CHADEMA yajiandaa 'kubutua' uchaguzi wa Kinondoni

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
*Mikutano ya CCM yawapa kiwewe*

*Yawaandaa kisaikolojia wafuasi wao*

Na Mwandishi wetu, Kinondoni

Hali ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yazidi kuwa mbaya viashiria vingi vinaonyesha Chadema kutaka kuharibu uchaguzi jimbo la Kinondoni.

YAWAANDAA KISAIKOLOJIA WAFUASI WAKE

Katika hali inayoonyesha Chadema kuusoma tayari hali ya mchezo ulivyo kuwa wanaenda kushindwa, wameanza kuwaandaa kisaikolojia Wafuasi wao kwenye kuelekea kushindwa.

Chadema wamekuwa wakilalamika kila siku. Mathalani wamelalamika juu ya kubadilishwa vituo, mara kuwalalamikia wasimamizi, mara kulalamika juu ya fomu za viapo, mara kulalamikia vyombo vya dola. Malalamiko yote hayo ni sehemu kuwaandaa kisaikolojia Wafuasi wao pindi watakaposhindwa waonekane wameonewa.

MIKUTANO YA HADHARA

Mikutano ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeendelea kupata wingi wa Watu wengi na huku ya Chadema ikiendelea kuporomoka kwa kasi kwa kukosa mvuto na kupata muitiko mdogo kabisa. Sasa hivi wameitelekeza mikutano ya hadhara na wameenda kufanya siasa majumbani kwa Watu.

WAKIMBILIA VYOMBO VYA HABARI

Chadema wameacha kufanya mikutano ya siasa, badala yake wamekimbilia kwenye vyombo vya habari. Kutwa kazi yao ni kulalamika tu kuwa wanaonewa. Hiyo yote ni mipango ya kuwaandaa kisaikolojia wafuasi wao kuelekea kuharibu uchaguzi Kinondoni.

MVUTO WAWATESA

Kupungua mvuto wa Mgombea wao Ubunge kunazidi kuwatesa kwani siku zinavyozidi kwenda mgombea wa ubunge wa CCM, Ndg. Maulid Mtulia amezidi kujiongezea umaarufu na Watu wengi kujitokeza kwenye mikutano yake.

Pia mvuto wanaoambatana na Salum Mwalim kwenye mikutano ya kampeni imezidi kupungua kutokana na kutokuzungumzia mambo ya Wananchi na kujikita kwenye siasa majitaka zisizo na mashiko wala mvuto kwa wapiga kura.

WATU WA LAWAMA

Katika hali inayoonyesha kutaka kubutua uchaguzi huu ili uharibike, Chadema wamekuwa wakitoa lawama kila kukicha. Walianza kwa kuilaumu Tume ya Uchaguzi (NEC) kubadili vituo, baadae wakamlalamikia msimamizi wa uchaguzi.

MWISHO

Kutokana na kutambua kuwa wanaelekea kushindwa uchaguzi huu wa jimbo la Kinondoni, Chadema wamejiandaa vyema kuharibu uchaguzi huu ili kuepuka aibu kubwa na wafuasi wao kuwakimbia zaidi. Hii ndio sababi kuu ya Chadema kujiandaa kubutua.

Na Angel Stanley
Mwanachama CCJ
Kinondoni.
 
Umelipwa kiasi gani kupotosha umma juu ya thuluma unayoitetea inayofanywa na CCM
 
Wale wahudhuriaji wa mikutano ambao wamekuwa wakizunguka nao tangu mikutano kuanza
 
Back
Top Bottom