CHADEMA yaichanganya CCM vijana wake wabakia kushindana kupanda bajaj

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,461
Baada ya chama cha mapinduzi kuelemewa na kashfa za wizi na ufisadi wa mali ya umma huku vijana wake na mawaziri wenye umri mdogo wakiwa wananuka rushwa na kuwa na vito vya thamani kwa haramu, sasa wamechanganyikiwa na kuanza kutaka kurubuni wananchi kuwa nao ni sawa na wao kwa kuanza kushindana kutumia usafiri wa masikini na watu wa kipato cha chini baada ya serikali ya CCM kuuza na kufilisi mashirika yote ya usafiri salama ndani na nje ya majiji kama UDA, reli, mabasi nk

Vijana hawa wakiongozwa na Mbunge wa bumbuli Bwana January Makamba na Mbunge wa tabora hamisi Kigwangala wameonekana wakipost kwa nyakati tofauti picha wakiwa wanatumia usafiri wa bajaj ili kuwaridhisha watanzania kuwa wako nao.

Kama kweli wana nia njema ya kusaidia masikini badala ya kuwasanifu wauze mali zao zote na magari yao wanunue magari ya wagonjwa ili yawasidie akina mama na wazee kufika hospitali mapema badala ya kuzalia njiani na watoto kufa.

Kama kweli wanauchungu na watanzania warudishe fedha za kifisadi walizozipata kutoka kampuni za madini, mikataba mibovu na posho haramu walizovuna tangia wakiwa watumishi wakawaida serikalini.

Kama kweli wanauchungu na wananchi wakaishi majimboni mwao na watoto wao watumie shule, hospitali na huduma zote za jamii zilizoko kule badala ya wao kugeuka kuwa kina masanja.

Inauma sana mtu mzima kuchezea akili za watu wenye shida za kweli na mahitaji. Umasikini wa Tanzania unaletwa na usanii wa viongozi kama hawa.

ni wajibu wa kila mtanzania kumwogopa kama ukoma kiongozi yeyote anayetumia umasikini wetu ili kututawala huyu ni mtu hatari sana kuliko njaa. Kwani njaa inaweza kukuuwa ila huyu atakutesa wewe na kizazi choko daima.

Tanzania hatuhitaji viongozi wanaofikiri kimasikini na kutaka kutushikamanisha na umasikini hatutaki. Wenzetu wanawaaminisha watoto wao wataweza mambo makubwa na hawataki watoto wao waishi maisha ya wazazi wao bali bora zaidi naz zaidi ila hawa viongozi wetu tena vijana wanataka tuamini kwenye umasikini, taabu, dhiki na ajali.

Naamini kiongozi ni mfano, kioo, mwanga, na njia ya jamii. simtaki kiongozi atakayeifundisha jamii umasikini kwa mtaji wa kupigiwa kura.

Raisi anayehubiri umasikini ni wa CCM ndio maana kila mara wanasema hawajui umasikini wetu.

Mmeuwa UDA mkaleta bajaj leo mnazisujudia : hatuzipendi tunazipakia kwa sababu hatuna jinsi.

Chief Mkwawa
Umasikini ukienziwe unadumu. kataa umasikini na kataa usanii wa Viongozi wa CCM
 

Man 4 M4C

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
743
114
Hawa wanafiki tena wakubwa mno, Hamisi tuambie umewasaidiaje watanzania wa Nzega kunufaika na Resolute (Mgodi) ambao kimsingi mwezi huu desemba wanaufunga???? Umejiandaa kufunika mashimo?? January wewe ndio kabisa, dada yako mwamvita kajenga mjumba wa bilioni zinakaribia 3 pesa hiyo kaitoa wapi??? Nin yi kupanda bajaji ni kuwasanifu watu, njooni mpande na daladala za dsm kwa mwezi mzima na wakati mvua inashenya muibiwe kidogo, mkutano na mitaro ya maji machafu kidogo, mkutano na waporaji kidogo ili mpate ali halisi ya kitaa:majani7::majani7:Bajaji mnajidai kupanda mkiona jamu na mna haraka ya kuwahi kumbi za maraha:majani7:
 
Dec 3, 2012
55
20
Mtaona vioja chungu mzima till 2015... Usishangae kumkuta ... Vyoo vya stendi, madai yake anaonyesha uzalendo!! Teh teh ..Mie nasema SIASA ni mithili ya mchezo wa chooni 'mende akikwepa kuangukia... Huku akitaka kufaidi kilichomo...'
 

Lwesye

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
5,292
1,137
Utapeli wa kisiasa kwa vijana wa CCM ndio mtaji wao na wananchi nao wamejitegesha kupokea utapeli wao si walaumu wapanda bajaji na walaumu watanzania wanaojigeuza mazumbukuku kukubali kutapeliwa na hawa makanjanja wa CCM mchana kweupe kwa vibook viwili tuuh tuna safari ndefu
 

Bob G

JF-Expert Member
Oct 5, 2011
2,351
447
Huu ni utapeli wa kijinga sana kwa wasaka umaarufu wa kitoto. Watu wa aina hii ndo wa hovyo walituambi huyu akikaa kwenye noti eti atapendeza. Ana sura nzuri. Sasa tunaumia
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,712
7,153
kigwa badala ya kutetea idara ya afya kama mtaalam amebaki kupanda vibajaji utadhani yuko kwenye kuact muvi ya kiindi
 

ngwendu

JF-Expert Member
Jun 7, 2010
1,965
173
Hawa wanafiki tena wakubwa mno, Hamisi tuambie umewasaidiaje watanzania wa Nzega kunufaika na Resolute (Mgodi) ambao kimsingi mwezi huu desemba wanaufunga???? Umejiandaa kufunika mashimo?? January wewe ndio kabisa, dada yako mwamvita kajenga mjumba wa bilioni zinakaribia 3 pesa hiyo kaitoa wapi??? Nin yi kupanda bajaji ni kuwasanifu watu, njooni mpande na daladala za dsm kwa mwezi mzima na wakati mvua inashenya muibiwe kidogo, mkutano na mitaro ya maji machafu kidogo, mkutano na waporaji kidogo ili mpate ali halisi ya kitaa:majani7::majani7:Bajaji mnajidai kupanda mkiona jamu na mna haraka ya kuwahi kumbi za maraha:majani7:
sasa dada yake kaingiaje humu tena? poor.
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,550
6,676
Unafiki Unafiki, aliahidi watanzania kuleta neema kwa watu wakipato cha chini kuangalia upya upandishaji kodi za maofisini na majumbani baada ya kulamba uwaziri hatumsikii tena( Ni huyu Makamba JR
 

sokoinei

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,832
559
Nikiona nguo yakijan nahisi kutapika,yaan ingekua dunia yangu!!nimechoka sanaaa sijisikii hata kuchangia kifupi walaaniwe na waumbuliwe muda mfupi ujao aamiii
 

malaka

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
1,328
375
na bado sio muda mwingi mtaanza kuingia bungeni na kandambili. wanafki tu. Kama hata wameshindwa kuuza magari kugeuza ambulnc basi wayatoe viti vya katikati ziwe ambulanc bubu kwa muda,
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom