CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,789
11,931
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza chama chake kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa madai wakishiriki wanahalalisha ubatili

Maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni baada ya Wabunge wa CHADEMA kukutana leo alasiri Novemba 7, 2019 katika Kikao cha Kamati Kuu ya dharura ya chama kilichofanyika mkoani Dodoma

Jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema Kamati hiyo itakutana leo kutoa msimamo wao wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

----
WAZIRI JAFO AWASHANGAA
Baada ya Chadema kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa, Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo amesema uamuzi huo unawanyima fursa wagombea wa chama hicho waliopitishwa, waliokata rufaa kupinga kuenguliwa.

“Nimesikia kuwa Chama kimojawapo kimejitoa kwenye Uchaguzi, ninachoweza kusema ni kuwa hawajawatendea haki Wananchi wa chini kwa sababu baadhi yao walishateuliwa na wengine wameshawasilisha malalamiko yao kwenye Kamati za Rufaa na tayari baadhi ya Kamati za Rufaa zimeshaanza kutoa maamuzi juu ya rufaa hizo.

Mtazamo wangu maamuzi hayo yatawanyima haki na kuwadhulumu wananchi wa chini haki yao ya kugombea na kuongoza Serikali za Mitaa ambao baadhi yao wameshateuliwa na wengine wanasubrii rufaa zao”

Mhe. Seleman S. Jafo
Waziiri wa Nchi OR-TAMISEMI
07/11/2019



EIwyPe5WoAI8iRD.jpg

Pia soma
 
Naona mpira umetiwa kwapani saaa

Wengi walitabili hili sasa rasmi CCM imeshinda mapema

Kauli ya mwenyekiti imenukuliwa na vyombo vyote baada ya kikao cha kamati kuu View attachment 1256620
Hongereni sana CHADEMA,Haya ni Maamuzi sahihi ili kuliweka Taifa katika hali ya amani. Mshindani wenu Mkuu dhamira yake imekufa kabisa yupo tayari kwa lolote bila kujali afya ya amani ya Taifa letu. Sasa kunusuru hali hiyo uamuzi huo kwa sasa unahitajika.
 
Back
Top Bottom