CHADEMA yaibwaga CCM Arumeru Mashariki; CCM Yakubali kushindwa (Zaidi ya kura 6,000)

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Hatimaye Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Arumeru amemtangaza Bw. Joshua Nassari kuwa Mbunge Mteule wa jimbo hilo kufuatia ushindi wake mnono dhidi ya mgombea wa CCM Bw. Siyoi Summari. Joshua Nassari amepata kura 32,972 sawa na asilimia 54.91 ya kura zilizopiwa. Hii inaendana na makisio yangu ambayo yalitabiri ushindi wake wa karibu asilimia 50!

[video=youtube_share;zjUI5AbO-Jk]http://youtu.be/zjUI5AbO-Jk[/video]

Mtandao wa JamiiForums waweza kutangaza kwa uhakika kabisa kutokana na vyanzo makao makuu ya Jimbo huko Arumeru Mashariki kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda uchaguzi mdogo ambapo mgombea wake Bw. Joshua Nassari ameibuka kidedea baada ya kumbwaga vibaya mgombea wa CCM Bw. Siyoi Sumari. Matokeo yanaonesha hadi hivi sasa baada ya zaidi ya asilimia 80 ya vituo vyote kuripoti CDM imeshinda kata 14 dhidi ya 3 za CCM.

Chama cha Mapinduzi tayari kimekuballi kushindwa na kutoa pongezi kwa mgombea wa CDM.

CDM imeshinda kwa zaidi ya kura 6000

MATOKEO OFFICIAL:

Kura halali - 60038

CHADEMA 32,972 - Joshua Nassari (Mbunge Mteule)
CCM 26,757 - Siyoi Sumari

Vyama vingine:

AFP 139
UDP 18
TLP 18
DP 77
UPDP 22
NRA 35

My Take:
Bila ya shaka Uongozi wa taifa wa CDM hauna sababu ya kujiuzulu kwa wakati huu! Upepo umevuma upande wao na mtumbwi unaelekea kwenye ushindi 2015!

Kutoka kwa Zitto (FB)

zitto-status.jpg

attachment.php
 
Mtandao wa JamiiForums waweza kutangaza kwa uhakika kabisa kutokana na vyanzo makao makuu ya Jimbo huko Arumeru Mashariki kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda uchaguzi mdogo ambapo mgombea wake Bw. Joshua Nassari ameibuka kidedea baada ya kumbwaga vibaya mgombea wa CCM Bw. Siyoi Sumari. Matokeo yanaonesha hadi hivi sasa baada ya zaidi ya asilimia 80 ya vituo vyote kuripoti CDM imeshinda kata 14 dhidi ya 3 za CCM.

Chama cha Mapinduzi tayari kimekuballi kushindwa na kutoa pongezi kwa mgombea wa CDM.
source plz, maana nsije nkawa broken herted baadae haya magamba si unayajua mzee, hawakawii kusema hizo kata zilikuwa na wapiga kura wachache
 
Mtandao wa JamiiForums waweza kutangaza kwa uhakika kabisa kutokana na vyanzo makao makuu ya Jimbo huko Arumeru Mashariki kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda uchaguzi mdogo ambapo mgombea wake Bw. Joshua Nassari ameibuka kidedea baada ya kumbwaga vibaya mgombea wa CCM Bw. Siyoi Sumari. Matokeo yanaonesha hadi hivi sasa baada ya zaidi ya asilimia 80 ya vituo vyote kuripoti CDM imeshinda kata 14 dhidi ya 3 za CCM.

Chama cha Mapinduzi tayari kimekuballi kushindwa na kutoa pongezi kwa mgombea wa CDM.

Mkuu MM,
heshima mbele! Unapodai "CCM Kimekubali kushindwa," nani katika CCM aliyekubali kushindwa? Nape, Mwigulu au nani?
 
weeeeeeeeeeeeeeeeee achana na thithiemu yanaweza kubadilika anytime.....
Kama ungekuweo usingesema lolote....
Nilikuwa Arumeru tangu saa 9 mchana..aiseeee ni raha sanaaaaaaaaaa
Yan unajihisi kama umekombolewa na matatizo yako yooooote....
Chadema wanatisha sana....
Mabasi na magari yote toka moshi na dar na njia hiyo wanatembea na vidole viwili nje ya madirisha....watu wana raha sana....Hakuna CCM hata mmoja...
Kuna jamaa kakamatwa na mfuko wenye karatasi za kura na tindikari....kamwagiwa hiyo tindikari machoni na hali yake ni mbaya sana...
Chadema mpooooooooooooooooooooooooooooooooo?????!!!!??
 
Tuombee iwe hivyo maana magamba ni hatari kupnyeza kura chafu na kwa kuwa tayari yameshatumia ccmpolisi kutawanya watu vituoni ili wawezeshe kuchakachua
 
173 Reactions
Reply
Back
Top Bottom