CHADEMA yajibu hatua ya Mbunge Cecil Mwambe, kusoma Ilani ya CCM Bungeni

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetetea hatua ya Mbunge wake jimbo la Ndanda Cecil Mwambe kuingia na ilani Ya Chama cha Mapinduzi bungeni kwa kile ilichokisema ni jambo la kawaida.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje CHADEMA, John Mrema amewataka watu wasishangae kwani Chama hicho kinawahamasisha wabunge wake kusoma ilani ya (CCM) ili kujua namna gani ambavyo Chama hicho tawala kinatekeleza ilani ahadi.

"Ni jambo la kawaida sana, sisi kama chama tunawahamasisha wabunge wetu kusoma, ndio maana huyo huyo Mwambe wiki iliyopita ulimuona akimpa sera Mbadala za Chama moja ya mawaziri Bungeni", amesema Mrema.

Aidha, amesema "kuingia na ilani ya Chama cha Mapinduzi si tatizo kwa sababu hata ukija ofisini kwetu utakutana na ilani ya CCM kwa hiyo kama angekuwa na nia ya kuhama chama, angehama kimya kimya kama wanavyofanya wengine".

Leo Novemba 14, 2018 akiongoza vikao vya bunge, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, amesema mheshimiwa Cecil Mwambe anasoma sana ilani ya Chama cha Mapinduzi, siku hizi baada ya kugundua ina mambo mazuri sana.
IMG_20181114_180628_857.jpeg
 
Ni kuweka mambo sawa, au kuondoa sintofahamu..Wewe huoni kuna ambao walisema yuko mbioni kukihama chama chake, ungetaka wakae kimya ili iweje?
Unajua lililoko moyoni mwake..?alitakiwa ye ndio atoe ufafanuzi..sababu hajaagizwa na chama chake kuitumia ilani ya ccm wakati mna vitabu vyenu vya sera mbadala na pale ndio ilikuwa mahali pake kuinadi..muda utasema
 
Kwani aliposema tunawahamasisha wabunge wao kusoma ilani na akasema hata ofisini utakunana nayo..Umelewaje?

Kama hujasoma uzi vizuri ukaelewa tusichoshane mkuu.
Unajua lililoko moyoni mwake..?alitakiwa ye ndio atoe ufafanuzi..sababu hajaagizwa na chama chake kuitumia ilani ya ccm wakati mna vitabu vyenu vya sera mbadala na pale ndio ilikuwa mahali pake kuinadi..muda utasema
 
Kwani aliposema tunawahamasisha wabunge wao kusoma ilani na akasema hata ofisini utakunana nao..Umelewaje?

Kama hujasoma uzi vizuri ukaelewa tusichoshane mkuu.
Muda si mrefu mtaanza kuinamisha sura chini..nyie kwa kuongea hamnaga tofauti na mabinti wa kizaramo.
 
Muda si mrefu mtaanza kuinamisha sura chini..nyie kwa kuongea hamnaga tofauti na mabinti wa kizaramo.
Shipa limekushuka sasa baada ya kukunyoosha..Kumbe ulikuja mbio kuchangia kitu usichokijua, by the way mwanasiasa kuhama Chama si jambo la kushangaza

Nyie uliotoka porini ndo mnatuletea shida mjini hapa
 
Shipa limekushuka sasa baada ya kukunyoosha..Kumbe ulikuja mbio kuchangia kitu usichokijua, by the way mwanasiasa kuhama Chama si jambo la kushangaza

Nyie uliotoka porini ndo mnatuletea shida mjini hapa
Mjini wapi hapo darsalaam?
 
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetetea hatua ya Mbunge wake wa Jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe kuingia na ilani ya Chama Cha Mapinduzi bungeni kwa kile ilichokisema kuwa ni jambo la kawaida.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano wa Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amewataka wananchi na wafuasi wa chama hicho wasishangae kwani chama hicho kinawahamasisha wabunge wake kusoma ilani ya CCM ili kujua namna gani ambavyo chama hicho tawala kinatekeleza Ilani yake.

“Ni jambo la kawaida sana, sababu sisi kama chama tunahamasisha wabunge wetu kusoma, ndio maana huyo huyo Mwambe wiki iliyopita ulimuona anampa sera mbadala za Chama moja ya mawaziri Bungeni,”amesema Mrema

Aidha, amesema kuwa kuingia na ilani ya Chama Cha Mapinduzi sio tatizo kwa sababu hata ofisini kao ukienda utakutana na ilani ya CCM kwa hiyo kama angekuwa na nia ya kuhama chama, basi angehama kimya kimya kama wanavyofanya wengine.

Leo Novemba 14, 2018 akiongoza vikao vya bunge, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa, Cecil Mwambe anasoma sana ilani ya Chama Cha Mapinduzi, siku hizi baada ya kugundua ina mambo mazuri sana.
 
Back
Top Bottom