CHADEMA yaitisha Kikao cha dharura cha Kamati Kuu kujadili hali ya siasa nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yaitisha Kikao cha dharura cha Kamati Kuu kujadili hali ya siasa nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, Sep 9, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  [FONT=&amp]TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama, Mheshimiwa Freeman Mbowe, itakutana tarehe 9/9/2012 katika kikao cha dharura, kujadili hali ya siasa nchini, kufuatia mfululizo wa matukio ya mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi kwenye shughuli halali (kwa mujibu wa katiba ya nchi) za chama na njama za CCM na baadhi ya viongozi wa Serikali kudhibiti Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) kwa mbinu haramu.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Itakumbukwa hivi karibuni baada ya mauaji ya Ndugu Ali Singano (Zona) mjini Morogoro, yaliyosababishwa na Jeshi la Polisi mkoani humo wakati walipoingilia kwa nia ya kuvuruga mapokezi na mkutano wa CHADEMA, chama kilitoa kauli kumtaka Rais Jakaya Kikwete aagize kutumika kwa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (Inquest Act) ili kubaini chanzo na kuondoa utata wa kifo cha kijana huyo.[/FONT][FONT=&amp]

  [/FONT]
  [FONT=&amp]Hivi karibuni, baada ya mauaji ya mwandishi wa habari wa Channel Ten na Magic FM, Ndugu Daudi Mwangosi, CHADEMA kilitoa tamko kumtaka Rais Kikwete, aagize kufanyika uchunguzi huru kupitia tume ya kimahakama. Kwani katika tukio hilo hakukuwa na utata kuwa mwandishi huyo aliuwawa na polisi. Hivyo uchunguzi huru ulihitajika ili kubaini vitu vya ziada, kama vile kwa nini kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa katiba, haki za binadamu na sheria za nchi na nani alitoa amri za mauaji hayo.[/FONT][FONT=&amp]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Itakumbukwa pia kuwa CHADEMA kilipinga kuundwa kwa kamati ya kuchunguza tukio la kuuwawa kwa Mwangosi, iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, kwa sababu iliundwa kinyume cha sheria ya tume za uchunguzi, ikiwa na lengo la kufunika mambo na kurejesha uhusiano wa serikali na vyombo vya habari, badala ya kutafuta ukweli. Kwa mara nyingine tena kilimtaka Rais Kikwete aunde tume huru ya uchunguzi kwa mujibu wa sheria ili kweli tupu ijulikane.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Wakati chama kikitangaza kuahirisha kwa muda mikutano ya Operesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), mjini Iringa, kilisisitiza kauli yake ya kumtaka Rais Kikwete kuingilia kati kuhakikisha analinda katiba ya nchi inayotambua haki ya kuishi, kwa kagiza uchunguzi huru ufanyike ili kubaini ukweli wa tukio hilo na kuzuia hali hii ya vyombo vya dola kufanya mauaji ikiwa na lengo la kutisha wapinzani na wakosoaji wa serikali ya CCM.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Kutokana na ukimya wa Rais Kikwete katika matukio hayo na mengine ya namna hiyo ambapo raia wasiokuwa na hatia wametekwa, kuteswa na kuuwawa na vyombo vya dola au wakiwa mikononi mwa vyombo hivyo, CHADEMA kimeitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu kujadili hali hii, kisha kufanya maamuzi ya hatua zaidi za kuchukua dhidi ya Jeshi la Polisi na Serikali inayoongozwa na CCM, kwa manufaa ya taifa letu na Watanzania wote kwa ujumla.[/FONT]

  [FONT=&amp]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Imetolewa leo 8 Septemba, 2012 na;

  [/FONT]

  [FONT=&amp]Tumaini Makene,
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Ofisa Habari wa CHADEMA;[/FONT][FONT=&amp]
  Kurugenzi ya Habari na Uenezi;
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Makao Makuu ya CHADEMA, Dar es Salaam [/FONT]
   
 2. P

  Penguine JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Kila la kheri. Dharura ilenge ktk kutafuta suluhu makini ya matatizo haya. Dharura ije na mikakati kabambe ambayo itaimarisha chama kuliko kukiangamiza. Dharura ije na mikakati yenye matumaini zaidi ya ukombozi kuliko mifarakano miongoni mwenu. Sauti ya Umma ni Sauti ya Mungu.
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Tunasubiri matokeo ya kikao!! bila shaka umakini wa viongozi utakuja na mikakati mizuri ya kuelekea pazuri zaidi!!
   
 4. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Kikao kisiishie katika kujadili vifo tu lakini kiende mbele na kuangalia hatari ya TBC kutumbukiza nchi katika machafuko.
  Pia kuna kila dalili za udini kupamba moto lakini as long as zinaonekana kupinga upepo wa CDM serikali imekaa kimya mno.
  Ukabila unazungumzwa wazi lakini ukemeaji wa viongozi wa juu wa serikalina CCM unaonekana kuwa wa kiwango cha chini.
  Haya yajadiliwe kwa kina na miongozo madhubuti itolewe.
  Kila la heri .
   
 5. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  "Kufuatia mfululizo wa matukio ya mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi kwenye shughuli halali (kwa mujibu wa katiba ya nchi) za chama na njama za CCM na baadhi ya viongozi wa Serikali kudhibiti Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) kwa mbinu haramu".

  Kwa kweli kwa mara ya kwanza sasa naona CCM ni zaidi ya makaburu. Ila hatutawaachia kwani hatuwaogopi. Makamanda tuko pamoja, kama noma na iwe noma. CCM ni makaburu weusi.
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  nanii naye atakuwepo?
   
 7. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #7
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Haya Bwana Kamanda MIGNON.
   
 8. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  ZZK au?
   
 9. B

  Baba Kimoko Member

  #9
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  lazma awepo.
   
 10. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  unamaanisha zito ?lazma awepo ili apate habari za kumpelekea jk katika ileee mipango yao ya 015
   
 11. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Jamaa pale magogoni sijui anakazi gani nyingine zaidi ya kula chakula cha walipa tax na kwenda nje kuomba msaada,sidhani kama kuna kazi nyingine zaidi ya hii, amekaa kimya it means kama kiongozi wa hii nchi anafurahi na inaonekana na yeye anashiriki kwenye huu mchezo mchafu,subirini tu....Chadema fanyeni kazi tupo pamoja kwa kila jambo

  Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
   
 12. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Zitto now sidhani kama yupo nchini....So naona hatokuwepo

  Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
   
 13. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yuko Colombo, Sri Lanka na Makinda kwenye Mkutano wa CPA.
   
 14. B

  Baba Kimoko Member

  #14
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  lazma awepo.
   
 15. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Unamfahamu anayemzungumzia??

  Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
   
Loading...