Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Hatimaye Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Arumeru amemtangaza Bw. Joshua Nassari kuwa Mbunge Mteule wa jimbo hilo kufuatia ushindi wake mnono dhidi ya mgombea wa CCM Bw. Siyoi Summari. Joshua Nassari amepata kura 32,972 sawa na asilimia 54.91 ya kura zilizopiwa. Hii inaendana na makisio yangu ambayo yalitabiri ushindi wake wa karibu asilimia 50!
Mtandao wa JamiiForums waweza kutangaza kwa uhakika kabisa kutokana na vyanzo makao makuu ya Jimbo huko Arumeru Mashariki kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda uchaguzi mdogo ambapo mgombea wake Bw. Joshua Nassari ameibuka kidedea baada ya kumbwaga vibaya mgombea wa CCM Bw. Siyoi Sumari. Matokeo yanaonesha hadi hivi sasa baada ya zaidi ya asilimia 80 ya vituo vyote kuripoti CDM imeshinda kata 14 dhidi ya 3 za CCM.
Chama cha Mapinduzi tayari kimekuballi kushindwa na kutoa pongezi kwa mgombea wa CDM.
CDM imeshinda kwa zaidi ya kura 6000
MATOKEO OFFICIAL:
Kura halali - 60038
CHADEMA 32,972 - Joshua Nassari (Mbunge Mteule)
CCM 26,757 - Siyoi Sumari
Vyama vingine:
AFP 139
UDP 18
TLP 18
DP 77
UPDP 22
NRA 35
My Take:
Bila ya shaka Uongozi wa taifa wa CDM hauna sababu ya kujiuzulu kwa wakati huu! Upepo umevuma upande wao na mtumbwi unaelekea kwenye ushindi 2015!
Kutoka kwa Zitto (FB)
[video=youtube_share;zjUI5AbO-Jk]http://youtu.be/zjUI5AbO-Jk[/video]