CHADEMA yaikamia serikali; Yampa siku 90 Dk. Mwinyi kutatua kero za ardhi jeshini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yaikamia serikali; Yampa siku 90 Dk. Mwinyi kutatua kero za ardhi jeshini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 28, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  MAWAZIRI Vivuli wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wameishambulia vikali serikali ya Rais Jakaya Kikwete juu ya utawala wake, huku wakimpa siku 90 Waziri wa Ulinzi, Dk. Hussein Mwinyi, kuhakikisha anaipatia ufumbuzi migogoro mikubwa ya ardhi dhidi ya Jeshi la Ulinzi la Wananachi (JWTZ) na wananchi.
  Wameonya pia Ikulu kutogeuzwa sehemu ya miradi ya watu binafsi bali kuiheshimu kama sehemu takatifu kama ambavyo Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyowahi kunena.
  Mawaziri hao Kivuli walioishambulia serikali ni Joseph Mbilinyi (Vijana, Habari, Utamaduni na Michezo), Ezekiel Wenje (Mambo ya Nje) na Highness Kiwia (Maji).
  Wakizungumza juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwaja vya Sahara jijini Mwanza, walisema serikali imeonekana kushindwa kuwatumikia vyema wananchi wake, jambo ambalo linawaumiza wananchi hao.
  Kiwia ambaye mbunge wa Jimbo la Ilemela jijini Mwanza, alieleza kuchukizwa na kitendo cha uvamizi wa mashamba ya wananchi wa eneo la Nyankunguru na Lukobe Ilemela unaofanywa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
  Alisema, JWTZ imehodhi mashamba ya wananchi bila kuwalipa fidia, huku wakitembeza vipigo na kuwazuia wananchi wa maeneo hayo kujenga wala kuendeleza makazi yao, jambo ambalo alidai ni uonevu wa hali ya juu.
  Kulingana na hayo, alitoa siku 90 kwa Waziri wa Ulinzi, Dk. Mwinyi, kuhakikisha analipatia ufumbuzi suala hilo, vinginevyo ataitisha maandamano makubwa ya kwenda hadi kambi hiyo ya jeshi Ilemela kudai haki za wananchi hao.
  “Natoa siku 90 kwa Jeshi kupitia waziri wake, kuhakikisha unapatikana muafaka kwa wananchi wa Nyankunguru, vinginevyo tutaenda pale na waandae mizinga yao yote,” alisema Kiwia.
  Kiwia alitoa pia siku 90 kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, mkurugenzi wa jiji, mganga mkuu wa mkoa pamoja na meya wa jiji hilo, kuhakikisha wanamaliza tatizo la uhaba wa dawa hospitalini, vituo vya afya na zahanati, vinginevyo nguvu ya umma itawashukia.
  Naye Mbilinyi ambaye ni mbunge wa Mbeya mjini (CHADEMA), alisikitishwa na hatua ya kuporwa mradi wake wa Malaria Haikubaliki na kudai kwamba alichakachuliwa mradi wake huo na Ikulu kisha kupewa mtu mwingine.
  “Mradi wa Malaria Haikubaliki ulikuwa wangu, lakini mtu mmoja ambaye yuko karibu na Ikulu (akamtaja jina), alifanya ujanja na kupewa mradi huu, iliniuma sana!
  “Ikulu isigeuzwe kuwa mradi wa watu kujinufaisha. Eti baadaye waliteuliwa mabalozi na kwenda nje ya nchi kuhojiwa ili wawaone watu wa Ulaya...sasa wanapoonekana huko Ulaya inasaidia nini Tanzania kuua mbu?” alihoji Mbilinyi maarufu kwa jina la Mr. Sugu.
  Kuhusu Masha, Mbilinyi alisema wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani alilitia hasara taifa kwa kutumia msafara wa pikipiki kwa kudai anawahi kazini wakati pikipiki hizo zilikuwa zikinyweshwa mafuta kwa pesa za umma. Naye Mbunge wa Nyamagana, Wenje, alisema tayari ameshaanza kusomesha watoto 908 kidato cha kwanza hadi cha nne, na watoto hao ni wale wanaotoka kwenye familia maskini. Kwa mujibu wa Wenje, yeye ni mbunge wa vitendo na kwamba ifikapo mwezi Septemba shule zote jimboni humo zitakuwa na madawati ya kutosha hivyo kuondoa adha kwa wanafunzi kukaa chini.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ni rahisi kuwapa Ardhi wawekaji uchwara rather than Military People???
   
 3. z

  zamlock JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  safi sana makamanda nawaunga mkono mimi nawazimia kichizi kwa sababu mnafanya kazi kwa vitendo na huyo mzee ruksa asipotekeleza inaitwa nguvu ya uma hata mimi nitakuja kushiriki maandamano alafu tuone kama hilo jesho litapambana na wananchi
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Siku 9, siku 30, siku 90,

  Sijui zingine ngapi mtatowa, duhh! Chadema wana washauri wazuri kweli. Bado miaka minne na nusu, muingie tena ulingoni, wacheni kudanganya watu na haya ya kutowa siku. Mbona zile siku 9 za mwanzo zimeisha. mmefanya nini?
   
 5. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,827
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  hii mipango ya Wenje nimeipenda mno!Safi sana inadhihirisha ni kwa namna gani hutaki masihara kwa wapiga kura wako hongera sana kaka....
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MHESHIWA PINDA CHINI YA RADAR YA ALIYEWAHI KUMUAMINI: UWEZO TUNAO

  Eti umesema Mhe Peter Kayanza Mizengo Pinda aka Mtoto wa Mkulima niliyewahi kumpenda na kumuamini ni JAAAAASIRI??? Ni ujasiri gani tena huo, huyu mtoto wa mkulima nisioifahamu mie???

  Nakuambia mimi huyu mtoto wa mkulima siku hizi simuelewi kabisa juu ya lolote lile!! Na kwa kukuthibitishia hilo mwenzenu tayari nimekua nikijihesabia KUMPOTEZA KIPENZI sawa sawa na ninsi nilivyowahi kujihesabia huko nyuma nikiwa sekondari huku nikion CCM ikinilazimisha kumpoteza KIPENZI CHA ROHO YANGU KISIASA MHE AUGUSTINO LYATONGA WA MREMA (the bureaucratic rule arch-rival charismatic leader) na hivi majuzi tena nikalazimishwa KUMPOTEZA KIPENZI MWINGINE JOHN POMBE MAGUFULI kwa kukataliwa kuzingatia sheria mstari kwa mstari kwenye utendaji wake.

  Nakuuliza mwenzangu ni ujasiri gani huo ulioigundua kwa huyu aliyewahi kuwa Mtoto wa Mkulima huko nyuma na sasa hivi kabakia tu kuwa Mtoto wa walima bustani ya mchicha Mto Msimbazi Dar es Salaam??

  Hakika ili niweze kumtendea haki katika kuanza kwangu kumkataa kule kwanza kulitokea azimio nzito sana katika kikao cha kukata na shoka ambapo wahudhuriaji walikua ni akina (1) Uwezo Tunao mwenye Kupenda, (2) Uwezo Tunao akili na fikra pamoja na (3) Uwezo Tunao jicho la walalahoi. Mkutano huu wa zaidi ya wiki ulikua mkali kweli kweli tena wenye futa nikuvute mkubwa mno.

  Lakini labda nianze kwa kuwashukuru sana tena sana ndugu zangu wengine hawa (Uwezo Tunao family) kwa kuafiki mapendekeza ya huyo mjumbe wa pili hapo juu ya kwamba kwanza tufanye utafiti utakaotuelekeza kama kweli bado kuna matumaini yamebakia ndani ya Baba huyu 'Mtoto wa Mkulima' hadi hapa tulipofikia au laa. Katika kutekeleza azima hiyo sote watatu tulichagua kujipa siku 90 kumsoma juu ya kauli zake na kwa kiasi gani zinavyokubaliana na matendo yake katika jamii yetu hii.

  Kiukweli kabisa, japo MATOKEO YA UTAFITI WA UWEZO TUNAO FAMILI NA HATIMA YA MHESHIMIWA PINDA A.K.A MTOTO WA MKULIMA utakamilika hapo Aprili 23, hata hivyo dalili za awali hazimpendelei saaana huyu kipenzi changu ambaye nasikitika kuelekea kumpoza hivi karibuni katika kitabu changu cha Wanasiasa ninaowaamini nchini.

  Hizo dalili za awali zisizompendelea huyu 'rafiki wa roho yangu, mara baada ya kumsogeza kwa karibu zaidi chini ya drubini yangu kwenye maabara binafsi ya siasa nchini (microscope) kumebainika mambo kadhaa wa kadhaa juu yake huyu mwenzetu. Na endapo dlili hizi zenye gizo totoro hazioonekana kupona kitu basi nawahakikishieni kwamba sitochelewa kupendekeza hapa JF na kote nchini kwamba hicho cheo cha heshima cha 'Mtoto wa Mkulima' nacho tukamnyang'anye kabisa kwa kutoitendea haki ipasavyo.

  Kwa mwenzetu, ndugu yetu na Baba yetu wa Taifa Mwalimu Nyerere cheo kile cha heshima toka kwetu wananchi aliendelea kukitumikia hadi dakika ya mwisho aliposema maneno mawili mtatu kwa Mzee Rashidi Simba wa Vita pembeni mwa kitanda chake hospitalini kule Uingereza hivyo hata akaendelea kustahili kubakia nayo hata baada ya safari ya kurudi kwa muumba wake ilipowadia.

  Mapungufu mazito tuliyoyaona ni haya na ni bora akayafanyia kazi kwa haraka kabla hatujafunga faili na kuikabidhisha kwa wapiga kura kumpima nayo zaidi pamoja na kwamba keshaahidi kurudi kupumzika nyumbani mara baada ya utumishi wake kama Waziri Mkuu, Mheshimiwa Pinda ni:

  1. Kiongozi anayeogopa sana LAWAMA:

  Hii tabia imegeuka kuwa jela yake binafsi anayotembea nayo kila mahali kama mfungwa wa hiari. Kwa kukuthibitishia madai yangu haya utagundua kwamba Mhe Pinda siku zote hajawahi kuonyesha OWN INITIATED ACTION BALI NI MZEE WA REACTIONS tu. Nasema akome kukimbizana na upepo kwa mtindo wa zimamoto kwa kila atendalo.

  2. Mtaalam wa Kukasimu Madaraka, Mchovu wa Kufuatilia:

  Delegating power is a very good sign of a leader who has confidence in colleagues and teamwork spirit. Lakini kama huna muda wa kufuatilia ulioyakasimu, wala uwezo wa kuhakikisha kwamba kweli ulioyakasimu yanaleta matunda ya kugusika kwa mikono na kuonekana kwa macho basi mwenzetu ukae ukijua kwamba wengi huku nje wanajiuliza kiti hicho unachokalia unakiachia wazi lini???

  Uthibitisho wa madai yangu; Mzee Pinda alijichagulia kuparamia swala nyeti la Madai ya Katiba nchini na kwa kuelewa kwamba anayo GOODWILL kwetu sie walalahoi tulio wengi basi akaona vema kuchangamkia tenda hiyo.

  Lakini, kwa bahati mbaya sana 'Wa Mkulima ' hajagundua siri kwamba goodwill ni goodwill tu na inayo ukomo wake na kwamba kitendo cha kuuchukua swala la katiba na kujirithisha kuuficha ndani ya mfuko wake wa suruali ya nyloni ni jambo la hatari kuliko angeliacha tu swala hili bila kuahidi kulishughulikia kabisa.

  Katika hili nasema Mhe Pinda usiombe mtu na au kundi la watu waliyokumini pindi wanapogeuka na kukosa imani kwako - mungalie Ndugu yetu Mhe Kikwete na jinsi alivyotuchukulia for granted imani yote kwake na kura zote katika kipindi chake cha kwanza mpaka akafika mahala na kuona kwamba tuliomuamini baada ya kutusaliti basi ni bora akatumie njia ya mkato KUTUIBIA KABISA KARU nadhani lengo likiwa ni kupata SECOND CHANCE kurekebisha mambo lakini ndio hivyo maji ya kunywa yakishamwagika bora ukayapigie tu deki.

  Mheshimiwa Pinda kwa taarifa tu ni kwamba 'Nguvu ya Umma' tunasubiri kwa hamu kuona endapo tena utaipigia danadana swala la Katiba Mpya na Mtume huru za Uchaguzi; Bara na Visiwa hata isipitishwe kwenye bunge hili la mnamo mwezi huu wa April 2011!!!!

  3. Group Thinking

  Mheshimiwa Pinda ni muumini mkubwa wa kanisa au msikiti wa maamuzi ya kikundi kundi hivi. Hili jambo linampa shida sana kwa kuwa kila mara anakosa ORIGINALITY katika msururu wa mambo ya kutekeleza hivyo jambo linapoenda kombo anashindwa kulitafutia lango la pili kwa kuwa he is NOT never married to the original idea either.

  Kwa mtindo huu 'Wa Mkulima' ni kwamba utajikuta siku zote unageuka kuwa MTUMWA WA FIKRA ZA WASHAURI ambao pindi mambo yanapoharibika wao hucheka mtindo wa Jino-Pembe kwa kuwa siri yote wanayo kwamba wewe hauna input yoyote mle na kwamba hata zile perspective mikanganyiko walizokupa washauri mbali mbali wala haukuweza hata kujitengea muda wa peke yako with a BRUTALLY CRITICAL MIND.

  Kama uliwahi kusikia Mheshimiwa Mwl Nyerere, Mkapa, Dr Shein na Dr Magufuli walipata kuheshimika sana ni kule katika wao kujitengea muda usioingiliwa hata na mama watoto pale nyumbani ili AKALIFIKIRIE TAIFA LAKE KWA UDHATI KABISA NA MOYO WA KIZALENDO ili ku-Question, kuomba ufafanuzi zaidi, uthibitisho wa maelezo na hata kule kufanya SUPRISE SELF-FACT FINDING MISSION bila kuwa pompus anda embarrassing to others kama Vijikamati Vya Bunge tunavyovishuhudia hivi leo viki-play both Police and Court roles together on their subordinate line ministries and related institutions whereas the costitution ONLY asks the to Oversee and Advise.

  Wakati bado utafiti wetu juu ya Mtoto-wa-Mkulima na hasa kwa kumpima zaidi atakavyoshugulikia jambo la msingi zaidi kwa taifa (an immediate People-Centred Constitutional Overhaul call) au kuyaacha kwenye mikono ya wachache akina Oliver Mhaiki na Celina Kombani au atawaita wadau wote kuliweka sawa kabla ya kutinga nayo bungeni Aprili, mambo mengine yatakayoendelea kuangaliwa kwake ni pamoja na:

  a. Pinda Leadership style and frame (Theories X and Y tools).

  b. Whether Pinda is already at the Plateaue of his performance or not (Goal-setting & Abraham Maslow's Theory of Needs)

  c. Jibu kama Mhe Pinda ni Innovative, Proactive or not

  ... na mjadala wa Uwezo Tunao family bado unaendelea juu ya kiongozi huyu kabla ya kuingia kwenye kuwachambu with a brutally critical mind mtu yeyote ambaye amewahi kutajwa kutamani kuwa kiongozi wetu ama wa kisiasa au technocrat kinamna fulani hivi.

  Nyote mnakaribishwa kwenye huu mkutano endelevu wenye lengo la kukosoa hadi wale tunaowapenda ndani ya CHADEMA chenyewe ili kila mmoja aweze kupata marejesho jinsi tunavyomuona na mambo gani yafanyike huruka vihunzi kadhaa kuelekea kwenye mafanikio maridhawa kwa Wa-Tanzania tulio wengi.
   
Loading...