CHADEMA yaitisha maandamano Musoma

Selous

JF-Expert Member
Jan 13, 2008
1,325
144
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Mara kimepanga kufanya maandamano makubwa ya kuingia ndani ya mgodi wa dhahabu wa North Mara, wilayani Tarime kudai asilimia moja ya vijiji vitano vinavyouzunguka kulingana na mkataba na mwekezaji.

Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mara, Machage Bartholomew Machage alisema kwenye mkutano wa hadhara kuwa zaidi ya miaka 10 ya uchimbaji wa dhahabu katika mgodi huo, vijiji vitano vya Kewanja, Kerende, Nyamwaga, Genkuru na Nyangoto havijawahi kulipwa asilimia moja ya mapato ya mgodi huo kama ilivyo kwenye mkataba.

Machage alisema mwekezaji huyo pia ameshindwa kutekeleza huduma za jamii alizoahidi kuzitoa katika vijiji hivyo, ambazo ni ujenzi wa vituo vya afya, umeme, maji, barabara na shule, badala yake amekuwa akifanya ukarabati kinyume cha mkataba aliowekeana na serikali za vijiji hivyo.

“Tutaitisha maandamano makubwa ya wananchi, na mimi ndiye nitakayeyaongoza kuelekea mgodini ili tuishinikize serikali iweze kumwagiza mwekezaji atoe asilimia moja ya mapato yake. Wananchi wa Nyamongo hatuwezi kuendelea kubaki masikini wakati dhahabu yetu inawanufaisha watu wengine, nipeni muda nimalize ziara zangu, halafu nitakuja tufanye maandamano,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Vijana wa CHADEMA Wilaya ya Musoma Mjini, Mwita Julius alisema licha ya Mkoa wa Mara kuchangia pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 10 kutokana na dhahabu inayochimbwa kwenye mgodi wa North Mara, inasikitisha kuona kwamba wakazi wa Nyamongo wanaishi katika lindi la umasikini. Mkutano huo wa hadhara ni wa kwanza kuhutubiwa na Machage tangu alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara kujaza nafasi iliyoachwa wazi na marehemu Chacha Wangwe aliyefariki dunia mwaka juzi


Mwandishi, Mabere Makubi, Musoma, Tanzania Daima
 
Wanayo haki ya kudai madai yao na pia ni aibu kubwa sana kuona watu walizungukwa na dhahabu hata rasilimali hawanufaiki hata kidogo
 
Si afadhali hawa? Kuna jamaa kule usukumani/nyamwezini nasikia wanaondoka hata kodi hawajaanza kulipa.

Hata zege la kuunganisha Nzega na Mkoani bado? mhh
 
Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mara, Machage Bartholomew Machage alisema kwenye mkutano wa hadhara kuwa zaidi ya miaka 10 ya uchimbaji wa dhahabu katika mgodi huo, vijiji vitano vya Kewanja, Kerende, Nyamwaga, Genkuru na Nyangoto havijawahi kulipwa asilimia moja ya mapato ya mgodi huo kama ilivyo kwenye mkataba
ASANTE WANACHADEMA kwa kuendelea na vita dhidi ya hayo majizi wa raslimali zetu, kweli nawapongeza....hakuna kula hadi kieleweke.
 
HII IMETULIA, kila kona nyie chadema fanyeni hivi hivi
Inafurahisha kuona kuwa sasa CHADEMA wanaanza kusikiliza tuliyowaambia wafanye miaka kadhaa iliyopita. Unfortunately inaweza ikawa ni a bit too late kwa wao kufaidika na hii civil disobedience kwenye uchaguzi ujao. Lakini nafuu wajaribu maandamano kuliko kuendelea kuruka-ruka na helkopta.
 
Inafurahisha kuona kuwa sasa CHADEMA wanaanza kusikiliza tuliyowaambia wafanye miaka kadhaa iliyopita. Unfortunately inaweza ikawa ni a bit too late kwa wao kufaidika na hii civil disobedience kwenye uchaguzi ujao. Lakini nafuu wajaribu maandamano kuliko kuendelea kuruka-ruka na helkopta.

sure mkuu!

Huu ndio mtaji pekee, maandamano, yapewe kibali a yasipewe kibali!

Leo hii Chadema wakitaka washike nchi hata mwaka huu, ebu andamaneni kudai haki ya watanzania, halafu mtu kama Slaa akae Segerea siku 2 tu!

mtapunguza hata bajeti yenu ya kampeni! wala helkopta itakuwa haina kazi tena,maana mtakuwa mmejiuza, tunavyopiga kelele wengine humu tunataka mfikie nafasi hii adimu na ya lazima!
 
One of the penalties of not getting involved in politics you end up being governed by your inferior - Plato
 
kuandamana sio tatizo lakini je wataungwa mkono na walengwa?.............maana kuna tabu klubwa kwa watz kudai au kuonesha hisia zao kwa njia ya maandamano.......MI NAWATAKIA KILA LA KHERI KATIKA MAANDAMANO HAYO....
mbona ccm huwa haiandamani lakini bado inachaguliwa?SWALI GUMU LENYE MJADALA MREFU SANA....NAPATA HASIRA SASA NAISHIA HAPA....
 
kuandamana sio tatizo lakini je wataungwa mkono na walengwa?.............maana kuna tabu klubwa kwa watz kudai au kuonesha hisia zao kwa njia ya maandamano.......MI NAWATAKIA KILA LA KHERI KATIKA MAANDAMANO HAYO....
mbona ccm huwa haiandamani lakini bado inachaguliwa?SWALI GUMU LENYE MJADALA MREFU SANA....NAPATA HASIRA SASA NAISHIA HAPA....

sisi tunataka waandamane, kuungwa mkono kutakuja tu baada ya maandamano!
 
1.jpg


Maandamano makubwa yalifanyika mjini Harare hivi karibuni kumshinikiza kibabu Mugabe kuhusu maslahi yao, hakukua na mkwaruzo katika maandamano haya. Je, sisi kama Watanzania tumeshindwa nini kuiga mfano na kumshinikiza Jakaya kuwatosa makuwadi wake - akina Rostam Azizi Fisadi papa hili linajulikana, Chenge, Mkapa, Lowasa na wenzake?

Wako wapi wale mashujaa ambao hawawezi kuona hili taifa linateketea kwa sababu ya Mafisadi wachache. Wako wapi wale viongozi mahiri wa kuweza kuwaamsha mamillioni ya walalahoi na walipa kodi? Wako wapi wale mashujaa wa kuweza kuweka bendera ya Tanzania kwenye mlima Kilimanjaro na mwenge wake kuwamulika Lowasa, Rostam Azizi, Chenge, Mkapa na magenge yao ya Ufisadi?

Siku za mwizi zinajulikana huwa hazizidi 40.
 
Kuandamana ndiyo njia pekee ya wanyonge ku express their indignations, swlala ni kwamba watapewa kibali? Kuna tabia ya serikali yetu kuwanyima wanyonge vibali vya kuandamana. Sijui wanaogpa kitugani!!!. Tunajitia tuna amani lakini tunashinwa na zimbabwe wanaandamana kwa amani.
Umefika wakati watu wakatae kunyayaswa, wachukue haki yao ya kuandamana hata kama polisi watakataa kutoa kibali.
Naogopa watawnyima kibali kwani huo mgodi kunawakubwa wanakula, hivyo itakuwa nikuinglia chakula chao.
Watanzania tukatae kunyanyaswa na watu wasio na madili wezi wa haki za wanyonge.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom