CHADEMA Yajitoa mchakato wa Katiba; Yadai Rais kawauza!

chadema wametia saini mkataba mbovu na kutuingiza hasara, Mbowe na Dr Slaa wajiuzulu damu mpya ya vijana ichukue nafasi
 
Huyo JK ni msanii tosha lakini CDM nao wangevuta subira kwanza sio kukurupuka kwenda kwenye media na kutoa maneno, kwanza bado wananchi hatufahamu kwa kina makubaliano yaliyofanyika ikulu.
 
Yaani hata mimi siwaelewi, nilitegemea wangevuta subira ili kuona kama serikali itapeleka mapendekezo ya kurekebisha sheria hii katika bunge lijalo. Job true true

kuna mtu kawastua naona,jk si mnajua mtoto wa mjini angewaingiza choo cha stendi kama alivyomfanyia lowassa kwenye ile "ajali" yake ya kisiasa....!wao walikua wanafurahia kugombea vikombe vya chai ya ikulu juzi kumbe mwenzao alikua anawasanifu tu!
 
kuna mtu kawastua naona,jk si mnajua mtoto wa mjini angewaingiza choo cha stendi kama alivyomfanyia lowassa kwenye ile "ajali" yake ya kisiasa....!wao walikua wanafurahia kugombea vikombe vya chai ya ikulu juzi kumbe mwenzao alikua anawasanifu tu!

Na kweli alikua anawasanifu na migwanda gwanda yao.
 
Hawa CHADEMA ni kama hawa hawaeleweki vile au wana lengo la kutusumbua akili zetu na misimamo yao

ALL IN ALL TUNAHITAJI AMANI kama wana susa wasuse tu wengine watakula wapo wengi tu
 
ooh boy!!

LOL. Hapa Chadema waliingia choo cha kike au choo cha stendi? Au ndiyo sababu inashangaza pale mdada anapoingia choo cha kiume kwa speed kali lakini shida inakuwa pale choo hicho kinapokuwa ni cha kusimama. Tabu tupu.
 
kwa makubaliano yale na jk ambayo yalisainiwa na mnyika na nchimbi hakuna hata moja lililosema kuwa rais asisaini muswada kabla ya marekebisho. Ila nakumbuka la kwanza lilikuwa linasema "pamoja na sheria hiyo kupitishwa na bunge ipo haja ya kuendelea kuiboresha ili ikidhi mahitaji ya kujenga kuaminiana na muafaka wa kitaifa". sina hakika kama mlilielewa hili. Yawezekana mlinogewa chai ya ikulu na kushindwa kulitafakari hili kabla ya kulisaini. Kwa maana hiyo kusema kwamba rais kawauza mmeniboa.

wewe hao sio wapwan,,ni watu wa kaskazin watu wa kaz na pesa
 
mnyika naona unaona maoni ya watu wengi hapo juu, hata kitaani ni hivyo hivyo

all i can say to you guys please sticky to your decision, chadema ijulikane ina mlengo gani, mlengo wa kulia, kushoto au kati, amueni kuwa radicals na dunia ijue hivyo...au muwe kondoo na dunia itawajua hivyo. Mmekuwa mnabadilika badilika sana.....

Hata iwe vipi hamtakuwa na uwezo wa kumfurahisha kila mtu.....ila amueni muwe vipi na mtavuta wengine kwa vile mtakavyokuwa!!

Leo mtakasirika, kesho mtamchekea yule yule aliyewakasirisha jana, kitu gani huwa kinatokea??...hatujui

lingine, jamani ikiwezekana hiyo ruzuku ichukue nafasi ya posho zenu za bungeni...susieni vikao vya bunge na dunia ijue hivyo ccm wanajua kuwa huwa mnatisha leo....mnakuja kesho! This aint good not neither for your supporters nor for your members.

hayo ni maoni yako tu,,,,,,
 
Wanatuzuga tu mbona hawasemi wwalichokubaliana na jinsi kutekeleza pia yale ambayo hawakukubaliana na sababu zake labda hili ndilo hawakukubaliana kwa sababu uwezo wa kuingiza marekebisho yao kwa sasa kwenye mswada ni vigumu na wataendelea kuyafanyia kazi taratibu kadri inapo faa

CHA
DEMA walikosea mapema bungeni kitendo cha kutoka nje ya bunge Mawazo yao wangeyawasilisha tuu hata kama ni kwa ukali kiasi gani Wananchi wangejua nini mawazo yao na wanajengaje hoja na kuitetea

Tatizo lao wanaharaka mno wanataka kile wanachotaka kifanyike hata kama hakiwezekani " Lazima kulikubali kosa na uwe tayari kutafuta means nyingine namna ya kulirekebisha " ILA KWA AMANI
 
hapa John Mnyika ulichofanya hakuna tofauti na NAPE NNAUYE, na wewe tumekuona Vuvuzela tu. Kwanini mlienda Ikulu kabla ya kutafakari? Halafu jana mnaitisha press Conferess aibu.
 
Mi nashangaa kweli,mimi toka alipokubali kuonana na chadema,i expected this to happen,you know why he signed?just to show the he has power and authority,i didnt expect anything lovely and creative from this man,
 
Wanatuzuga tu mbona hawasemi wwalichokubaliana na jinsi kutekeleza pia yale ambayo hawakukubaliana na sababu zake labda hili ndilo hawakukubaliana kwa sababu uwezo wa kuingiza marekebisho yao kwa sasa kwenye mswada ni vigumu na wataendelea kuyafanyia kazi taratibu kadri inapo faa

CHA
DEMA walikosea mapema bungeni kitendo cha kutoka nje ya bunge Mawazo yao wangeyawasilisha tuu hata kama ni kwa ukali kiasi gani Wananchi wangejua nini mawazo yao na wanajengaje hoja na kuitetea

Tatizo lao wanaharaka mno wanataka kile wanachotaka kifanyike hata kama hakiwezekani " Lazima kulikubali kosa na uwe tayari kutafuta means nyingine namna ya kulirekebisha " ILA KWA AMANI
Kwenye nyekundu hapo ndiyo pointi, mimi nilikuwa nasubiri sana nondo za CDM, ingawa ni CCM damu, ningependa sana kuona malumbano yao na wabunge wa CCM na CUF, but to my and I think most Tanzanians disappointment..........
 
Hapa ndipo ninapopata taabu na umakini wa Viongozi wa CHADEMA katika issues. Hivi walitegemea JK asalimu amri kwao wakati wao ni maadui wakubwa wa Utawala wake? Ni heri wasingeenda na wangeishia kufanya maandamano na mikutano ambayo ingekijenga zaidi chama na kuwaamsha wananchi kuelekea utoaji maoni sahihi kuhusu Katiba mpya.

Nadhani, wakubali matokeo baada ya kudhalilishwa vilivyo kwenye Mkutano wa "wazee wa CCM" na hata kukiukwa kwa kinachoitwa "makubaliano" na JK.

Bado kuna safari ndefu kufikia Demokrasia ya vyama vingi!
 
Chadema mlipoteza gemu pale mlipoomba kukutana na jk, tangu mwanzo msimamo wenu ulikuwa dhahiri na wa2 waliwaelewa. Lissu kaeleza vizuri tangu pale bungeni kabla ya nyie kutoka nje, ameeleza tena kwenye mdahalo pale starTV wa2 wakamwelewa. Nini kilichowafanya kutaka kumwona rais? Mngebaki na msimamo ule ule wa kususia huo muswada na uhakika 100% watanzania wengi wangekuwa upande wenu. Mmeenda kumwona JK, mazungumzo yameisha na mmesaini makubalino, JK kasaini muswada kuwa sheria, cku 1 tu baada ya mazungumzo, tuelewe nini hapa?...bao mmejipiga wenyewe. Kwa hili mmetukatisha tamaa sana wana cdm na wananchi wa kawaida.
 
Mnyika kwani ulitaka mapendekezo yote lazima Jk ayakubali? kama yalikuwa sita unajuaje labda matano yalibaki kayakubali?

Hivi unajua tukiwa na katiba mbovu itakugusa wewe, watoto wako na wajukuu? Kenya imetuacha mbali sana, maana kuna watu makini hawaangalii masilai yao ya sasa wanafikiria na vizazi vya baadae.
 
They never seem to have plan B before taking plan A.

Nakupa guarantee hawawezi kususa hadi mwisho wa huo mchakato.
Watakuja kubadili maneno tu baadae kuwa hatukuwaelewa kama madai yao ya kutomtambua rais
Jamani toka tulivyoona yale makubaliano na namna CDM walivyokuwa wanatoa maelezo tata kuufafanua while wenzao wa CCM wakiwa kimya tuliwaonya viongozi wetu waitishe kikao haraka cha kamati kuu kujadili reaction ya watu na makosa ya wazi ya makubaliano yale.tamko hili la cdm tulilitarajia lakini tayari ni too late! jk kashinda kirahisi sana,yale makubaliano na zile picha za tabasamu huku rais akiwagawia juice ni turufu kwa serikali na itatumia kuwaonesha taasisi za kimataifa na kuwaambia "hawa ni walalamishi,mbona tumewasikiliza na makubaliano ndio haya hapa na tulielewana vizuri tu kama mnavyoona kwenye picha!" hapa hatuchomoki kwa hizi bla bla na matamko! Wananchi wameshazoea,lazima turudi nyuma tujiulize kabla hatujaangukia pua kabisa! Kumbukeni pia hizi vurumai zinawapa fursa ccm kujipanga na uchaguzi 2015! Muda unakwisha hatujawaandaa wananchi vya kutosha kuelekea kwenye mabadiliko! Kibaya zaidi uchaguzi utafanyika ktk mazingira haya haya hata kama ni katiba mpya! Tunaelekea kushindwa kama hatuoni! Mawazo yangu tu jamani kama mzalendo!
 
Back
Top Bottom