CHADEMA yaja na mpango wa kumtoa Lema mahabusu

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Chadema imeamua kuja na mpango mpya wa kuhakikisha Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema anatolewa mahabusu.

Lema amekuwa mahabusu tangu Novemba mwaka jana, lakini chama hicho kimesema sasa kinataka apate haki ya kisheria na kuwa huru kwa kuwatumia wanansheria katika kesi mbalimbali zinazomkabili.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amesema hayo baada ya yeye, mwenyekiti wake, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine kumtembelea Lema mahabusu anakoshikiliwa tangu Novemba 2, mwaka jana kwa tuhuma za kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.

Lema amekuwa akikwama kupata dhamana kutokana na sarakasi za kisheria zilizosababisha upande wa utetezi uende hadi Mahakama Kuu katika kuhakikisha anapata haki hiyo, lakini hadi sasa bado vita hiyo ya kisheria haijaisha.

Lissu amewaambia waandishi wa habari mjini Arusha kwamba wataongeza nguvu ya mawakili wa Chadema katika kesi hiyo kila itakapokuwa ikitajwa mahakamani.

Pia, watakiandikia Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) barua rasmi kukitaka kitoe tamko kwa namna yoyote ili kiseme katika kesi ya Lema kipo upande upi na kama kikisema hakihusiki, basi hakutakuwa na chama cha wanasheria nchini na wakiona kuna hoja, basi watawataka watoe mawakili waliopo Arusha kusaidia kesi zinazomkabili Lema.

“Hawa wanasheria wasijidai hamnazo wakati mbunge wao yupo mahabusu. Tutawaambia wawepo mahakamani kwa kuwa wananchi wa kawaida hawaruhusiwi kuja kusikiliza kesi hiyo, basi wajae wanasheria,” amesema Lissu.

Awali, Mbowe amesema chama na viongozi waliamua kwenda kumuona Lema na familia yake kwa kuwa yupo mahabusu kinyume na haki za binadamu.

“Lema ana moyo mkuu sana na amejifunza mambo mengi kwa mujibu wa maelezo yake. Anasema wapo mahabusu asilimia 70 wenye makosa yanayostahili kupewa dhamana, lakini hawajapewa,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Wanaosemaga maneno ya mdomo yana nguvu kuliko za mkononi.. wana maana kubwa..

Tamko la hiyari yake mwenyewe linamfanya anyee Debe hadi leo..

Ama kweli mdomo uliponza kichwa..
 
Hivi TLS nayo ni jumuiya ya CDM kama ilivyo BAVICHA au LHRC kiasi kwamba washinikizwe kutoa tamko kwenye mambo ya kipumbavu kama hilo?

Kuna issues ngapi za msingi zinahitaji kauli zao leo waanze kuhangaika na wasaka uMandela?

Kibatala si alishapigwa chini hapo TLS?

Wafu wazike wafu wao wasianze kutafuta wachawi.
 
Naona nao walimuacha Lema ajifunze kabla ya kuamua kumsaidia

TLS inashinikizwa na CDM kutoa tamko na kusema Ni batili isipofanya hivyo. Smh

Kumbe wapo wengi wanaokosa dhamana sio Lema peke yake, nilidhani kuna mkono wa JPM kwenye hii kesi kama wengi wanavyodai kumbe sivyo ni mambo ya sheria yenyewe au na hao wengine wamemtishia mtukufu.
 
papaa pipiii trafick jam in the city,najaribu kukunbuka nyimbo flani ya miondoko ya rege
 
Tundu lissu inaonekana anavuta bangi.
Analazimisha chama cha wanasheria kitoe tamko la kuiunga mkono chadema,vinginevyo hakuna chama cha wanasheria!
Taaluma ukishaichanganya na siasa ni tatizo kubwa sana.Wanasheria wanaoelewa wajibu wao huwa hawatoi matamko ya kudhalilisha mahakama hata kama imetoa uamuzi mbovu,wanasheria wanaoelewa wajibu wao hawaongei kama wamevuta bangi,wanapambana kwa kufuata njia za kimahakama.
Taratibu za kukata rufaa zipo,sijui chadema na Lissu kwa nini hawataki kuwaambia wafuasi wao ukweli kuwa mawakili wao wasomi,wanakosea kwa makusudi au kutojua jinsi ya kujaza hati za viapo na kuzingatia muda na utaratibu wa kukata rufaa.
Hata Lema awekewe mawakili 100,kama utaratibu haufuatwi itakuwa ni kazi bure.
 
Chadema imeamua kuja na mpango mpya wa kuhakikisha Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema anatolewa mahabusu.

Lema amekuwa mahabusu tangu Novemba mwaka jana, lakini chama hicho kimesema sasa kinataka apate haki ya kisheria na kuwa huru kwa kuwatumia wanansheria katika kesi mbalimbali zinazomkabili.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amesema hayo baada ya yeye, mwenyekiti wake, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine kumtembelea Lema mahabusu anakoshikiliwa tangu Novemba 2, mwaka jana kwa tuhuma za kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.

Lema amekuwa akikwama kupata dhamana kutokana na sarakasi za kisheria zilizosababisha upande wa utetezi uende hadi Mahakama Kuu katika kuhakikisha anapata haki hiyo, lakini hadi sasa bado vita hiyo ya kisheria haijaisha.

Lissu amewaambia waandishi wa habari mjini Arusha kwamba wataongeza nguvu ya mawakili wa Chadema katika kesi hiyo kila itakapokuwa ikitajwa mahakamani.

Pia, watakiandikia Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) barua rasmi kukitaka kitoe tamko kwa namna yoyote ili kiseme katika kesi ya Lema kipo upande upi na kama kikisema hakihusiki, basi hakutakuwa na chama cha wanasheria nchini na wakiona kuna hoja, basi watawataka watoe mawakili waliopo Arusha kusaidia kesi zinazomkabili Lema.

“Hawa wanasheria wasijidai hamnazo wakati mbunge wao yupo mahabusu. Tutawaambia wawepo mahakamani kwa kuwa wananchi wa kawaida hawaruhusiwi kuja kusikiliza kesi hiyo, basi wajae wanasheria,” amesema Lissu.

Awali, Mbowe amesema chama na viongozi waliamua kwenda kumuona Lema na familia yake kwa kuwa yupo mahabusu kinyume na haki za binadamu.

“Lema ana moyo mkuu sana na amejifunza mambo mengi kwa mujibu wa maelezo yake. Anasema wapo mahabusu asilimia 70 wenye makosa yanayostahili kupewa dhamana, lakini hawajapewa,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
ONGEZENI NGUVU ZAIDI KAMANDA AACHIWE NA KAMA SIVYO BASI AHUKUMIWE KAMA ANA HATIA.....
 
Back
Top Bottom