Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Updates
=====
CHADEMA imeibwaga serikali mahakamani kwa kushinda Rufaa ambayo ilikatwa na DPP kutaka kwamba Mbowe na Matiko walikiuka dhamana yao hivyo wawekwe mahabusu.
Kesi yao itaendelea kama kawaida ....
Faili lao litapelekwa Mahakama kuu ili wapatiwe dhamana Mahakama Kuu...
Leo watarudi mahabusu
Habari zaidi...
Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam leo, Ijumaa, imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko.
Hata hivyo, mahakama hiyo imeelekeza jalada la kesi hiyo kurudishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikiliza rufaa ya Mbowe kuhusu kufutiwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Novemba 23, 2018.
Mahakama iliwafutia Mbowe na Matiko dhamana baada ya wawili hao kudharau maamuzi ya mahakama. Mbowe alishindwa kuhudhuria mahakamani November 8, mwaka jana kwa maelezo kuwa alisafiri kwenda Afrika Kusini kwa matibabu.
Habari zaidi, soma=>Kutoka Mahakama Kuu, Dar: Mwendelezo wa Rufaa ya dhamana ya Freeman Mbowe na Ester Matiko yaendelea kusikilizwa - JamiiForums