CHADEMA yaibwaga CCM Arumeru Mashariki; CCM Yakubali kushindwa (Zaidi ya kura 6,000)

Nimefurahi sana kwa kijana Joshua kushinda ubunge. Mchango wangu wa kifedha kwa ajili ya kampeni umefanya kile kilichokusudiwa.

Sasa ngoja nijipongeze kwanza na ze laga mbili tatu za ndovu.
 
Ama kweli inaonekana the majority of jamii forums members ni wafuasi wa chadema. Peoplesssssss poooooooower
 
Kazi yako ya kwanza Mbunge unasema anaanza kutekeleza ahadi ya kufuatilia visima vya msaada ulivyoahidiwa na Ndesamburo. Huna mawazo na mikakati mikubwa zaidi ya maendeleo kupitia misaada? Isitoshe, sitaki maji ya visima, siko karne ya 19.

Kazi ya pili on your agenda, kuanzisha mfuko wa Mbunge wa kusaidia Yatima na kina Mama. Again, small thinking, such insidious Matonya-ism.

Sasa wewe ulitaka afanyeje wakati CDM haina serikali? Tumewasikia wenyeserikali wakisema, kama jimbo linaongozwa na mbunge wa upinzani basi wao watachelewesha maendeleo kwa makusudi. Kwauhakika zaidi, bofya hapa: CCM Arumeru Mashariki - YouTube
 
Natamani utokee uchaguzi mdg tena sehemu nyingine tuzidi kuongeza majimbo. Watanzania wanazidi kuamka sipati picha 2015
 
Waliojiandikisha ni 120,000 na waliopiga kura ni 60,000 - hapa kuna tatizo la msingi. Utaratibu wa kutunza na ku-update dafatari la wapiga kura unahitaji kuboreshwa kama sio kuangaliwa upya. Inawezekana wapiga kura halali hawafikii hata 100,000 lakini hiyo idadi ya 120,000 imewekwa makusudi ili ukipatikana mwanya wajanja wajazie! just thinking aloud!!:shock:
 
Hongera sana kwa CHADEMA kwa ushindi huu mnono....

Hakika ushindi huu ni wa halali kabisa na ni fundisho kubwa sana kwa CCM kuelekea mwaka 2015....

Kiukweli CCM kama chama kinapaswa kujitathmini na kuangalia ni wapi kinateleza maana kwa hali ilivyo matokeo haya ya uchaguzi wa Mbunge wa Arumeru Mashariki na yale ya Udiwani katika kata za Kirumba, Kiwira, Lizaboni na Msambweni ni kiashirio kwamba sasa Anguko la CCM linakaribia....

Kwangu mimi CCM ilishindwa uchaguzi mara baada ya kura za maoni kumalizika....Ikumbukwe kwamba mara baada ya mchakato wa kura za maoni kuanza ndani ya CCM kule Arumeru na baada ya Siyoi Sumari kushinda na baadae matokeo kubatilishwa na suala hili kupelekwa CC ya CCM nilitegemea CC ingeliondoa jina la Siyoi kwa kujihusisha na vitendo vya Rushwa.....CC hawakufanya hivyo na badala yake walimuacha Siyoi ashiriki uchaguzi wa pili wa kura za maoni(kwa kumuogopa EL) na kweli alishinda licha ya uchanga na udhaifu wake katika tasnia ya siasa....

Sababu nyingine iliyopelekea CCM kushindwa ni vijana....CCM ya sasa imejitenga sana na vijana....CCM ya sasa inakumbatia zaidi wazee na sijaona hatua zozote za makusudi ilizoziweka katika kuwa karibu na vijana...Asilimia kubwa ya vijana wenye nafasi ndani ya CCM kwa sasa ni watoto wa vigogo ambao waliwahi kuwa ama bado ni viongozi ndani ya CCM na serikalini kwa sasa....Tatizo la ajira kwa vijana pia ni mojawapo ya kitu kilichoiponza CCM...Siku hizi hakuna hata ule utaratibu wa kufungua mashina ya vijana wakereketwa wa CCM....CHADEMA wapo karibu zaidi na vijana na wanaonesha kuwajali na kuwaamini kiasi cha kuwapa nafasi katika nafasi na shughuli mbalimbali za kichama...

CCM pia imeshindwa Arumeru kwa sababu ya kushindwa kutatua/kuondoa kero mbalimbali(sugu) zinazowakabili wananchi hasa kero ya maji,umeme sehemu vijijini pamoja na ugumu wa maisha...Kwa muda mrefu CCM imekuwa ikienda kinyume na sera yake ya 'Maisha bora kwa kila Mtanzania'....Nusura pekee ya CCM mwaka 2015 ni kutekeleza ahadi zake zilizopo katika Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010 ambazo kimsingi nyingi ni za kinadharia(hazitekelezeki) na hazitatekelezeka kwa wakati...

CCM imeshindwa pia kutokana na udhaifu wa mgombea wake ukimlinganisha na yule wa CHADEMA JOSHUA NASARI....NASARI pamoja na umuri wake mdogo ni mahiri sana katika kujenga hoja na anaweza kuiteka hadhira iliyo mbele yake.....Huyu kijana ni hazina kwa taifa na CHADEMA wanapaswa kumtunza na kuendelea kumjenga kisiasa na kiuongozi ili aje kuwa kiongozi mahiri wa Taifa hili....

CCM pia imeponzwa na makundi....Makundi yaliyopo ndani ya CCM bado ni tatizo na yataendelea kukigharimu chama endapo hatua madhubuti hazitachukuliwa....Pia kitendo cha CCM kuendelea kuwakumbatia watuhumiwa wa ufisadi ni sababu nyingine ambayo inasababisha makundi ndani ya chama kiasi cha kudhoofisha chama kwani badala ya kupanga mikakati ya kukiimarisha chama CCM wao wanajaribu kuunganisha makundi ....

Kingine kinachoiponza CCM ni kubebana....Kwa hali ilivyo Arumeru Mashariki mwana CCM aliyekuwa na nguvu ya kupambana na NASARI ni WILLIAM SARAKIKYA....SIYOI hakuwa na hana ubavu wa kupambana na NASARI....Lakini CCM kwa kutojifunza makosa waliyofanya mwaka 2010 waliendelea na utaratibu uleule wa kubebana kwa kulazimisha kumteua SIYOI mtu ambaye hakuwahi kushiriki kwenye siasa za ushindani hata siku moja na alipewa kwa sababu tu ni mtoto wa marehemu Jerry na pia ni kwe wa EL....

Uchaguzi huu wa Arumeru Mashariki pia ni salamu kwa EL kwamba ana safari ndefu katika kutimiza ndoto yake ya mwaka 2015.....Na imedhihirisha kwamba hana nguvu ndani ya CCM na Tanzania kama watu aina ya akina Pasco wanavyodhani....Tanzania na CCM ni zaidi ya EL...

Nadhani bwana Pasco atakuwa anaona aibu sana kwa ***** kama huu hapa chini aliounadika siku za nyuma na mimi nikamjibu.....

Psco alisema hivi:

Arumeru is done!, kinachoendelea sasa ni kukamilisha tuu taratibu!. Wameru ni watu wenye msimamo, uamuzi wamchague nani, umeishafanyika hivyo hautegemei kampeni yoyote!.

Kama ni kamanda yule yule aliomba kura kwa watu hao hao huku akishindana na kivili cha mahituti kitandani, na akatoswa, what chances does he stand now?,
Next....?.

Nami nikamjibu hivi:

Kuna msemo unasema 'Watanzania si wajinga tena'....So CCM tusitegemee mteremko hapa.....

Binafsi nilitegemea kwenye hatua ya awali ya kura Sioi Sumari(kama kweli anakubalika kutokana na kukubalika kwa baba yake) angepata asilimia 100 kama sio 51 ya kura za maoni....Lakini cha kushangaza alipata asilimia 30+ tu ya kura...Hii ina maana alikuwa hakubaliki hata ndani ya CCM wilayani Arumeru......Kitu ambacho ni hatari sana maana nilitegemea angepata ushindi wa kishindo.....Hayo masuala ya kwamba baba yake alishinda akiwa kitandani so na mwanaye atashinda hayana nafasi na tusiyape nafasi kabisa maana Jery Sumari na Sioi Sumari ni watu wawili tofauti na mbaya zaidi huyo Sioi alikuwa hajishughulishi na mambo ya siasa(ameibuka mara tu baada ya baba yake kufariki)......Sina uhakika kama Wameru wote wana mawazo finyu kama haya unayotaka tuyaamini kwamba wanaendekeza mambo ya kurithishana,kwamba wanamchagua mtu kwa kujuana na si kwa kuangalia sera/Ilani ya chama chake wala uwezo wake....Hili litakuwa ni TUSI kubwa sana kwa Wameru na kama CCM wanataka Sioi ashinde wasijaribu kutumia ama kuitegemea dhana hii mbaya na chafu........

Sina uhakika(pamoja na kuwa ni Mwanasheria) na uwezo wa Sioi wa kumiliki jukwaa la kisiasa(kuongea kwenye haliki kubwa ya wananchi wakati wa kampeni) kama ilivyo kwa mpinzani wake wa karbu Joshua Nasari,...Huyu bwana mdogo anaongea na ana uwezo mkubwa sana wa kulimiliki Jukwaa na pamoja na kushindwa kwa zaidi ya kura 11,000 na Jery Sumary,huyu kijana alionesha kwamba anao uwezo mkubwa wa kuhimili siasa za ushindani hasa ukizingatia kwamba alikuwa akishindana na mtu ambaye pamoja na kwamba ni kama baba yake pia alikuwa ni mwanasiasa mzoefu,Mbunge aliyemaliza muda wake,Naibu Waziri na pia Mzazi mwenza wa aliyepata kuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa.....Pamoja na hayo yoote huyu kijana aliweza kupata kura nyingi kiasi cha kuwa tishio kwa Jerry Sumari....

Ninawashauri wana CCM wasibweteke na waachane na hii dhana mbaya na potofu ya Pasco ya kusema eti 'Arumeru is Done' kisa tu Mkwe wa Lowassa ameshinda kuiwakilisha CCM.....Haiwezekani eti mtu ambaye hakubaliki ndani ya chama chake(kwa matokeo ya awali na hata ya leo) eti ndio apewe nafasi kubwa ya kumshinda kijana mahiri wa aina ya Nasari......Nakataa.....Cha msingi ni CCM kujipanga kwa ajili ya mapambano(ya kisera) na si kubweteka eti watashinda kiulaini.......Tanzania ya sasa si ya mwaka 1995 wala 2000.......Ikumbukwe kwamba mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 mkoa wa Arusha hasa wilaya za Arusha mjini na Arumeru umekuwa ni ngome kuu ya CHADEMA na maandamano na hekaheka za kisiasa ambazo zimekuwa zikitokea mara baada ya uchaguzi huo zimeifanya CHADEMA izidi kupata wafuasi na wanachama katika wilaya za Arusha mjini na Arumeru hivyo CCM tusitegemee kushinda kiulaini kama Pasco anavyojaribu kupotosha......Kama Lowassa anakubalika sana Arumeru na ndani ya CCM sidhani kama mkwewe Sioi angeweza kupata asilimia 30+ ya kura za maoni za awali na hata uchaguzi wa leo inajulikana wazi kwamba Sioi ameshinda kutokana na nguvu ya ziada iliyotumika ikiwa ni pamoja na matumizi makubwa ya fedha ambapo imeripotiwa kwamba TAKUKURU wamewakamata watu watatu(03) ambao wanadaiwa ni wafuasi wa Sioi wakijihusihsa na vitendo vya utoaji wa Rushwa kwa wana CCM...

CCM inapaswa kugangamala na kujipanga maana kazi iliyopo mbele ni ngumu hasa tofauti na Pasco anavyotaka tuamini....

Wakatabahu......

Bala.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...evu-anguko-lililo-wazi-ccm-3.html#post3416629


Mwisho niwatakie tena watani zangu wa CHADEMA ushindi huu mnono na mtamu....Endeleeni kukaza uzi na mjipange kwa mwaka 2015(na sisi tunajipanga)...Msibweteke.......Tanzania yenye neema inawezekna
 
Huo ni mwanzo tu bado cheche zenyewe 2015, Chadema tusonge mbele na tuepuke wenye nia mbaya kutuvuga kama wanavyofanya kwa CUF na NCCR
 
Back
Top Bottom