CHADEMA Yaisambaratisha CCM Kyela; ngome ya Mwakyembe yatikiswa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Yaisambaratisha CCM Kyela; ngome ya Mwakyembe yatikiswa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Nov 4, 2009.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Nov 4, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ngome ya Siasa ya Mbunge wa Kyela (CCM) Dkt Harrison Mwakyembe imesambaratishwa vibaya na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya wapambe wake karibu wote kuangushwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji!

  Kuangushwa kwa wapambe wake ni dalili za wazi mbaya kwa Dkt Mwakyembe anayeonekana hodari wa kutumia vyombo vya habari kujiaminisha kuwa anapendwa.

  Habari zilizopatikana kutoka Kyela zinaeleza kuwa mpambe wa Dkt Mwakyembe aliyekuwa amejitosa kuwania kitongoji cha Ikolo anakoishi mbunge huyo, ameangushwa na kitongoji hicho kwa sasa kipo chini ya CHADEMA.

  Dkt Mwakyembe aliyekuwa amepanga wapambe wake waweze kutwaa vitongoji kadhaa ili aweze kujiwekea mazingira mazuri ya kushinda kwenye kinyang'anyiro mwakani lakini juhudi zimefikia tamati baada ya CHADEMA kuwazidi ujanja na kuibuka washindi kwenye vitongoji vya Kyela Mjini, Mikumi, Bondeni, Mpakani, Ndandalo, Mwaya, Ngyekye, Bwato B na Ipinda!

  (Source: Tazama, tr 3-9/11/2009, uk. 1-2).
   
 2. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hizi ni salamu kwa Mwakyembe mwaka 2010,kwani atumuhiyaji kabisa.
  Yeye kelele richmond wakati jimboni hata barabara moja kashindwa kujenga,umeme ndio usiseme aibu tu?
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Dr jiandae kurudi faculty. mambo ya kuwapigia wananchi magoti wakuchague noma.
   
 4. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,145
  Likes Received: 1,236
  Trophy Points: 280
  Hii imekaa kishabiki zaidi,
   
 5. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ni kweli. Tutofautishe wapambe wa Mwakyembe na Mwakyembe mwenyewe. Kuwa mpambe wa Mwakyembe hakumpi mtu free ticketi ya kushinda uchaguzi wako binafsi. Unaweza ukawa mpambe mkubwa wa mwanasiasa hata kama ni Rais lakini una mapungufu yako binafsi ambayo wananchi wanayatambua vizuri hivyo hata ufanyeje kama huna sifa wala uwezo wa kuchaguliwa utakataliwa na wapiga kura. Itakuwa ni kujidanganya kutabiri ushindi wa Mwakyembe 2010 kwa kutumia kigezo cha kuanguka kwa wapambe wake. Inawezekana wapambe wake ni wazuri kwa kupiga debe kwa wengine lakini inapokuja kwao wanashindwa maana mganga hajigangi!
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Nov 4, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kama chama cha Mwakyembe hakikubaliki nyumbani kwake na kumbuka yeye aliwapanga wapambe wake ili mambo yamwendee murua mwakani, hizo sio salamu tosha akae chonjo 2010?
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Nov 4, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Du kama ni kweli basi jamaa ana kazi 2010, bora arudi darasani aendelee na kazi ya kufundisha.
   
 8. S

  Samwel JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2007
  Messages: 224
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  .

  Hayo tuliisha wahi kuyaandika humo,Kwamba huyo bwana anapenda sifa sana.yeye anafikiri uongozi ni kukimilia kwenye gazeti la nipeshe na majra.
  Jimbo la Kyela ni maarufu. kutokana na domo lake na sio kwa maendeleo.Msomi mzima utaendesha jimbo kwa kutumia media?(Nipashe na Majira)
   
 9. E

  Engineer JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Buchanan,

  Hii habari mbona niliileta siku ile ile ya uchaguzi?

  Kilichofanyika ni kwamba mheshimiwa aliweka wapambe wake ili wachukue baadhi ya vitongoji na akafanya kampeni ya wiki nzima.

  Kambi ya Mwakalinga (sina uhakika kama Mwakalinga aliidhinisha strategy hii) ilipoona hilo ikaweka mkakati wa kuwatungua hao wapambe wote wa Mwakyembe. Baadhi ya wanachama wa CCM wakaamua kugombea kupitia CHADEMA na hilo kundi likawaunga mkono.

  Wao wanasema lengo lilikuwa kumpa kipigo mbunge na pia kuwatisha madiwani wachache ambao bado wanamuunga mkono Mwakyembe kwamba wajiandae kupoteza nafasi zao kama wataendelea kumshabikia huyo msanii.

  Kweli strategy imefanya kazi sana maana hata kitongoji anakotoka Mwakyembe (Ikolo) nacho kikatekwa.

  Pigo kubwa lilikuwa mjini ambako Kilumbu, ambaye ndiye mfuasi mkubwa wa Mwakyembe aliangushwa na mzee mmoja mganga wa kienyeji.

  Ukiwa karibu na mwakyembe hapa Kyela kwasasa jua kitumbua chako kisiasa kiko hataraini.

  Mimi naona alifanya makosa makubwa sana kuweka wapambe wake maana hii imeonyesha watu wengi kwamba Dr ni weak na hata waliokuwa wanamuunga mkono, taratibu wanaanza kutafuta namba za Mwakalialinga ili wamsalimie.

  Hizo ndio siasa za Kyela. Ila Mwakalinga aangalia maana hao CHADEMA wasije wakapata nguvu na kuamua kuitumia dhidi yake. Pia mwenyekiti wa CCM wa wilaya ambaye ndio pekee katika uongozi wa chama bado yuko na Mwakyembe, ameshaanza kusema Mwakalinga anawasaidia CHADEMA. Lakini wapambe wa Mwakalinga wanatamba kwamba hawaogopi hilo maana kwenye vikao vya CCM wakiamua nani ni hatari kwa CCM, kati ya hawa watu wawili, itaonekana ni bora kuwa na Mwakalinga kuliko Mwakyembe.

  Jambo lingine la kushangaza ni kwamba CHADEMA Kyela walikuwa karibu sana na Mwakyembe na ghafla wamebadilika sana na wanaongoza kumuita msanii.

  CCM bado wameshinda Kyela kwa asilimia zaidi ya 95.
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Nov 4, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Engineer sikuiona thread yako, kwa bahati mbaya, sorry! Hata hivyo tuwie radhi wale ambao hawakuiona kama mimi wa-exhaust maoni yao!
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0

  - Mungu Aibariki Kyela na hasa wananchi wake walalahoi.

  Respect.


  FMEs!
   
 12. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,644
  Likes Received: 21,855
  Trophy Points: 280
  Mimi tatizo langu liko kwenye source ya habari hiyo. Kwa mtazamo wangu hilo gazeti ni moja ya magazeti nisiyoyaamini hapa Duniani.
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Nov 4, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nikisoma magazeti ya Nipashe na Majira mara kwa mara nimeshaona kuwa yako pro-Mwakyembe! Kwa kifupi kumbe ni sabuni ya Dkt ya kumsafisha na kashfa ya kulamba posho mbili kwa kazi moja, kukataa kuhojiwa na TAKUKURU huku akijua kufanya hivyo ni kosa la jinai chini ya kifungu cha 10(2) cha CPA, 1985, kulipwa mafao ya kwenda kutibiwa Ujerumani kumbe hujaenda kutibiwa, kutoku-declare interest ya umeme wa upepo Singida wakati wa kufuatilia kashfa ya Richmond, kutoa taarifa 'nusu' ya kufuatilia suala la Richmond kwa mwavuli wa 'kuficha aibu ya Serikali' nk. Kaazi kweli kweli!
   
 14. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Mkuu,
  Kama Majira na Nipashe yako pro-Mwakyembe, inakuwaje Mwandishi wa Tazama aseme Chadema yaisambaratisha Kyela, wakati CCM imeshinda kwa asililmia 95? Je kama ni kuegemea upande si wazi mwandishi huyu yuko against Mwakyembe?
  Halafu, kutodecrare interest kwenye Taarifa yake ya Richmond, kunaondoa ukweli kwamba Richmond ni kampuni hewa, ikliyoundwa kwa minajili ya utapeli ?
  Na je, Mwakyembe alikuwa na kampuni yake kwenye mchakato wa Richmond by then?
   
 15. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35

  Cheap politics
   
 16. G

  Gwa-Ntwa Member

  #16
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 24, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna wanakyela feki humu ambao wanajifanya mslahi yao ni kyela tu, hiyo ni dhambi mbaya! kwamba wanachokiona kwa Dr, ni kusahau jimbo na kuwa Mtaifa na kwao hili ni baya! HAWATUFAI

  hivi unafikiri barabara itajengwa kwa kirahisi ndani ya miaka 4 wakati tuko kwenye mapambano................

  Mheshimiwa Shukuru apange bajeti, Mhe. Mwakipesile atoe mazingira mazuri ya ketekelezeka....bado.

  tuje kwenye source;tazama. lile la charles charles!!!!!!!!!!!
  kama ndio washabiki wa kyela wanatumia source ambayo kila mtu anajua imecling na akina nani, na hao akina nani wanamsaada gani kwa taifa....basi hata akikosa ubunge next He will be right at, cause its seemz most of people are ignorance by choice, not by design as most pple be.

  all in all, Dr ni kichwa, na amebadilisha mfumo wa kisiasa, majadiliano mpaka ushabiki.
  within 4 years as MP, things have changed totaly. Na kwa wale wanaodhani watatudiscourage kwa kupitia humu ndani, ni ngumu, jamaa influence yake bado ni great per now, i don knw next!

  bravo Dr
   
 17. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #17
  Nov 4, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa habari ya magazeti kuwa pro-somebody nafikiri uko sahihi, japokuwa title ya thread originally ilikuwa inasomeka "CHADEMA yaisambaratisha Ngome ya Dkt Mwakyembe." CCM ilikuwa haijatajwa, naona kuna mshabiki amefanya edition kwenye post yangu ya kwanza! Just being curious: mambo ambayo Dkt Mwakyembe na Kamati Teule kuhusu Richmond ni yapi na waliyaacha kwa manufaa ya nani?
   
 18. E

  Engineer JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gwa-Ntwa,

  Hata kama gazeti lililoandika lina matatizo lakini habari yenyewe ina ukweli.

  Labda kitu ambacho mwandishi hakuonyesha ni hicho cha makundi ndani ya CCM yanavyopigana na faida inavyoweza kupatikana kwa CHADEMA.

  CCM wameshinda viti vingi Kyela, swali la kijiuliza ni kwanini pale ambapo mbunge aliweka wapambe wake, wote wakabwagwa?

  Watu wanashangaa mpambe wake kushindwa kule Ikolo ambako ndio nyumbani kwa Mwakyembe. Unategemea nini kwa mtu ambaye ana ugomvi na hata majirani zake na wala hata hawapeani mikono?

  Mimi huwa nashangaa kama Mwakyembe kweli ni mwanasdiasa maana anatengeneza maadui wengi mno wakati mwanasiasa lazima uwe bingwa wa kutengeneza marafiki na wala sio maadaui.
   
 19. E

  Engineer JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu,

  Vipi zile habari zako fake za vikao vya NEC unaona hazitoshi na unaanza kuingilia na Kyela?

  Sisi hatuhitaji kupiga simu kujua yanayotokea Kyela, tunayaona yakitendeka. Utashangaa sana mwaka huu na hao wapiganaji wako.

  Mpigia simu huyo rafiki yako Mwakyembe na mwulize mbona anashindwa hata kusalimiana na majirani zake?

  Vinginevyo ya Kyela niachie mimi engineer wa Majungu according to Masanilo (aka Ze Comedy_ niendelee kuwaletea za jikoni.
   
 20. G

  Gwa-Ntwa Member

  #20
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 24, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eng..
  Unakumbuka one time ilisikika kwamba wananchi wanamuhitaji aende CHADEMA?

  ninachokiona in roots wanakyela wamechoka na CCM lakini sio na Harison. sababu kwa sasa bado sijaona alternative ambayo wanayo, ambayo ni afadhali kuliko aliyopo, si Chadema wala CCM.

  Na chadema kufanya vizuri japo kwa 5% ni mwamko wa Mkoa wote since 1995' politics, Mbeya vijijini campaign, operation sangara na ziara ya Raisi iliyopita.
  Na ukiangalia vizuri ni vita kati ya mwakyembe na 'Mafisadi' na si CCM na Chadema, na kama ni hivyo, 'Mafisadi' wako kwenye vyama vyote vi2, so its like mwakyembe vs (ccm&chadema)
   
Loading...