CHADEMA yaishukia SMZ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yaishukia SMZ

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee wa Kale, Feb 18, 2009.

 1. M

  Mzee wa Kale Member

  #1
  Feb 18, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na Mwandishi Wetu, Zanzibar

  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeeleza kusikitishwa na Serikali ya Zanzibar (SMZ) kuingilia majukumu ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), wakati huu wa maandalizi ya kuandikisha wapiga kura katika daftari la kudumu.

  Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Hamad Mussa Yussuf, alieeleza masikitiko hayo alipohutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.

  Alisema NEC ni chombo huru na kwamba inapaswa kutekeleza majukumu yake bila ya kuingiliwa na serikali au taasisi yoyote ile.

  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hivi karibuni ilipinga azima ya Tume ya Uchaguzi kutumia vyeti vya kuzaliwa, leseni za biashara na magari kutumika kama kielelezo cha mpiga kura na kutangaza tume hiyo imevunja sheria ya uchaguzi.

  “CHADEMA tunalaani kitendo cha serikali kuingilia majukumu na kuipa maelekezo NEC,” alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.

  Alisema uamuzi wa ZEC kutumia vielelezo hivyo ilikuwa ni muafaka kwa vile umelenga kutanua demokrasia na ungesaidia wananchi wengi hasa wale ambao hawajakamilisha taratibu za kupata vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi.

  Alisema kutokana na kitendo hicho cha serikali, Mwenyekiti wa ZEC, Khatib Mwinyichande anapaswa kujiuzulu kutokana na tume yake kuingiliwa utekelezaji wa majukumu yake na serikali.

  Yussuf alisema kitendo hicho cha serikali hata makamishna kutoka CUF wanapaswa kuwajibika kama kweli chama chao kinapinga kitendo hicho.

  Alisema suala la daftari la kudumu la wapiga kura ni jambo la msingi na kitendo cha kukataa vyeti vya kuzaliwa kinaweza kusababisha wananchi wengi kukosa haki za kuandikishwa katika daftari hilo.

  Akizungumzia ununuzi wa magari ya kifahari kwa viongozi wa serikali, wakati wananchi wakikabiliwa na huduma mbovu za afya na elimu, alisema kitendo hicho ni kinyume cha ahadi ya kupunguza umaskini unaowakabili wananchi.

  Alieleza kipaumbele katika mkazo wa kupunguza umaskini ni kuimarisha sekta za kilimo, uvuvi na utalii na iwapo fedha hizo zingetumika kuimarisha kilimo zingesaidia kupunguza umaskini.

  Akizungumza katika mkutano huo, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Mzee Said Mzee, alisema CHADEMA imesikitishwa na matokeo mabaya ya wanafunzi wa Zanzibar katika mitihani ya kidato cha nne iliyopita.

  Alisema matukio hayo mabaya yanasababishwa na mazingira duni yanayoikabili sekta hiyo na kuitaka serikali kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu kwa vile ndiyo itakayosaidia kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
   
 2. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  MKO WAPI MNAOFIKIRI KUWA ZANZIBAR NI SEHEMU YA BARA? Vioneni vitendo hivi na mtowe maoni yenu au hayawahusu? Yanakuhusuni pale tu tunapoambiwa tusiweke makazi ya kudumu?
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Awali ya yote ni vema watu wakajua kazi za Sheha katika Shehia yake
   
Loading...