupi, tunaomba umwage mchele hapa uwanjani tuweze kuupata ukweli kuliko kusikia uongo wa kina Ngleja ambao walitumwa kugombea ubunge ili wapewe uwaziri halafu walinde maslahi ya magod father wao.

  Tunakusubiri mkuu
   
 19. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tangu Zitto akubali uteuzi wa Rais kwenye kamati ya kurekebisha mikataba ya madini ndipo alipoanza kuisaliti Chadema,Chadema wanamwangalia tuu wakati anawaangamiza kwa tamaa zake za utajiri.Angalia pia msimamo wake kwenye kifo cha Wangwe,na Dowans na hata kwenye vita ya mafisadi Zitto haeleweki vizuri msimamao wake.Mimi yangu ni kuwatonya Chadema wamdhibiti Zitto kama hataki bora aende CCM tujue moja.
   
 20. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na Lipumba je?

  ......ndiyohiyo
   
Loading...