Hebu jibu hili swali Kada Mwenzangu "wangeshiriki unadhani nani angenufaika??"Wapo watu waliojiweka mkao wa kula 2020, kumbuka hata Mzee Lowassa alidandia jahazi na kumpiga kikumbo Dr. Slaa lakini mwisho wa siku haikuwa vile alitaka iwe.
Hebu jibu hili swali Kada Mwenzangu "wangeshiriki unadhani nani angenufaika??"Wapo watu waliojiweka mkao wa kula 2020, kumbuka hata Mzee Lowassa alidandia jahazi na kumpiga kikumbo Dr. Slaa lakini mwisho wa siku haikuwa vile alitaka iwe.
jibu ni wale wote waliotaka kukitumia chama kama jahazi la kuwavusha 2020 na kutwaa ubingwa ambao kiukweli sio wao. kila siku tunasema Chadema ina wenyewe, na wenyewe wameshasoma alama za nyakati kama kuna watu wanataka kukiondoa chama nje ya dhumuni lake la kuanzisha na kukimbia nacho kusikojulikana.
Tunacho kiona sasa, ni chama kujiweka kwenye "sleeping mode", kujirudisha nyuma na kujikosesha nguvu kwa makusudi ili kisiwe kivutio kwa wale wanotala kukitumia kwa manufaa yao. Wimbi la bahari likishapita, basi ni rahisi kujiamsha na kuanza kuendeleza ajenda ya awali au hata ikiwezekana mpya na yenye mvuto zaidi.
Mkuu, ungepeda niseme wananchi, lakini nashindwa kutumia hilo neno. Maana kama wanufaika wangekuwa ni wananchi, wasingetumia uwamuzi ambao sio wa kidemokrasia wa kususa uchaguzi.Hebu jibu hili swali Kada Mwenzangu "wangeshiriki unadhani nani angenufaika??"
Hii inanikumbusha hata 2015 walikataa matokeo na kutokumtambua JPM, matokeo yake wakajikuta hata shughuli zao za kawaida za bungeni na nje ya Bunge zinakwama. Kwenye siasa za vyama vingi huwezi kuikwepa serikali, ni lazima utashirikana nayo utake usitake.Mwananchi wa kawaida ni lazima atoe ushirikiano kwa serikali ya mtaa kwa sababu vinginevyo anaweza kujikwamisha katika kutimiza mambo yake muhimu.
Mabwanyenye ndio aghalabu kutumia Huduma za serikali ya mtaa kwani wenyewe wana consultants na mawakala katika kila jambo hata jumuiya hawasali lakini Kanisani wanakaa viti vya mbele kabisa.
Inawezekana kukawa na uonezi kweli katika maeneo fulani ya uchaguzi lakini kule uswahilini kutotoa ushirikiano kwa serikali yako ya mtaa ni jambo ambalo haliwezekani.
Tusidanganyane
Maendeleo hayana vyama!
Mnalaumu mtu asie na hatia, siku postmortem ikifanywa mtakuja kuona ukweli uko wapi.Msipate shida, Tiss wapo na nyie wapambe mpo, anzisheni chama mnachotaka kama mnaona hivi vyama vibaraka vilivyopo havina mvuto. Lakini wananchi tunajitambua hatuko tayari tena kushiriki siasa na chaguzi za kishenzi.
CHADEMA kama chama kikubwa cha siasa, nategemea wawe na viongozi wao na wanachama huko huko mitaani. Hawa ndio askari wa kutegemewa kuikomboa nchi.
Hao viongozi waliopo makao makuu ya chama na mikoana/wilayani ndio wanaotakiwa kusimamia zoezi la ukombozi kwa kuwa na mipango thabiti ya kuelekeza mapambano sehemu zote nchini.
Ni swala la kuwa na mpangilio mzuri tu wa kazi.
Urojo unaujua au unaongea tu mnya njiani weweEmbu kalale huko na urojo wako
Wa kutoka kuwa 'mifugo' ya watu na kuwa watu wenye haki kamili inayoheshimiwa na wale tunaowaweka kuwa viongozi wetu.Ukombozi wa nini unazungumzia wewe???!!!
Kafunge viatu vya watawala wezi huna lolote la maana.Mrema na Cheyo jee wamevinyanyua vyama vyao?Mbowe ni mwanaCCM damudamu alipandikizwa kufanya mission ya kuipandisha na kuiua CHADEMA amefanikiwa maana Chadema itaenda Makumbusho kama CuF, NCCR MAGEUZI
Kwani hata ikifa wewe nini kinakuwasha?kama mmebaki peke yenu machozi ya nini!au mtakosa buku 7 za bando?